Ndoa ya rafiki yangu imedumu miezi miwili tu! -kweli ndoa ni mtihani?

Mkuu somo la tofauti ya feminine na feminist please
I am glad you asked.

Feminine ni neno linaloashiria tabia fulani hivi ambazo zimepitishwa kuwa ni za kike.

Mfano. Kwa jamii yetu na jamii nyingi, kuwa feminine kunaendana na kuwa na stara na haiba fulani za kike, labda kupenda maua, kupenda kupika, kupenda kushona, kupenda kulea watoto wachanga, kupenda uturi na marashi ya kike, kupenda mambo ya design na kupanga rangi vitu vya urembo, kupenda vivazi vya kike, kupenda kupendeza wanaume na mambo kama hayo.

Kitamaduni tumejikubalia hivyo ndivyo mwanamke anavyotakiwa kuwa.

Kwetu, kiutamaduni, ukiona mtoto wa kiume anapenda kucheza na midoli ya watoto kama anailea, anapenda kudarizi maua, unaweza kupata shaka kuwa labda "huyu mtoto si riziki".

Feminism ni kitu tofauti. Feminism ni falsafa ya wanawake kuwa na haki sawa na wanaume kimizania. Na hii si lazima mtu awe mwanamke kuwa nayo, kwa sababu hata mwanamme anaweza kuwa na falsafa hii.

Na kwenye feminism, kuna falsafa ya kukataa "gender roles". Habari za kusema mtoto wa kike ndiye anatakiwa kupenda kupika na kuosha vyombo, mtoto wa kiume anatakiwa kupenda hesabu ma mpira zimekataliwa. Watoto wote wana haki sawa kupenda kupika, kuosha vyombo, hesabu na mpira pia.

Sasa ukielewa hilo, ndipo unaweza kuelewa kwa nini Feminism inaweza kukataa characteristics za kuwa feminine.

Kwa sababu, kimsingi, kuwa feminine mara nyingine - si mara zote, kuna sehemu Feminism ina overlap na kuwa feminine- mara nyingine kunaendana na gender assigned roles, na gender assigned roles, habari za kusema "wanawake wanatakiwa kupika na wanaume wanafanya kazi za umakenika wa magari", zinapingana na Feminism, kwa sababu Feminism inampa ihuru mwanamke kuchagua kazi au ibterests anazotaka kulingana na matakwa yake nanuwezo wake, si kulingana na anavyopangiwa na jamii.

Hiyo ni very basic, in a nutshell, mimi mwenyewe najifunza si mtaalamu sana.
 
Back
Top Bottom