.
. mtu anajiunga mwenyewe kwa hiari na mtu asiyempenda labda tu alitamani visenti vyake siku ya siku anatamani atoke but the task is not easy where now problems start.Kumbe ndoa kama "pingu za maisha" inazaliwa pale wawili wanapoweka makubaliano yao kwa hiari mbele ya wajumbe halali. Hicho ndiyo KIINI
ndoa ni upendo, kama sio upendo hiyo sio ndoa bali ni ndoana.
Leo nasoma gazeti fulani, nikashangaa kuona kichwa cha habari:
NDOA SI UPENDO!
Nimeshangaa sana... Je wanaJF, NI KWELI NDOA SI UPENDO?
Nafikiri ndoa ni zaidi ya upendo... yaani si upendo peke yake unaowafanya watu wakaishi katika ndoa kuna chachu kibao ambazo lazima ziwepo ili ndoa idumu na iwe na amani na katu chachu hizo hazihusiani na upendo. Unaweza ukawa unampenda mtu kufa but kuna vitu anavyo ambavyo utajikuta unashindwa vumilia unaamua kubwaga manyanga.
Ndio maana huwa tunashuhudia kuna mtu anamwacha mwenzi wake ikingali bado anampenda.
Hee,
Hii ni mpya tena! Kumwacha mtu wakati bado unampenda?
Ni shida gani ewe MwanajamiiOne zitakazokupelekea umwache mtu ungali bado unampenda?
Ndoa ni upendo.
wanawake labda ndoa si upendo. Maana wanavumilia manyanyaso mengi sana ndani ya ndoa nyingi ikiwemo vipigo, tuhuma za kutembea nje hata pasipo na ushahidi wa kutosha, matusi na karaha mbali mbali.
Manyanyaso wanayoyapata na kuendelea kuyavumilia yamenishangaza sana hasa ukitilia maanani wengi wanaonekana ni waajiriwa ambao wanaweza kujisupport wenye ingawaje katika hali ya kujibana sana.
cha kushangaza ni kuendelea kuwemo kwao katika ndoa hizo hata kama kuna ushahidi tosha kwamba mapenzi ya wenzao kwao yamepotea kabisa na kila siku wanaishi maisha yasiyokuwa na furaha yoyote na wakati mwingine kuishi maisha yaliyojaa woga dhidi ya wenzao kutokana na vipigo na manyanyaso wanayoyapata.