Ndoa ndoano!

Esperance

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
364
84
Habar za masiku wanajamvi la MMU. Me bado hali yangu ni tete na hiki kitambi. Leo nikiwa clinic nimepata kisa cha kusikitisha, kuna dada mjazito alikuwa analia.

Katika maongezi akaniambia ana mimba sio ya mume wake ila kamweleza ukweli mumewe kasema atamtunza tu huyo mtoto ila aandikishwe clinic kwa jina la mumewe. Mwenye mzigo nae kasema aandikishwe clinic kwa jina lake.

Mumewe kamsamehe kwa sababu alikuwa anamtesa mkewe na kulala nje. Sasa amejirudi. Na mume hataki huyo mtoto akizaliwa aitwe kwa jina la baba mwingne. Leo ameshindwa kuanza clinic. Tumsaidie kwa mawazo.
 
Habar za masiku wanajamvi la MMU. Me bado hali yangu ni tete na hiki kitambi. Leo nikiwa clinic nimepata kisa cha kusikitisha, kuna dada mjazito alikuwa analia. Katika maongezi akaniambia ana mimba sio ya mume wake ila kamweleza ukweli mumewe kasema atamtunza tu huyo mtoto ila aandikishwe clinic kwa jina la mumewe. Mwenye mzigo nae kasema aandikishwe clinic kwa jina lake . Mumewe kamsamehe kwa sababu alikuwa anamtesa mkewe na kulala nje. Sasa amejirudi. Na mume hataki huyo mtoto akizaliwa aitwe kwa jina la baba mwingne. Leo ameshindwa kuanza clinic. Tumsaidie kwa mawazo.
Ndio akome kutoka nje ya ndoa, ngoja nisubiri comments
 
Kwani hapo clinic wanataka nini? Kama ni jina la mume basi awape la mume wake....na kama wanataka la aliyeshiriki kwenye huo ujauzito basi ampe jina la huyo 'kidumu'.
 
Sasa jamani, atamwandikishaje jina la huyo mwingine kama bado anapenda kuendelea kuishi na mumewe??!!!! Mimi nafikiri kama ana mpango wa kuachana na mumewe basi amwandikishe huyo nyumba ndogo, lakini kama bado anapenda kuendelea kuishi na mumewe basi amwandikishe mumewe!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hapo pagumu sana, ndoa kweli ndoano....
aandikishe jina la ukoo wake huyo mke, itakuwa fair treatment kwa wote watatu...mke, mume na mwizi.
 
Kwani hapo clinic wanataka nini? Kama ni jina la mume basi awape la mume wake....na kama wanataka la aliyeshiriki kwenye huo ujauzito basi ampe jina la huyo 'kidumu'.
tatizo litakuja kwenye cheti mtoto akizaliwa. Na mwenye mzigo hatak mtoto apotee.
 
Hebu arudi nyumbani kwanza akaongee na mume wake kuhusu matakwa ya mwenye mtoto, na asikie anasemaje coz huyo wa nje si alijua wewe ni mke wa mtu? inabidi akubali matokeo ila cha msingi ajue kuwa ana mtoto kwako regardless anaitwa kwa jina la baba gani
 
hapo pagumu sana, ndoa kweli ndoano....
aandikishe jina la ukoo wake huyo mke, itakuwa fair treatment kwa wote watatu...mke, mume na mwizi.

Hapo humuongelei huyohuyo mtu mmoja!?? mwizi ni huyo wa mke kwa mtazamo wangu!

Back to the topic:
Yesu rudi tu mapema....
 
Mmmmh hii ngumu,lakini ilikuepusha aibu ni kumwandika jina la mumewe,kumwandika jina la mwizi sio vizuri
 
Why amweleze mwizi ako na mimba bwana? Alikosea hapo, ila kukata fitna akate mawasiliano yake na njemba ya nje, aandike jina la mumewe na huyo wa nje hata aende mpaka kuzimu km mume ameikubali mimba bs hana chake, kitanda hakizai kharamu bwana. ILA MAISHA YAKO NA MITIANI SANA JAMANI...!
 
kama anataka kukaa na mumewe basi aandike jina lake...kama anataka kwenda kwa huyo mwivi basi aandikishe jina lake.
 
Hatari lakini salama,ingekuwa busara kwanza kujua msimamo wa huyo mama kwanza yeye kama yeye la sivyo itakuwa Majuto ni mjukuu
 
Hatari lakini salama,ingekuwa busara kwanza kujua msimamo wa huyo mama kwanza yeye kama yeye la sivyo itakuwa Majuto ni mjukuu
huyo mdada alisema anaogopa aibu kwa familia, halaf mkaka mwiz yupo tayar kumchukua ila akavunje ndoa mahakamani.
 
huyo mdada alisema anaogopa aibu kwa familia, halaf mkaka mwiz yupo tayar kumchukua ila akavunje ndoa mahakamani.
​Sasa inavyoonekana hampendi mume ila anaogopa aibu ya familia,wakati kukubali kubeba ujauzito wa mtu mwingine wakati upo kwenye ndoa ni aibu tosha.
 
huyo mdada alisema anaogopa aibu kwa familia, halaf mkaka mwiz yupo tayar kumchukua ila akavunje ndoa mahakamani.

Sidhan kama huyo dada anaupendo wa dhati kwa mumewe, ausikilize moyo wake kwanza na kama kweli anampenda mmewe mtoto amuandikishe kwa jina la mmewe wala asimusikilize huyo mwizi
 
Hapa lazima tuipe kipaumbele principle ya KAIZER Ctrl+Alt+Delete), kote ni aibu bora arudi kwao akajifunze kuwa makini kwenye kuiishi na wanaume. kama ni aibu inayokuja ni zaiidi ya hiyo. Siku anaenda kujifungua atafanyaje? Nani atamsindikiza? Kidumu au mume halali? Kama ni mimi nafikiri ningekata hiyo picha kwa kufunga kilicho changu na kurudi nyumbani.
 
hiyo tisa, kumi ni kwanini unajigijigi na kidumu bila hata kutumia kinga jamani......................?
hii inanichefua sana aaaggghhhrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ama kweli dunia ngumu, na mambo yake ni magumu. Huyu dada mi naona majibu anayo mwenyewe, kwa hiyo mwambie afanye kile anachoona ni sahihi. Kwanza kwa ujasiri alopata wa kumwambia huyo mume wake kuwa ana mimba ya mtu mwingine inatosha kabisa kusema hataki kuishi na huyo mwanaume.
 
Back
Top Bottom