SoC01 Ndoa na Mahusiano: Yupi mke au Mume bora?

Stories of Change - 2021 Competition

Salimu Kajembe

New Member
Nov 5, 2018
4
4
YUPI MKE BORA/MUME BORA (NDOA NA MAHUSIANO)

Lengo kuu la andiko hili ni kwenda kuibadilisha jamii ya watanzania hususan vijana wa kizazi cha leo ilo kuweza kutambua vema dhana halisi ya mahusioano na ndoa na namna ya kuweza kuwa na maamuzi sahihi juu machaguo sahihi kwenye mahusiano yao/ndoa zao ,thaman ya mahusiano waliyonayo /ndoa zao,faida zake kijamii,kiafya na kiuchumi.

Lakini pia makala yangu itajikita zaidi kuelezea madhara makubwa ya kiuchumi,kiafya na kijamii ambayo mtu anaweza kuyapata katika masuala mazima yahusiyo ndoa na mahusiano hususani katika dhana ya kutafuta mke bora na mume bora.

Watu wengi sana wanaingia kwenye mahusano au ndoa kila mmoja akiwa na malengo yake,malengo hayo yamegawanyika katika nyanja tofauti tofauti,watu wanaingia kwenye mahusiano na ndoa ili kutimiza malengo yao zaidi kihisia na kiuchumi.

Watu wengi sana wanaingia kwenye mahusiano na ndoa bila hata kujua nini maana ya hivyo vitu,kwa ufupi sana napenda nielezee maana ya mahusiano,na pia maana ya ndoa japo sio maana rasmi.

Mahusiano ya kimapenzi,ziko maana nyingi Sana za kimahusiano ya kimapenzi,ila kwantamaduni zetu za kitanzania naweza nikaeleza mahusiano ya kimapenzi ni kitendo cha Mwanamke na Mwanaume/msichana na Mvulana kuwa urafiki wa kimapenzi unaoweza kuwapelekea kuzaa watoto na pia kufunga ndoa na kutengeneza familia pamoja.

Ndoa ni makubaliano ya hiari yanayohusu mwanamke na mwanaume kuamua kuishi mapoja kinyumba kama mke na mume mbele ya mashahidi kutoka pande zote Kwa upande wa mwanamke na upande wa mwanaume ,Kwa tamaduni za kitanzania mara nyingi ndoa pia inaweza huhusisha ushahidi kutoka viongozi wa kidini,kiserikali au viongozi wa kimila.

Kuna aina mbili tu za ndoa zinazotambulika, nazo ni ndoa ya mke mmoja, na ndoa ya wake wengi. Aina hii ya ndoa inaruhusu mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja. Kwa mfano, ndoa za kimila na za dini ya kiislam.

MISINGI YA NDOA

1. MUNGU KUWA KIONGOZI WA NDOA
Ndoa au mahusiano ambayo Yana mahusiano ya karibu na Mungu inakuwa na baraka kubwa Sana. Kama Kila mwanandoa au mwana mahusiano atakuwa na uhusiano mzuri na Mungu na atajitahidi kuishi katika maadili ya dini matokeo yake ni kwamba shetani atakaa mbali na Ka shetani akikaa mbali basi upendo wa kweli huongoza ndoa.

Ndoa na mahusiano yenye msingi wa dini huwa na maombi na maombi ni mawasiliano ya wanandoa na Mungu, hivyo kwa kuwa na mawasiliano kati ya Mungu na wanandoa/Walio

2. UPENDO WA KUJITOA
Maisha ya binadamu ni safari ndefu, si sahihi kwamba siku zote Ndoa/Mahusiano vitakuwa na mapenzi yaleyale ya motomoto, au kupendana kule kule kama mwanzo, kiwango cha mapenzi hupanda na kushuka kutokana na kuwa na malezi tofauti na mambo mengine hivyo kusababisha ndoa au mahusiano kupita kwenye wakati mgumu sana, kuna msongo wa mawazo, kuna kukata tamaa, kuna biashara kuharibika, na kuna wakati tu inatokea mume/Me au Mchumba kila mmoja hampendi mwenzake bila sababu, hivi vyote vinahitaji watu wenye Upendo wa kujitoa ili kurudi kwenye mstari.

3. MAWASILIANO
Mawasiliano ni kitu muhimu Sana cha kuzingatia kwenye mahusiano au ndoa, mawasiliaono ya ndani ya nyumba pindi watu wanapokuwa katiribu mfano matukizi mazuri ya lugha za kistaarabu zisizo Kali ambazo zitampendezea Lila mmoja,lakini pia yako mawasiliano ambayo watu wanapokuwa mbali mbali,mfano watu wanaishi mbali mbali mawasiliano ya mara Kwa mara ni muhim Sana kwasababu huyaleta Wana ndoa au wapenzi kuwa karibu zaidi hivyo kuimaisha ndoa/mahusiano na kuepusha mtamanio ya nje.

Kwanini watu wanaingia kwenye mahusiano? Kama nilivyotangulia kusema ,watu wengi wanaingia kwenye mahusiano ii kukidhi mahitaji yao ya kihisia,yaani kukidhi mahitaji ya kimwili kwa mwanamke au kwa mwanaume.Pia watu hujiingiza kwenye mahusiano kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi,hapa ni pale ambapo mtu anavutiwa na hali ya kiuchumi ya mtu flani,hivyo anaona akiwa na mtu huyo kwenye mahusiano itakuwa rahisi kwake kuweza kutatua shida zake kutoka kwa mtu huyo,shida hizo inaweza kuwa katika kukidhi mahitaji ya kupata chakula,kukidhi mahitaji ya kodi za nyumba,mavazi,ada za masomo na mahitaji mengine ambayo yanahitaji fedha.

Sababu hizo ziko kwa watu wa jinsia zote,wako wanawake ambao wanaingia kwenye mhusiano wakishawishika na vipaumbele hivyo kutoka kwa wanaume,lakini pia wako wanaume wanaongia kwenye mahusiano wakishawishika na vipamumbele hivyo kutoka kwa wanawake ambao wana uwezo wa kifedha kuliko wao.

Kwanini watu wanaingia kwenye ndoa? ziko sababu nyingi sana za watu kuingia kwenye ndoa,sababu kuu ya watu kuingia kwenye ndoa ni kujenga familia,hii inahusu kuzaa watoto na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo yanayohusu uchumi na kijamii pia,lakini pia ziko nasharia zinazoonyesha watu hingia kwenye ndoa ili tu kikidhi takwa la kidini na si vingingivenyo.

Zote hizo ni sababu tofauti tofauti za watu kingia kwenye mahusiano na ndoa kwa wanawake na wanaume pia.

Siku hizi vijana wengi sana wanaingia kwenye mahusiano wakiwa na umri mdogo sana, si hivyo tu hata kwenye ndoa,wako vijana wengi sana wanaingia kwenye ndoa wakiwa na umri mdogo sana, hiyo inafanya kuwepo na ongezeko la idadi kubwa sana ya vijana walio kwenye mahusiano ya kipamenzi na wengine wao kuingia kwenye ndoa za mapema.

Msingi mkuu wa andiko langu ni kujikita zaidi kuelezea namna hali za mahusiano zilivyo sasa,hii inatokana kwamba siku hizi watu wengi wanaojiingiza kwenye mahusiano pamoja na ndoa wanakuwa hawadumu wanaishia katikati hivyo kutengeneza ile dhana ya kupotezeana muda.

Siku hizi si mahusiano ya vijana pekee bali hata watu wazima,aidha iwe mahusiano tu ya kawaida bali hata ndani ya ndoa watu wanashindwa kuvumiliana hivyo hujikuta baada ya muda mfupi tu wanatengana na kujikuta tena wanaenda kuanzisha mmahusiano mengine au kuoa na kuelewa sehem nyingine.

Suala hili limezidi kuwa kubwa sana katika jamii zetu za kitanzania,kutokudumu katika mahusiano kunagusa makundi yote,watumishi,wanafunzi,wasomi,viongozi wa kiserikali,wanasiasa na mpaka watumishi wa dini.

Kiukweli hili limekuwa ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu,changamoto hii inatokana na sababu kwamba siku hizi watu wameshindwa kuwa na uvumilivu kwenye mahusiano/ndoa,watu wanashindwa kuitambua na kuielewa vizuri au Kwa uchache misingi ya ndoa na mahusiano,watu wapaswa kuelewa kwamba kila mtu ana mazuri yake na matatizo yake,kwahiyo watu inabidi wavumiliane kwa yote,kwa mazuri na matatizo pia.

Mfano,unakuta Juma anaanzisha mahusiano na Asha,unakuta Asha anakuwa na sifa nyingi nzuri kama vile maadili mazuri,heshima kwa watu Nk,lakini Asha huyo unaweza kuta kasoro yake inakuwa ni mkali sana, yaani ni mtu wa hasira za karibu,sasa badala ya Juma kumvumilia huku akizidi kumrekebisha taratibu taratibu anaona hafai anatafuta mwanamke mwengine ambae anahisi hilo pungufu alokuwa nalo Asha huyo mwanamke mwengine hatakuwa nalo.

Baada ya kuwa na huyo mwanamke mwengine unakuta kweli hilo tatizo la ukali hana ila ana tatizo jengine la uchoyo,unakuta tena anamuona hafai atafute mwengine ambae pengine hatakuwa na tatizo hilo.Unakuta hali hiyo inaendelea inazidi kuendelea mwisho wa siku mtu anajikuta alishakuwa na mahusiano mengi na yote hakuna manufaa yoyote alonufaika nayo.

Tabia hii ipo kwa wanaume na kwa wanawake pia,lakini si kwenye mahusiano ya kawaida tu bali pia hata mwenye ndoa,watu wengi hawadumu kwenye ndoa kwakukosa uvumilivu kwa wake zao na waume zao huku wakidhani wakiachana basi watapata wengine bora zaidi kuliko walokuwa nao kitu ambacho sio kweli.

Hisia za kuamini kwamba ukiachana na huyo ulokuwa nae utapata mwengine bora zaidi ya huyo sio sahihi, utakuja pata mwingine nae utamkuta na changamoto zake nyingi zaidi na kusema ni bora na yule wa kwanza.

Kwahiyo lengo kuu la andiko hili ni kuisihi jamii ikihusisha makundi yote, vijana, na hata watu wazima,wanawake kwa wanaume waliopo kwenye mahusiano ya kawaida na waliopo kwenye ndoa waridhike na watu waliokuwa nao, ili mahusiano na ndoa viweze kudumu msingi mkuu ni kila mmoja akubali kubeba mapungufu ya mwenzake ili kuweza kuvumiliana, kuwa katika mahusiano ya watu wengi au ndoa nyingi haijawahi kuleta mafanikio, kibaya zaidi ni kwamba mtu utakuwa unajiweka zaidi kwenye hatari kubwa ya kupata maradhi kama "UKIMWI", matatizo ya KISAIKOLOJIA, KUATHIRIKA KIUCHUMI, MIGOGORO ISIYOISHA,WATOTO KUKOSA MALEZI YA WAZAZI WAWILI na kadhalika.

Kwa kumalizia tu, napenda kusemaa kwamba ni matumaini yangu makubwa sana kwamba andiko hili litakwenda fungua fikra za jamii zetu na kuibadilisha mitazamo yao hivyo kuweza kuona kwamba watu walio kwenye mahusiano wanavumiliana, wanadumu hivyo kuweza kutimiza malengo yao ambayo ni kufunga ndoa, lakini pia ni matumaini yangu makubwa sana kwamba andiko hili litakwenda kuongeza chachu na muamko mkubwa sana kwa wale wote walio kwenye ndoa kuona wanavumiliana na ndoa zao kuweza kudumu hivyo kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

Andiko hili limeandaliwa na kuandikwa na Salimu Juma Kajembe.

P O BOX 11077, DODOMA, TANZANIA

Ahsante.... TEAMO!
 
Back
Top Bottom