WANASAYANSI wamegundua protini maalum iliyomo kwenye ndizi ambayo inazuia wanawake wasiambukizwe ukimwi wakati wa tendo la ngono.
Wanasayansi hao toka Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani wanaamini kwamba ugunduzi huo utasaidia kutengenezwa na kuuzwa dawa za bei nafuu zitakazozuia kuenea kwa ukimwi duniani.
Protini iliyomo katika ndizi huitwa kwa jina la Kitaalamu lectins na kiasili huwemo katika ndizi wakati inapoanza na kuendelea kukua tayari kukomaa na kutumika na walaji. Kemikali zilizomo katika protini hiyo inasemekana husaidia kuzuia mgonjwa kukumbwa na maradhi mengi kufuatia kuambukizwa ukimwi.
Katika maabara protini hiyo iliyosilimishwa kwa jina la BanLec imekutwa ina nguvu sawasawa na dawa mbili zilizopo madukani leo dhidi ya ukimwi.
Kufuatia kuchapishwa kwa matokeo ya utafiti huu katika jarida la 'Journal of Biological Chemistry,' BanLec ina uwezekano mkubwa wa kuwa kinga nafuu na salama zaidi kutumika katika sehemu nyeti za wanawake ili kujikinga na ukimwi.
Ingawa kondomu zinasaidia sana kuzuia ukimwi lakini wanasayansi hao wanasema huwa zinafaa zaidi katika kuzuia maambukizi pale tu zinapotumika bila kuacha na zikatumika kwa namna inayotakikana kitu ambacho sio rahisi kufanywa na wanawake katika nchi zinazoendelea maana hawana sauti sana wakati wa tendo la ngono kama wenzao wa nchi zilizoendelea.
David Marvovitz kiongozi na mwandishi wa taarifa ya utafiti huu anasema kwamba dawa itakayotokana na ndizi itakuwa ni ya muda mrefu na inayotumiwa na mwanamke mwenyewe toauti na ilivyo kondomu ambayo budi ivaliwe na mwanamme pale anapotaka.
Utafiti huo unaelezea kwa kirefu jinsi ambavyo protini ya lectin ilivyo na uwezo wa kushinda VVU. Lectin ni protini inayobeba sukari na ina uwezo wa kugundua wavamizi katika mwili kama vile virusi na kuambatanisha na pathogen.
Watafiti hao wamegundua kwamba BenLec, lectin iliyomo kwenye ndizi inazuia maambukizi ya VVU kwa kuambatana na sukari iliyojaa katika bahasha ya protini ya gp120 kwenye HIV-1 na hivyo kuizuia kuingia kwenye mwili.
Tiba itakayotumia ndizi wanadai wanasayansi hao itakuwa ni ya gharama za chini zaidi kulinganisha na tiba za kupunguza makali ya ukimwi za sasa ambazo hutumia malighafi ambayo si asili. Isitoshe tiba hiyo mpya inaweza kuja na mambo mengine ya ziada kuliko hii ya sasa, wanasema watafiti hao.
'Tatizo la baadhi ya madawa ya ukimwi ya sasa ni kuwa virusi vya ukimwi vinaweza kujizalisha vyenyewe na ksuambaa mwilini zaidi kisha kuwa virusi sugu kutibika,' ansema Michael Swanson mmojawapo wa watafiti hao, ' lakini mbele ya lectin vidudu hivyo haviwezi kufurukuta na husalimu amri na hivyo muathirika kuwa salama kwa muda mrefu na pengine kupona kabisa kama atafuata masharti ya madaktari wake.' {Source: Afrol News }