Maambukizi mapya ya VVU yamepungua kutoka 7% hadi 4.3%

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Imeelezwa kuwa kasi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI imepungua kutoka Asilimia 7% Mwaka 2003 hadi kufikia Asilimia 4.3% Mwaka 2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, akimuwakilisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akiongoza ujumbe wa wageni kutoka Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Msaidizi (PDAS) na Kaimu Naibu Mratibu Mkuu wa masuala ya UKIMWI wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR), Dk Rebecca Bunnell ulipotembelea Mkoa wa Tanga katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Mhe. Waziri Kindamba pamoja na Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya "Gift of Hope" kilichopo Jijini Tanga.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha huduma za afya, hasa katika huduma jumuishi kwa waathirika wa dawa za kulevya na VVU,” amesema Dkt. Magembe.

Aidha, Dkt. Magembe amesema kupitia ufadhili wa PEPFAR Tanzania imeweza kuanzisha vituo tisa vya utoaji wa Dawa ya Methadone kwa waathirika wa Dawa za Kulevya nchi nzima, pamoja na huduma ya kliniki ya kutembea katika vituo saba.

“Tunaishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada wake kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kwa kuendelea kushirikiana katika uboreshaji wa huduma za afya nchini na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi” amesema Dkt. Magembe.

Upande wake, Dkt. Rebecca Bunnell ameishukuru Serikali ya Tanzania kumkaribisha kuja kuona shughuli za PEPFAR Mkoani Tanga na pia alishukuru kwa ushirikiano unaonyeshwa na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya VVU na UKIMWI nchini.

Dkt. Rebecca amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma za afya nchini na kuahidi kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha zaidi huduma za Afya.
 
Umetumwa wewe sio bure ,,,,mimi huku mtaan kaya za ukimwi zinaongezeka alaf takwimu kitaifa zinapungua mpaka nawaza hivi hizi kaya sio za Tanzania?

UKIMWI upo mwingi sana ukitaka kupona kuupata kaa mbali na mapenzi
 
Kukaa mbali na mapenzi wala haikuzuii kupata virus vya h.i.v.
 
Umetumwa wewe sio bure ,,,,mimi huku mtaan kaya za ukimwi zinaongezeka alaf takwimu kitaifa zinapungua mpaka nawaza hivi hizi kaya sio za Tanzania?

UKIMWI upo mwingi sana ukitaka kupona kuupata kaa mbali na mapenzi
ndio kanuni yangu mkuu kukaa mbali na mapenzi hupati ukimwi

halafu hawa wanatudanganya ili tuathirike wao walipwe

haiwezekani huku kwetu ukimwi watu kibao halafu wao wanatuambia eti umepungua

wingi wa waathirika unailipa serikali na mashirika
 
sijui kama mada imeeleweka
 
Imeelezwa kuwa kasi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI imepungua kutoka Asilimia 7% Mwaka 2003 hadi kufikia Asilimia 4.3% Mwaka 2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, akimuwakilisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akiongoza ujumbe wa wageni kutoka Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Msaidizi (PDAS) na Kaimu Naibu Mratibu Mkuu wa masuala ya UKIMWI wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR), Dk Rebecca Bunnell ulipotembelea Mkoa wa Tanga katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Mhe. Waziri Kindamba pamoja na Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya "Gift of Hope" kilichopo Jijini Tanga.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha huduma za afya, hasa katika huduma jumuishi kwa waathirika wa dawa za kulevya na VVU,” amesema Dkt. Magembe.

Aidha, Dkt. Magembe amesema kupitia ufadhili wa PEPFAR Tanzania imeweza kuanzisha vituo tisa vya utoaji wa Dawa ya Methadone kwa waathirika wa Dawa za Kulevya nchi nzima, pamoja na huduma ya kliniki ya kutembea katika vituo saba.

“Tunaishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada wake kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kwa kuendelea kushirikiana katika uboreshaji wa huduma za afya nchini na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi” amesema Dkt. Magembe.

Upande wake, Dkt. Rebecca Bunnell ameishukuru Serikali ya Tanzania kumkaribisha kuja kuona shughuli za PEPFAR Mkoani Tanga na pia alishukuru kwa ushirikiano unaonyeshwa na Serikali ya Tanzania katika mapambano ya VVU na UKIMWI nchini.

Dkt. Rebecca amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma za afya nchini na kuahidi kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha zaidi huduma za Afya.
Kulikuwa na tabia pia ya kuku cook data, kuonesha maambukizi yako juu sana, ili pesa za ufadhili ziongezwe. Mara nyingi wanaofanya ni hao hao wanaopokea fedha toka kwa wafadhili.
 
Back
Top Bottom