Ndio maana alipoahidi kuweka vielelezo vyake hadharani ni miezi 6 sasa hajafanya hivyo?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Democracy,Magufocracy or Lootocracy?

Onyo:Nimepona.Kama una hasira usisome post hii.İnaweza kukuchochea hasira zaidi.Najadili Rais Magufuli Kulipwa zaidi ya Shilingi Milioni 422 kwa mwaka wakati kwa mujibu wa ripoti Benki ya Dunia 2015 Pato la Mwananchi kwa mwaka kulingana pato la ndani la taifa ni Shilingi milioni 1.8(Dola 842.44) tu. Linaingia mara 229 kwa Pato la Rais wao kwa mwaka. Post hii inaweza kuamsha Hasira kwa Walipa kodi,Wasiopenda kudanganywa au kupotoshwa na viongozi,Wapenda Ukweli,Wastaarabu,Wazalendo kwelikweli,Wacha Mungu,Waadilifu,Wachapa kazi na wale wanaotambua nguvu na mamlaka yao kikatiba kwamba msingi wa mamlaka yote ni wao kama sehemu ya Umma.Watu wa aina hii msiisome post hii vinginevyo labda kama mna uvumilivu

Kwa mujibu wa Mtandao wa MyWage Rais Magufuli wa Tanzania analipwa kama ifuatavyo.

Annual (Kwa Mwaka)Tzs.422,135,637.00. Monthly(Kwa Mwezi):Tzs. 35,178,053.00. Weekly(Kwa Wiki):Tzs 8,118,012.00. Daily(Kwa Siku):Tzs 1,156,539.00

Halafu mtu akuambie anatamani Urais ungekua miaka 2 tu.Hebu angalia kama utamuamini

İkulu ipo kimyaah! Rais Magufuli atoke hadharani aseme ule mshahara wa Milioni 9.5 aliosema ulikuwa wa Wiki akakosea akasema ni wa Mwezi?

Je,Ndio maana alipoahidi kuweka vielelezo vyake hadharani ni miezi 6 sasa hajafanya hivyo? Atawekaje kwa mfano?Na akiweka sasa atazuia vipi hisia kuwa zimepikwa?

Siamini kama hii vita ya ufisadi imekua ngumu kiasi hiki kama ile vita ya Ufisadi wa elimu hasa suala la Uhakiki wa Vyeti.

Ni Rahisi sana kwenda Ufukweni Kuongoza Kufanya Usafi au kuhakiki Silaha lakini ukitaka kujua ngoma ni nzito linapokuja suala pesa mwambie mtu aweke hadharani nyaraka za mshahara wake utasubiri miezi 6.Pesa Mwanaharamu ati.

Ni Rahisi sana mtu kujua Rafiki yake ana wake au mahawara wangapi na kuwataja hadharani hata kama hakuna zoezi la kuhakiki wake au mahawara kitaifa lakini Uhakiki wa Vyeti ukawa mgumu kwelikweli kwake na linapokuja suala la uhakiki wa Mshahara unaweza kuonekana Mchawi au mchochezi bure ukiendelea kumkumbusha.Japo ni haki yako kama mlipa kodi.Waweza kukamatwa au kufunguliwa kesi ya kumchonganisha kiongozi na Wananchi.Hatari Sana hii.Veery Dangerous Affair!

Lakini nina kila sababu ya Kuamini Data hizi za My Web kwa kuwa Rais Magufuli hakutimiza ahadi yake aliyotoa kuweka nyaraka za mshahara wake hadharani.

Pia nilijiuliza ikiwa Marais Wastaafu wanalipwa asilimia 80 ya Mshahara wa Rais wa Sasa ina maana Mamilioni aliyotajwa kulipwa Kikwete and consequently Mkapa na Mwinyi ina maana ghafla yangeshuka hadi Milioni 7 (sawa na ile Faini ya Cyber Crime) kutokana na kuwa asilimia 80 ya shilingi Milioni 9.5 za Rais Magufuli kwa sasa?

Mshahara huu wa Milioni zaidi ya 35 kwa mwezi ni mkubwa kuliko mshahara wa Marais wote Afrika Mashariki ukiwepo wa Kenyatta ambae Uchumi wa nchi yake yenye uchumi wa daraja la kati ndio mkubwa Afrika Mashariki na ni mshahara mkubwa kuliko hata wa Fatah Asisi wa Misri taifa lenye nguvu za Kiuchumi na Kijeshi Afrika na amezidiwa kidogo na Jacob Zuma wa Afrika Kusini(Mla Rushwa aliyekubuhu mwenye mashtaka mengi ya Ufisadi mahakamani) lakini Taifa lake Tajiri Afrika.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Salary Explorer, Mtanzania mwenye mshahara wa daraja la kati ni shilingi 1,284,000 kwa mwezi ambao unaingia kwa mshahara wa Rais Magufuli mara 27.4 kwa mujibu wa Data za MyWage.

Nikitaja kima cha chini cha mshahara kwa mwezi kwa mtanzania na hesabu zake kuwa zinaingia mara ngapi naweza kuishia kukasirisha hata watu ambao sitaki wakasirike .

This is absolutely scandalous!

Tunayo Katiba İbara ya 43 inasema mshahara wa Rais haupunguzwi.Niliwahi kuandika mfumo unadhamini ufisadi.Ni rahisi kwa kiongozi kusema nalipwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa sheria inambeba.Lakini hawezi kuigusa .Lakini ni rahisi kutoka na maneno ya kishujaa kuwa nitawashusha Malaika waishi kama Mashetani au Wale wanaolalamika Maisha Magumu walizoea hela za kifisadi mwisho atawaambia wananchi vumilieni tu ni hali ya kawaida.Yeye je?

Huyu ndio Rais wa Maskini anayelipwa hela ndogo sana.Mwanademokrasia,Msomi Nguli wa PhD aliyetafiti Kweli Maganda ya Korosho.Hana Roho ya Korosho.Yeye ni Kama Nyerere .Akiahidi anatekeleza.Ni baba mdogo wa Taifa.(Natania tu).

But....!

This is official looting constitutionalised.

The status quo is a direct insult to the generality of hard working Tanzanian's in essence what it says is, you Tanzanian citizens are foolish buffoons,keep quite while we legalize looting the treasury.

I'm repulsed to the extreme and i have no adjective to describe this affront to common political leaders.

Sasa [HASHTAG]#MagufuliToaVielelezo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Magufulideclareyourpaytubes[/HASHTAG]

[HASHTAG]#MagufuliHakikiPhDyako[/HASHTAG]

Mungu Awabariki,Tujadili bila hasira Jamani.

A Luta Continua, Victory Ascerta
 
Nchi hii kuna watu wajinga sana wanaacha kujadili maendeleo wanajadili mtu. Huyu ben ndo nani sijui hata kama raisi anamjua au ndo anatafuta kutoka mambo ya nitoke vipi.
 
Juzi wamekaa Ledger Plaza viongozi wa CDM na kulipa ela kibao tena kwa dolari na kujilipa pesa nyingi Per DM,wiki chache kabla ya hapo walikuwa ziarani Ulaya, huku chama hakina hata ofisi, kinapanga pale Ufipa, kabla hujamnyooshea kidole mwenzako jitazame kwanza.Hizi siasa za kukosoa kosoa na uzushi bila kujitathmini zitaupoteza upinzani jumla.
 
Pesa tamu sana jameni, muwe mnazisikia tu! Si mnaona hata viongozi wa kidini wanavyoingia wazimawazima kwenye mitego ya noti? Mpaka 'mababa askofu' wamo, linapokuja suala la noti! Itakuwa JPM. Mzee wa uzwaaji wa nyumba za serikali?:D:D
 
Back
Top Bottom