Ndege za Mwanza zaleta kizazaa uwanja wa ndege Dar

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Abiria waliokuwa safarini kwenda Mwnza leo kwa ndege za 540 na Precision air wamekwamba uwanja wa ndege wa JNIA na hali ni mbaya.

Precision Air wamebadili ndege yao iliyokuwa iondoke saa 5 asubuhi (kwa kutumia ndege aina ya Boeng) bila taarifa na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa abiria. Baadhi yao wamehamishiwa kwenye ndege za saa 8.30 mchana na saa 12 jioni. Wakati huo huo, kuna abiria ambao wamecheleweshwa hadi kesho.

Jambo ambalo linakera sana ni kwamba wakubwa wa shirika hili hawapo ofisini kutoa majibu kwa abiria ambao wanateseka bila sababu.

Ndege ya 540 imekwama kuondoka toka jana na hadi sasa hakuna maelezo ya maana! Baadhi ya abiria wako airport hadi sasa!
 
Mmh sasa hapo uzuri,haraka ya safari iko wapi? Nchi ya wajanjawajanja mpaka viongozi nao wajanja wajanja.Poleni sana inauma kwakweli mipango,malengo yote yanaharibika unaona kbs.
 
Labda kama wanaanza kusafiri ni hizo ndege kwenda mwanza, ila kama ni wazoefu ni suala la kawaida tu. Mimi nimeshaweka mgomo baridi wa kupanda ndege za mza -dar-mza labda iwe haraka sana na dharura. Vinginevyo nakamata Gombe expedictions, princess muro au shabaha huyoooo, safari bila karaha. Tena hao precisior ndo wapuuzi mno
 
Inakera sana ndugu yangu!
 
Hawa jamaa ni wababaishaji sana,

Precision Air wamekimbia wote...Tumeomba namba ya MD wao tumpigie aje kutafuta suluhu tukaambiwa ni week end!!

Watu walikaribia kuwafikisha polisi! Hakuna kinachoeleleweka!

540 ndo hawaeleweki kabisa...Nimeambiwa abiria walilala hotelini na sasa wameombwa kwenda kupata lunch Flamingo restaurant...Maelezo yanayotolewa ni utata mtupu!!
 
Mimi hawa jamaa sina hamu nao kabisa, muda mwingine unalazimika kusafiri na ndege kuepa usumbufu wa kukaa kwenye basi siku nzima au pale unapokuwa unasafiri na watoto wadogo lakini inapokuwa unaepuka usumbufu na kukutana na usumbufu zaidi kwakweli inakera. Mimi waliniweka siku nzima Airport na kuniharibia kabisa mipango yangu
 
Nawashauri wampigie simu Dr Mwakyembe haraka sana (Namba hiyo ya simu aliyoitoa pale Jangwani ni 0782 242526); si ajabu akapanda helicopter ya jeshi akaenda KIA kuokoa suluhu. Pigeni sasa hivi, keshatoka kanisani kwa Rev Gwajima.
 
Mama Mdogo, .. mipaka Mwakyembe ni wizarani kwake .. Hao 540 & Precision hana cha kuwafanya/ ... zaidi ya kufoka au kutishia kuwanyang'anya leseni.
 
Nimechoka!!! Lakini je, utaratibu huo umeandikwa kwenye katiba???? Precission Air, air 540 na vyote vitembeavyo kwa tairi la mpira, chuma, kutambaa/kuteleza majini na kulea/kuruka angani, bila viwe vinasafiri au vinasafirishwa, viko chini ya Mwakyembe kikatiba. Wao waliokwama wapige atawapa msimamo.

sasa nyie ndege ina itirafu mnataka iende hivo hivo,mkipata ajali,mje tena jf kulalamika,ukiona wameairisha safari kwa matengenezo mshukuru,si kila kitu mnalalamika
 
Naona umeamua kuongea kama wafanyakazi wa hizi ndege...Kuna mmoja kanambia kuwa, tunalalamika nini wakati hili ni jambo la kawaida??

Kwa hiyo wewe pia unaona ni sawa, abiri atoke Mbezi ya Kimara au Tegeta kuwahi ndege ya saa5 asubuhi, akifika aambiwe kwamba ndege imeharibika bila kupewa maelezo na suluhisho la safari yake? Na hizo gharama anazoingia zitalipwa na nani?

Anyway, ngoja niishie hapa...kinachotusumbua watanzania ni ujinga!!
 
Nawashauri wampigie simu Dr Mwakyembe haraka sana (Namba hiyo ya simu aliyoitoa pale Jangwani ni 0782 242526); si ajabu akapanda helicopter ya jeshi akaenda KIA kuokoa suluhu. Pigeni sasa hivi, keshatoka kanisani kwa Rev Gwajima.

Ningekuwa na hii namba, ningempigia....Jamaa hawajali utadhani anatoa huduma bure kama kanisani....(hata huko kanisani tunatoa sadaka)!!
 
Mimi hawa jamaa sina hamu nao kabisa, muda mwingine unalazimika kusafiri na ndege kuepa usumbufu wa kukaa kwenye basi siku nzima au pale unapokuwa unasafiri na watoto wadogo lakini inapokuwa unaepuka usumbufu na kukutana na usumbufu zaidi kwakweli inakera. Mimi waliniweka siku nzima Airport na kuniharibia kabisa mipango yangu

Hawa jamaa wanaofanya biashara ya usafiri wa anga Tanzania sina hamu nao....
 
Itirafu = hitilafu

halafu ndege inapokuwa na hitilafu mara kwa mara, delays zisizoisha bado unatetea wenye ndege???????????????? Wabongo bwana

sasa nyie ndege ina itirafu mnataka iende hivo hivo,mkipata ajali,mje tena jf kulalamika,ukiona wameairisha safari kwa matengenezo mshukuru,si kila kitu mnalalamika

wameairisha = wamehairisha
 
Nyie Precision, Juzi tu tumenunue hisa zenu halafu mnaanza uharibu, pesa zetu zitasalimika kweli kwa mtindio huu
 
Abiria waliokuwa safarini kwenda Mwnza leo kwa ndege za 540 na Precision air wamekwamba uwanja wa ndege wa JNIA na hali ni mbaya.Precision Air wamebadili ndege yao iliyokuwa iondoke saa 5 asubuhi (kwa kutumia ndege aina ya Boeng) bila taarifa na kusababisha usumbufu mkubwa sana kwa abiria. Baadhi yao wamehamishiwa kwenye ndege za saa 8.30 mchana na saa 12 jioni. Wakati huo huo, kuna abiria ambao wamecheleweshwa hadi kesho. Jambo ambalo linakera sana ni kwamba wakubwa wa shirika hili hawapo ofisini kutoa majibu kwa abiria ambao wanateseka bila sababu.Ndege ya 540 imekwama kuondoka toka jana na hadi sasa hakuna maelezo ya maana! Baadhi ya abiria wako airport hadi sasa!
Huo ndio muda muafaka kwa ATCL kurudisha na kupata wateja wapya, ATCL inatakiwa ijiimalishe zaidi na kuchukua advantage ya failure za Prec na 540
 
Back
Top Bottom