Ndege ya precious Air yashindwa kutua Dodoma

Watz bwana
Ndege iliyoanguka kwenye maji katika harakati za kutafuta kutua, tulisikitika tukasema heri ingeenda kutua Mwanza.

Leo ndege imerudi kutua Dar ilikotoka, Tunasema yaani imerudi tena hadi Dar.
 
Ushindwe kutua Dodoma na engine moja, ugeuze angani urudi Dar na engine moja na utue...

Habari haijakamilika...
 
soma kitabu kinaitwa "Aircraft Manufacturing in the New Era"utaelewa jinsi ndege inavyoweza kutua Manually kunapotokea tatizo la kiufundi,kikubwa Uwanja husika uwe na technology hiyo,kwa Tanzania ipo Dar tu sina uhakika kuhusu KIA kama ipo
Nipe hiyo technolojia iliyopo dar
 
Ndege ya Precision Air PW 600, iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma imeshindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma na kulazimika kurudi mkoani Dar es Salaam baada ya moja ya injini zake kuzima wakati ikikaribia kutua.
---
Ndege ya Precision Air PW 600, iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma imeshindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma na kulazimika kurudi mkoani Dar es Salaam baada ya moja ya injini zake kuzima wakati ikikaribia kutua.

Taarifa ya tukio hilo imeelezwa na moja ya abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, ambaye ni Naibu Meya wa Kinondoni, Joseph Rwegasira Samson, ambapo ameeleza kuwa wanashukuru Mungu, wamefanikiwa kutua salama kwenye uwanja ndege wa Dar es Salaam, ikiwa inatumia injini moja.

PIA SOMA
- Ndege ya Shirika la Precision Air iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma yalazimika kutua kwa dharura

Credit: ITV
Habari nusunusu. Injini moja tu ilikuwa inafanya kazi. Hivyo, ndege ilishindwa kutua hapo Dodoma na hiyo injini moja. Badala yake ikaweza kusafiri na hiyo injini moja mpaka Dar na ikaweza kutua na hiyo hiyo injini moja ambapo ilishindwa kufanya hivyo Dodoma!
 
Back
Top Bottom