Ndege Mpya ya Mizigo ya ATCL imeanza rasmi safari zake leo 7 Julai 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kampuni ya Ndege Air Tanzania (ATCL) leo imeanza safari yake ya kwanza ya ratiba ya kusafirisha mizigo kwa kutumia ndege yake ya mizigo Boeing 767-300F iliyowasili nchini mapema mwezi Juni 2023 ambapo mzigo wa leo unasafirishwa moja kwa moja kwenda Dubai kwa muda wa saa tano tu.

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni hiyo Patrick Ndekena amesema ratiba ya safari za Dubai itakuwa mara mbili kwa wiki ambapo jukumu la ATCL kwa ndege hii ni kuhakikisha bidhaa za Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi zinafika kwa wakati na zikiwa na ubora wake kwenye Nchi mbalimbali kwa kadri ya mahitaji.

“Leo tuna furaha kubwa kwa kuanza rasmi safari zetu za ratiba kwa ndege yetu hii mpya ya mizigo Boeing 767-300F yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu na uzito mkubwa yaani tani 54 kwa mara moja, kwa Dubai peke yake tutakuwa na safari mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa”

Kuhusu uwezo wa ndege hiyo, amesema Boeing 767-300F ni ndege ya kisasa yenye uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 850 kwa saa na kukaa angani kwa zaidi ya saa 10 bila kutua.

Kwa upande wake Wakala wa usafirishaji mizigo George Magoti amesema uwepo wa ndege hii ni Mkombozi kwa Wafanyabiashara nchini kwani itawasaidia kupunguza gharama za usafirishaji ambapo amesema kutokana na ukubwa wa mizigo hii, isingewezekana kusafirishwa kwa ndege ya abiria hivyo wangelezimika kukodi ndege ya mizigo kutoka nje ya Tanzania ili kuweza kupakia mizigo mikubwa ya aina hii

WhatsApp Image 2023-07-07 at 20.09.14.jpeg

WhatsApp Image 2023-07-07 at 20.09.15.jpeg
 
Back
Top Bottom