Nchimbi: Tupo tayari serikali kukaa pamoja na vikundi/taasisi za kidini

mnyanyaswaji

JF-Expert Member
Nov 10, 2009
478
117
Amesema kama serikali hatupo tayari kusubiri watu wauwane ndipo tuseme tukae chini,inatosha na wapo tayari kukaa kimazungumzo na taasisi za kidini.
My take: kauli kama hii ilitakiwa mapema mnoo na sio mpaka watu walaluwane, na isiwe kwenye dini hata siasa na mambo mengine.
Source Channel Ten Habari saa moja.
Nawakilisha
 
Pimbi huyu alikuwa kajificha kwa mama mkwe wake kwa kuwaogopa wafuasi wa ponda. Kaona hali imetulizwa na JWTZ sasa ndio anaibuka.
 
Tatizo la Waislamu ni BAKWATA + CCM. Serikali ya CCM inawalazimisha Waislamu wote kua chini ya BAKWATA wakati upande wa pili wa Wakristo kuna Mabaraza mengi tu ya kuwasimamia.

Upo ushahidi kua kuna taasisi nyingi tu zinashindwa kutoa misaada mbalimbali kwa Waislamu kwa kulazimika kupitia Bakwata wakati hawaiamini.

Bakwata ndio iliyouza kwa Manji kiwanja cha waislamu cha Chang'ombe kwa bei ya kutupa. Lakini kama kungekua na mabaraza mengine Huru, hili lisingetokea kwa urahisi.

Serikali ya CCM kama inania ya dhati ya kumaliza haya matatizo basi iondoe monopolistic kwa hili baraza juu ya affairs za Waislam.

Tukianza hapo kwanza, mengine pia yatafuata maana naamini waislam wana hoja nyingi tu za kusikilizwa.
 
waongee nini na vikundi vya kidini.? Haoni kama ni kuhalalisha udini.?....akianza kusikiliza vikundi vya kidini vya kiislamu sawa na kuhalalisha makundi ya kidini tanzania na ndio mwisho wa tanzania moja.!
Hamna wasikilize madai ya wanaolalamika awe mwanasiasa/dini/michezo etc ila kama ana haki yake asinyimwe kwani kumnyima mtu haki yake unarusha mbele matatizo na wala humalizi matatizo.
 
wake chini kuzungumza nini ....? hawa wanachotaka ni kuchoma makanisa .... Nchimbi awape kibali basi?

disgusting
Acha roho ya korosho! Kamshaurini basi Nchimbi asitishe kama alivyositisha Membe kipindi kilee
 
Nchimbi haaminiki kabisa,kauli yake ni ya kisanii uliokubuhu Shark naunga mkono hoja juu ya ubabaishaji wa BAKWATA.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la Waislamu ni BAKWATA + CCM. Serikali ya CCM inawalazimisha Waislamu wote kua chini ya BAKWATA wakati upande wa pili wa Wakristo kuna Mabaraza mengi tu ya kuwasimamia.

Upo ushahidi kua kuna taasisi nyingi tu zinashindwa kutoa misaada mbalimbali kwa Waislamu kwa kulazimika kupitia Bakwata wakati hawaiamini.

Bakwata ndio iliyouza kwa Manji kiwanja cha waislamu cha Chang'ombe kwa bei ya kutupa. Lakini kama kungekua na mabaraza mengine Huru, hili lisingetokea kwa urahisi.

Serikali ya CCM kama inania ya dhati ya kumaliza haya matatizo basi iondoe monopolistic kwa hili baraza juu ya affairs za Waislam.

Tukianza hapo kwanza, mengine pia yatafuata maana naamini waislam wana hoja nyingi tu za kusikilizwa.
Kweli wewe GreatThinker. Na unajua nini kinachoendelea na sio kuropoka. But sasa hivi ndio mwisho wa Bakwata
 
weakest proposal and offal ever to be made by the ministry in question of the expense on unknowingly.
 
Hamna wasikilize madai ya wanaolalamika awe mwanasiasa/dini/michezo etc ila kama ana haki yake asinyimwe kwani kumnyima mtu haki yake unarusha mbele matatizo na wala humalizi matatizo.

Mkuu unaweza kufafanua madai ya hayo makundi/kundi dhidi ya serikali hadi yasikilizwe.?
 
waongee nini na vikundi vya kidini.? Haoni kama ni kuhalalisha udini.?....akianza kusikiliza vikundi vya kidini vya kiislamu sawa na kuhalalisha makundi ya kidini tanzania na ndio mwisho wa tanzania moja.!

Hiyo ndio Pointi Yangu na mimi waongee nini hasa? Siasa za bongo ni mazoea yasiyo endana na wakati ndio maana tunazidi kuwa masikini.
 
Sawa! lakini wakienda kuwachukua BAKWATA na kuzungumza nao na kutuambia kuwa wameshazungumza na Waislamu kupitia Baraza lao kuu basi itakuwa ni kujisumbua tu.
Bakwata needs to be isolated! at least for the moment.
 
Nchimbi alikuwa likizo? Where was he? Compare his reaction hii meltdown iliyotea Dar na Zanzibar na jitihada zake za kujiweka karibu na wanaandishi wa habari wakati wa mauaji ya Mwangosi? Photo opporunity?

Na anaamini suluhisho la hii hali ya sasa wanalo viongozi wa dini? Kabla ya kuwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa waziri wa habari, je, aliridhika na contents za radio Imaan? au gazeti la Al-Nuur?

Na inakuwaje waziri wa mambo ya ndani anajitokeza so late?
 
Akakaee na bibi yake makanisa yalipochomwa akusema hivyo limewafika shingoni wanahaha sasa....pu.....vu
 
Kauli yenyewe ni dhaifu kama wao wenyewe walivyo..hivi hawa jamaa wana agenda gani na watanzania?
 
Nchimbi haaminiki kabisa,kauli yake ni ya kisanii uliokubuhu Shark naunga mkono hoja juu ya ubabaishaji wa BAKWATA.
Kweli mkuu wangu, wangelivunjilia mbali, au kuacha mabaraza mengine yasiyofungamana na Bakwata yaanzishwe.

Hivi nikuulize, linalowasimamia Baraza moja tu linalowasimamia Wakatoliki, Waanglikana, Walutherani, Wasabato, Walokole n.k.kwa pamoja?? Linaitwaje??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom