Nchimbi anaibua Mazuri ya Serikali dhidi ya Mabaya Machache, Makonda anaibua Mabaya Mengi dhidi ya Mazuri machache kati yao nani Bingwa wa Siasa?

nasimama na bashite hao wazee hawana mvuto wowote kazi kusifia Chama wakati huo bashite alisimama kutetea wananchi
Mvuto gani? Au unavutiwa na msambwanda wa Bashite?
Screenshot_20240415_144237_Google.jpg
 
Kinachotakiwa ni mabadiliko ya mfumo wa utawala kwa faida ya wengi.
Iwe CCM au upinzani, itategemea nani atawahi. Mama Samia kaja na 4R, Makonda kajaribu ktatua kero kwa uwazi, Nchimbi na Mongela kutatua kero kimya kimya huku upinzani ukitoa hoja za kutatua matatizo na changamoto kwa njia zao.
Kwa mwananchi wa kawaida, shida zake ziondoke bila kujali jina la anayeziondoa.
 
Wanajamvi nimefuatilia kwa karibu Ziara zote mbili za Chama cha Mapinduzi zilizofanyika hivi karibuni,ya kwanza ni ile ya Mwenezi Mstaafu Makonda peke yake akiwa na Serikali aliyoita Back to Back na ya pili hii ya Nchimbi akiwa na Sekretarieti ya Chama.

Nilichokiona Binafsi Ziara ya kwanza ya Makonda iliyotawaliwa na Populism iliibua Mabaya mengi sana ya Serikali na kujenga Taswira kwamba Serikali haipo na hakuna inachokifanya,katika Ziara hii upande wa pili wa Mema ya Serikali au utekelezaji wa Ilani haukunadiwa kama yalivyonadiwa Madudu.

Kiuhalisia Kero haziishi popote hata kwenye Ngazi ya Familia bado zipo mtu akiamua kuibua anaweza kukutana na Familia ikaibuliwa kero ya chakula kibaya,baba kuchelewa kurudi n.k,Naamini hata yeye akikaa Miaka 10 Arusha akija Kiongozi wa Kariba yake kutoka juu anaweza kusikiliza Kero na akazipata akamfanyia kama alivyofanyia wenzake kwa tafsiri kwamba hata alivyokuwa Dar hakumaliza Kero.

Kwa Upande wa Ziara ya pili ya kina Nchimbi naona iko tofauti inaonyesha upande wa Pili wa Serikali kwamba kuna Mema na Mazuri yamefanyika mengi kuliko mabaya hivyo inastahili kupewa nafasi nyingine kuendeleza yale mazuri.

Kwa Wataalamu na Weledi wa Kisiasa hebu tusaidieni kudadavua,kisiasa hapa nani Bingwa na nani anafanya vizuri?Zingatia neno KISIASA.

Povu Ruksa.
Kupo ulikolalia!
 
Makonda Yuko vzr kujitekenya na kucheka.....mtu anajitekenya hacheki haipendezi ...tafsiri upendavyo..
 
A

Asiyejua kuwa Serikali haifanyi kitu ni nani hata ahitaji kuambiwa? Kwa ujumla WaTz ni wajinga, kwa sababu hao wote wawili wanawachezea shere, mbaya zaidi wanakubali kuchezewa! Wote ni takataka tu mpaka mwenyekiti wao!
 
Back
Top Bottom