Nchi kwanza chama baadae na kinachoendelea Arusha

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE
 
Vipi Nape, mbona siku 90 ziliisha jamaa bado wamo chamani?, vipi au tuseme mko dakika za nyongeza au?, nadhani ingekuwa jambo la busara ukadili na joka lenu?.
 
Nape Kuna tuhuma za rushwa, Chama chako cha magamba kinaendeleza magamba yake kwa kununua demokrasia. Hakuna Muafaka pale ulifanyika uhuni ulioasisia na chama cha Magamba. Hatuwezi kufanya kazi kama magamba, kumbuka ulisema siku tisini, Mukama akasema hakuna kitu kama hicho.

CDM ni chama chenye taratibu na kinachofuata sheria na kanuni, na wanaonyesha kwa uwazi kwa hilo wako tayari kumwajibisha yeyote. We walk the talk.

Kwanza pambana na siku tisini ulizodanganya wananchi na wanachama wako. Pili waambie wakubwa zako hakuna mchezo mchafu wananchi wanataka demokrasia. Kama CCM mnauhakika wa kushinda kinyanganyiro cha Meya wa Arusha mnaogopa nini kurudia kura mpaka mgawe vyeo kama pipi, hii ndio demokrasia na siasa unayoihibiri karne ya 21? Huko ndio kuvua gamba?

Halafu hizi siasa za kuiba kura na ulaghai halafu kutaka muafaka zimeanza lini? Huwezi kuiba kura, kuvunja kanuni, kununua wasimamizi wa mchakato wa demokrasia halafu ukitegemea muafaka utalainisha mambo.

Taifa mbele na vyama baadaye naam. Haki kwanza vyama baadaye.
 
Toka lini CCM mkawa na mtazano huo! mbona haikuwa rahisi kuachia chaguo la wananchi juu ya uraisi?... nadhani CCM ishukuru uungwana wa DR Slaa kukaa kimya juu ya wizi wa kura uliofanywa na CCM na NEC yake, amasivyo yangetokea ya kenya
 
Nape,

Wananchi walisema mlipane posho au hizo za sasa hazitoshi? Kumbe matakwa ya viongozi wa CCM ndo matakwa ya wananchi? LOL
 
Babuwaloliondo, changia mada. Nape alishajibu Hilo siku nyingi HATA Kama sikubaliani naye sana KWENYE majibu yake.
Hapa mada NI UZALENDO wa cdm uko wapi kwa sakata la Arusha? Hivi kweli kwasababu Tunataka Kesi ZA viongozi wetu zifutwe, bass tuko tayari mgogoro usiishe, kisa kesi ziko mahakamani ZA Freeman na Slaa?
KWAHILI CHAMA CHANGU MMENICHEFUA AAAAGHAAAAA!!!!!!!!
 
Mbona unajishushia heshima mkuu?kwa nafasi yako sidhani kama ungechukulia yanayotokea arusha kimzahamzaha!unafahamu kwamba watu wamekufa pale arusha kwa kupigania haki?leo hii madiwani wenye uchu wa fedha wanawasahau wananchi na kufikia muafaka wa kiujanja ujanja.chuki ya wananchi kwa meya feki bado ni kubwa toka lini madiwani wa3 wanaweza kufikia makubaliono bila kupewa ruksa au kupata inputs za wananchi wake.
Kawaambie wabunge wa magamba wasimamie wananchi na sio kupiga mikelele ya ndiooo.
Usikejeli watu bana!
 
nimeamini wewe kijna ni mtu wa ajabu sana......kuna thread umeanzisha kule, umekimbia na kuanzisha thread hii...hujajibu tuhuma lukuki zilizoelekezwa kwako.......nakushanga sana...chadema sio kama ccm..chadema wanatekeleza kwa vitendo..subiri tume imalize kazi yake ndani ya siku sita na kama wakipatikana na hatia hao madiwani chadema hawana cha salia mtume
 
Babuwaloliondo, changia mada. Nape alishajibu Hilo siku nyingi HATA Kama sikubaliani naye sana KWENYE majibu yake.
Hapa mada NI UZALENDO wa cdm uko wapi kwa sakata la Arusha? Hivi kweli kwasababu Tunataka Kesi ZA viongozi wetu zifutwe, bass tuko tayari mgogoro usiishe, kisa kesi ziko mahakamani ZA Freeman na Slaa?
KWAHILI CHAMA CHANGU MMENICHEFUA AAAAGHAAAAA!!!!!!!!
Nape bwana kumbe upo na ID kibao!
 
Hivi Nape, ni kweli unaamini kwamba ni watu watatu tu ndio walioipotezea umaarufu CCM! Sema ukweli ukimwogopa Mungu, hivi kwa akili yako timamu unaamini kwamba wakifukuzwa Chamani leo, Edward Lowasa, John Chenge na Rostam Aziz ndio CCM itakuwa imejisafisha kwa Wananchi! Hivi wewe binafsi huoni kwamba unatumika na kundi moja la wanaowania Urais kupitia chama chako kuwamaliza wengine! Je huoni kwamba umeweka maslahi ya Tumbo lako mbele kuliko hata maslahi ya Ubinaadam wako!

Angalizo: Hata condom huwa na heshima sana kabla ya Bao, lakini baada ya bao hushikwa kwa kinyaa! Angalia usiwe umetishwa heshima hiyo!

Ya Chadema waachie Chadema, dili na lako linaloelekea kukushinda maana umedandia roli kwa mbele.
Nimewaza tu kwa kutafakari.
 
Nape ungewafundisha hilo wale wabunge wa chama chako wanaoimba ngonjera za kusifia bajeti a100% baadae wanaanza kuorodhesha mapungufu na matatizo kibao!!
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

Kumbuka chanzo cha mgogoro wa Arusha then utajua kuwa hakuna muafaka bali ni uhuni. Tatizo la Arusha ni kutofuatwa kwa sheria na taratibu katika uchaguzi wa Meya na sio kuwapa watu vyeo hovyo hovyo.. Kama mlikubali hilo tatizo kilichotakiwa kufanywa ni kuitisha Full Council nyingine na column itimie bila kuweka mapandikizi (Chatanda etc) na uchaguzi ufanyika upya.. Huu muafaka wa sasa haukuzingatia sheria na ndio maana bado ni batili vile vile hata kama Meya, Naibu na Viongozi wote wa kamati wangekuwa wa CHADEMA.

Sheria na taratibu lazima zifuatwe sio kupeana vyeo kiholela!!
 
Mkuu Nape, Nadhani tumesikia kwamba kuna tuhuma za rushwa, kilichofanyika ni CDM makao makuu kuunda tume ili kuchunguza hilo, kwa sababu hata kama nia ilikuwa nzuri lakini kama imefanyika baada ya kupewa rushwa hili halikubaliki na huo ndio uzalendo wa kwanza kwa nchi yetu.
Ni kwa sababu chama chako Rushwa ni kama mazoea unaweza kuona hilo si tatizo kubwa.
 
Nape mawazo yako nayashangaa sana hoja yako ya taifa kwanza hivi wewe ndio unajua taifa kwanza leo? umesahau ulivyochakachuliwa ubungo na kwenye uvccm kama unakumbuka na namna haki ilivyokunjwa maana ndio kawaida yenu ukapozwa kwa vyeo ukatulia wala hukukemea uovu ule sasa SUALA LA MSINGI SIKU ZOTE TAMBUA HAKI KWANZA YOTE YATAFUATA BAADAE uchaguzi wa meya haukua halali maana yake hauku fuata misingi ya haki hata maridhiano yasiyo kumbuka usahihi wa kanuni ya wakaendelea kuvunja haki. Kauli yako imejaa ushabiki na haina manntiki si kauli yakutolewa na msomi tazama hoja ya msingi wewe ni kijana mdogo sana bado unasafari ndefu kisiasa achana na siasa za wazee wako wa ccm ndi waliotufikisha hapa tulipo kaka Nape. Waache wenzio wajenge chama chenye nidhamu WAKIYAACHA HAYA BAADAE WATAINGIA KWENYE KUVUANA MAGAMBA SUALA AMBALO LINAWASHINDA KWASASA
 
Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE

Nape uelewa wako wa mambo kwa ujumla ni mdogo, huwezi kuweka hayo unayoyaita maslah ya Taifa kwa unafiki,rushwa,na kujali madaraka. vinginevyo ikiendelea hivyo,basi jua kuwa mbele ya safari USUGU WA KUKALIA VITI VYA MADARAKA UTAOTA TANZANIA HII.kwa ufupi ni hivi,Chadema ikikubali mazingira kama unayoyasema,basi jua kwamba haotakuwa tofauti na CCM. Kwani CCM mlikofikia sasa mlianza hivyo hivyo. ndo inafikia hapa kuwa mtu na matajiri wenye Fwedha inakuwa haki na rahisi kushika madaraka...
 
Nape mbona unachekesha banaa!hivi wale wabunge wenu(plus spika),wanaounga mkono kila upuuzi na kupinga kila hoja yenye maslahi kwa taifa zinazoletwa na wapinzani ndo wameweka nchi kwanza?Ebu kuwa muungwana kidogo...!
 
Back
Top Bottom