Nyami2010
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 227
- 50
Wana Jamii
Nionavyo mimi, hali ya NCHI ni TETE kuliko tulivyozoea. Baadhi ya viashiria ni hivi hapa:
1. Hazina ni kweupe. Mhe. Waziri Mkuchika alibainisha hili, japo Serikali imekuwa ikipinga muda mrefu. Ona sasa Mhe. Rais analazimika kupunguza baadhi ya maafisa wake kwenye safari za nje
2. Bunge kwa namna moja au nyingine halina imani na Rais. Mhe. Spika alisema Rais amebariki posho za Waheshimiwa Wabunge, Ikulu ikakana. Kumbuka sakata la Jairo na Luhanjo
3. Viongozi wetu wameanza kupeana sumu....hadi wanaogopa kupeana mikono. Sakata la Mhe. Mwakyembe
4. Ndani ya vyama hakupikiki. Magamba ya CCM, Mhe. Kafulila, Mhe. Hamad.....
5. Uchumi umekufa:
-Mfumko wa bei ni takribani 20% leo....ukitoka 4% mwaka 2005.
-Serikali imeshindwa kutoa fedha za maendeleo kwenye halmashauri zote nchini, Waziri wa TAMISEMI amekiri hayo Bungeni jana.
-Serikali imeshindwa kununua vifaa vya tiba na kutoa viposho vidogo vidogo kwa madaktari
6. Hali ya Maisha miongoni mwa Watanzania tulio wengi ni mbaya sana X sana!
7. Serikali kupitia Waziri Mkuu imekubali kuwa imeshindwa kuwaletea wananchi maisha bora. Tazama gazeti la Tanzania Daima la leo tar 3 Feb 2012.
8. Viongozi wa Serikali wakiwemo Wabunge wanajitazama wao tu...., wanaacha raia tunakufa..........
9.....ongeza list
Hivi katika hali kama hii, watanzania twaweza kufanya nini? Ebu tupeane mawazo na mikakati kisha tuamue, la sivyo tunazidi kuangamia!