Nchi haizidi wasanii + wanamichezo 900 waliofanikiwa ndio maana tunawaasa vijana wasome wajaribu bahati ya ajira, wajiajiri au kufanya biashara.

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Vijana wengi wadogo wakiwaona celebrities kina Diamond, Mario, Mbwana Samata, Masoud Kipanya, Joti. n.k. wanashawishika kutaka kuanza maisha ua sanaa ama michezo bila kujua kundi hilo halizid watu 900 kwa ujumla wenye maendeleo kwa kutegemea kazi hizo,

Unganisha wasanii na wanamichezo wote hapa Tanzania hawazidi 900 wanaoweza kutegemea kazi zao kuendesha maisha yao, Mbaya zaidi uchumi wa wanamichezo hao huwa mashakani wakistaafu wakiwa bado vijana wenye miaka 38 tu nao wasanii mfano bongo fleva kuna kipindi wanahit lakin baada ya hapo wanaipotea kabisa na mifano ni mingi.

Ni heri kijana usome uje ujaribu bahati kwenye ajira serikalini hata private kuna watanzania zaidi ya laki 1 wanaingiza milioni na kuendelea kila mwezi, ni pesa ambayo ukiji manage vizuri itakutosha walau uwe na maisha ya wastan

Ni heri kijana ujiajiri, kuna vijana wengi sana hii nchi wamejiajiri wana uhakika wa kuingiza wastani wa milioni 1 kila mwezi .

Ni heri kijana ufanye biashara, huku kuna matajiri vijana wanapiga mkwanja sio kitoto japo panahitaji uvumilivu wa kuzijua changamoto na kujenga network yako,

Ni heri kijana ujikite na siasa, vijana wengi wanaendesha maisha kwa siasa, hakuna jambo la kujionea aibu kuwa mwanasiasa ila ni chaguzi yako itakuweka uwe mwasaiasa mzuri ama mbaya katika maslahi ya jamii
 
Mkuu kauli yako haina ukweli,jumlisha wanamichezo wote wanaolipwa tz na wasanii uone idadi yao ndio ulete habari,najua ukichoangalia ni wale maarufu tu,unafahamu Sanaa Ina matawi mangapi?
 
Vijana wengi wadogo wakiwaona celebrities kina Diamond, Mario, Mbwana Samata, Masoud Kipanya, Joti. n.k. wanashawishika kutaka kuanza maisha ua sanaa ama michezo bila kujua kundi hilo halizid watu 900 kwa ujumla wenye maendeleo kwa kutegemea kazi hizo,

Unganisha wasanii na wanamichezo wote hapa Tanzania hawazidi 900 wanaoweza kutegemea kazi zao kuendesha maisha yao, Mbaya zaidi uchumi wa wanamichezo hao huwa mashakani wakistaafu wakiwa bado vijana wenye miaka 38 tu nao wasanii mfano bongo fleva kuna kipindi wanahit lakin baada ya hapo wanaipotea kabisa na mifano ni mingi.

Ni heri kijana usome uje ujaribu bahati kwenye ajira serikalini hata private kuna watanzania zaidi ya laki 1 wanaingiza milioni na kuendelea kila mwezi, ni pesa ambayo ukiji manage vizuri itakutosha walau uwe na maisha ya wastan

Ni heri kijana ujiajiri, kuna vijana wengi sana hii nchi wamejiajiri wana uhakika wa kuingiza wastani wa milioni 1 kila mwezi .

Ni heri kijana ufanye biashara, huku kuna matajiri vijana wanapiga mkwanja sio kitoto japo panahitaji uvumilivu wa kuzijua changamoto na kujenga network yako,

Ni heri kijana ujikite na siasa, vijana wengi wanaendesha maisha kwa siasa, hakuna jambo la kujionea aibu kuwa mwanasiasa ila ni chaguzi yako itakuweka uwe mwasaiasa mzuri ama mbaya katika maslahi ya jamii
Tajiri..mafanikio ni subjective. Kila mtu ana standard yake ya mafanikio. Mfano kwangu mafanikio ni kuafford life. Kupata chakula, mavazi na malazi.

Kwenye chakula kuna cha buku jelo na kuna cha laki kadhaa kwa sahani.....mavazi kuna ya tshirts na jeans za vunja bei kwa 30k au kuna za woolworth za 1.5m....same kwenye malazi..kuna nyumba za 30k per month na kuna makazi ya mil 300 yote ni makazi. Ni wewe tu kusema ni level gani unaweza afford.

Mfano wa wanamichezo ulio wataja hapo ni wale walio extra ordinary katika fields zao..na iyo haipo kwa wanamichezo na wasanii pekee, huo utofauti uko kwenye kada zote.

Otherwise utawaambia wafanyabiashara wa Sembe warudi kusoma maana waliofikia level ya bakhresa hawazidi 10 nchi nzima.

Au utawaambia ma CEO wa bank warudi kusoma maana waliofanikiwa kuwa ma CEO wa kampuni kama google au apple hawazidi 20.

Tuache watu wapambane kila mmoja kwa nafasi yake. Aslong as anachokifanya kinamtimizia mahitaji yake japo kwa uchache
 
Back
Top Bottom