Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

furaha mpate wapi
km vile wapenzi wa timu wanavyopigwa bao
poleni
ila usiseme tanzania haina furaha
jisemee wewe na washabiki wenzako
sie wengine mbona amani tupu furaha tele
wengine wanajua mirija ya mafuta ya bure imekata
 
Kuna mtu anajidai kaniuliza matokeo huku anajidai kuwa na sympath kwa EL mnafiki mkubwa sijui nimtupe katika meza yangu rasmi? hivi Kweli kuna mtu hajui kinachoendelea mpaka sasa. Namdiscipline potelea pote
 
Hata huku ni kimyaaaaaa jamani raisi hata watu hawafurahiiii tatizo sio maguful tatizo ni ccm

Tatizo la nchi hii ni Kikwete na kama Magufuli anataka kurudisha furaha kwa wananchi ni lazima ahakikishe kuwa Kikwete anaondoka kama mwenyekiti wa ccm as soon as possible otherwise atamuwekea kiwingu ili kuwalinda wezi wenzie na hapo magufuli kazi itamuwia ngumu sana!!
 
Kama vile watu wa kaskazini walivyoona ni mwaka wa mapinduzi na kuleta mabadiliko kupitia upinzani, watu wa usukumani na mikoa ya jirani waliona ni mwaka wao wa kuwa na rais aliyetokea eneo lao na walimpenda. Sasa tusilazimishe kila mtu aone kile tunachoona sisi, wingi wa watu walikuwa wakija kwny kampeni sio wingi wa kura, tuliona kwa Mrema, kwa Slaa na hata sasa imetokea, hivyo tukumbuke kila mtu anayo Uhuru wa kunichafua amtakaye
 
Kama vile watu wa kaskazini walivyoona ni mwaka wa mapinduzi na kuleta mabadiliko kupitia upinzani, watu wa usukumani na mikoa ya jirani waliona ni mwaka wao wa kuwa na rais aliyetokea eneo lao na walimpenda. Sasa tusilazimishe kila mtu aone kile tunachoona sisi, wingi wa watu walikuwa wakija kwny kampeni sio wingi wa kura, tuliona kwa Mrema, kwa Slaa na hata sasa imetokea, hivyo tukumbuke kila mtu anayo Uhuru wa kumchagua amtakaye
 
Ni uzuni kubwa na dua mbaya kwa wote walio husikaa kuto patikana kwa mabadiliko .Mungu anajua yote kwake tunapeleka sala zetu.
 
Nimeangalia TBC wakitoa maoni ya wananchi MIKOA MBALI MBALI leo, nimeshamngaa sanaaaa.. Mikoa yote kimyaaaa, wanasikitika... wameanza na Tabora wanafuta watu hadi Bar kuwaulizia wanajisikiaje..wakaonyesha Mtwara yaani hadi aibu, wakaonyesha DAR mitaa kadhaa, watu wala hawana habari...wamekataa tamaa kabisa..!!

Wakaonyesha, Tanga, yaani jamani
watu wanafuatwa hadi vituo vya mabasi, watu hawana stori wala FURAHA yoyote.... mmoja akasema anaona kama CCM sidhani kama watafanya chochote, maisha ni yale yale na yatakuwa magumu zaidi mkaazi wa UBUNGO...!!

Hakuna shamra shamra kokote kule...

Isipo kuwa pale Lumumba, waliokwenda kumwangalia wana mapinduzi sio wengi kivile...!!

The country WENT OFF TRACK...!!!

Sasa, kila mtu ale jasho lake...!!!😨😨
 
Habari wadau.

Naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa.

Nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele.

Hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania.

Kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa.

Labda wala rushwa wanatafakari hatma yao baada ya JPM kupata uraisi
 
mtu anayependa majungu hawezi kuwa na furahan, Majungu yote UKAWA
kweli wazimu n fani!; ukumbuke Mwenyezi alipo iangamiza dunia kwa moto kisha kwa maji kulikuwa na watu kama wewe walio wanenea wajumbe wa mwenyezi kwamba; wanawaletea majungu! ndio sababu mwenzio katahadharisha,ni kwa wale wenye imani, na si kwa makafiro! sawa eeh?
 
Kwanza nianze kwa kuikiri imani yangu kuwa mimi ninaamini katika Biblia na nitatoa mifano yangu kutoka katika kitabu hiki kitakatifu.

KWENYE BIBLIA IMEANDIKWA
"Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua."..... MITHALI 29:2
"Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha."..... MITHALI 28:12


......Ni huzuni kubwa imetanda katika Taifa baada ya haki na maamuzi ya wapiga kura walio wengi kuporwa, demokrasia na uhuru wa kuchagua kuuwawa na kufanywa kuwa danganya toto kwa ajili ya kuficha maovu ya watawala na watu wachache wanaonufaika na kutajirika na utajiri wa taifa huku wananchi walio wengi wakiendelea kuwa masikini na kuteseka.


........Ni huzuni nchi nzima baada ya watanzania kuporwa matunda ya mabadiliko waliyoyahangaika kwa miaka mingi. Ushindi aliopewa mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. John Pombe Magufuli umeoneka kuwaumiza watanzania wengi sana. Nchi imejawa na huzuni, kila mtu anasononeka kila kona ya nchi.


Mabadiliko waliyokuwa wanayahitaji wananchi walio wengi yameporwa kwa nguvu na vitisho na CCM, Jeshi la Polisi na Serikali.


Magufuli ametangazwa kuwa Rais lakini ni rais wa manung'uniko na maumivu ya watanzania.

Nchi imekuwa ukiwa kama mtoto yatima aliyekosa msaada. Nchi imejawa na huzuni kila kona, hakuna shangwe wala furaha machoni, usoni wala kwenye mioyo ya watanzania.

Wananchi wameogopeshwa na kutishwa kuwa wakidai haki yao watauwawa, watapigwa virungu, watamwagiwa maji ya kuwasha na hata kufungwa jela LAKINI ni nani atakayewaokoa watanzania hawa waliotawanyika huku na huko kwa hofu na uoga kama kondoo waliokosa mchungaji jangwani huku wakiwindwa na simba?


Magufuli sio chaguo la Watanzania wengi waliojitokeza kupiga kura na kutaka mabadiliko. Magufuli ametajwa kuwa Rais wa wananchi wasiokuwa tayari kuongozwa naye ila kwa hofu ya kupigwa na kuteswa wamenyamaza na kukubali kuumia ndani ya mioyo yao.


Mungu anasikia sauti za maumivu ambazo huwa hatuziongei. Sheria ya Mungu ipo wazi ya kuwa "MTANYAMAZA NAMI NITAWAPIGANIA" kwahiyo watawala wetu wanapoona tumenyamaza wasifikiri ndio mwisho ila watapambana na ghadhabu ya Mungu muda si mrefu.


CCM unayoiona leo HUTAIONA TENA.
Magufuli unayemuona leo HUTAMUONA TENA.


Mungu aliporuhusu wanadamu wajichagulie viongozi wao wenyewe sio kwamba aliamua kuwasusa wanadamu na kuamua kuwaacha kabisa, LA HASHA! Ndivyo itakavyokua, Mungu hajawatupa watanzania, anayasikia majonzi, huzuni na vilio vya watanzania wengi.


TANZANIA MPYA INAKUJA.
Mh. Edward Ngoyai Lowassa ndiye Rais wa nchi mpya ya Tanzania ambayo wananchi wengi wanaamini katika mabadiliko wamekuwa wakiisubiri kwa shauku kubwa.

Watanzania, msiogope huu ni muda wa mambo yasiyowezekana kuwezekana. Hakuna uchaguzi uliokuwa umejawa na ndoto nyingi kama huu wa mwaka huu.

Wazee waliota, vijana waliota na watoto pia waliota na wakasema walichokiota na kuandika chini ya kuwa Lowassa ndiye atakuwa Rais wa nchi hii. Hakika ndoto ni BAYANA na MUNGU HADHIHAKIWI.

"Kilichotoka kwa Mungu hakuna mwanadamu wa kukizuia ila kitacheleweshwa kidogo tu kufikia malengo yake"

TANZANIA MPYA INAKUJA.
 
Back
Top Bottom