Nchi 5 zenye jeshi imara afrika Tanzania haipo pamoja na sifa zote wanazojipa

Hapa Tz hakuna jeshi ...yaani unakuta Askari police au mwanajeshi kakondeana utadhani anamwaka mzima Ajala hata chakura ....Alafu wanatuambia tarh 26. /04 tusiandamane kuwa watatuvunja miguu au kutuua kabisa ...kiukweli uwa nashangaa mno ..Labda itokee miujiza trh 26/04 la sivyo iyo kazi yao wataijutia kuifanya.
Ajala= hajala
Chakura=chakula
Utakua nshomile wewe lugha mgogoro.
 
Kwani Tanzania tupo wazi sana upande wa jeshi?..au hizo data wanapataje wao?
 
Tovuti ya Global fire.com kila mwaka inatoa safu ya jeshi duniani kutokana na ubora wake wa kijeshi unaotokana na ubora wa jeshi katika nchi husika. Safu ya utofauti wa kijeshi kwa nchi za kiafrika zenye nguvu za kijeshi na kivita zimetajwa mwaka huu.



Katika kuandaa safu ya nchi yenye nguvu wanahusisha vigezo vifuatavyo: wastani wa idadi ya watu walio mstari wa mbele vitani na idadi ya waliobaki kama akiba ikiwa wameingia vitani. Idadi ya mizinga na magari yaliyojihami kupigana. Manuari yenye kituo cha ndege za kushambulia, ndege zenye uwezo wa kuepusha mashambulizi, na helkopita.

Pia wanaangalia uwezo wa jeshi kusambaza vifaa kama malazi, vifaa vya jeshi kwa jeshi lake, teknolojia inayotumiwa na jeshi, bajeti ya ulinzi na usalama kwa nchi husika na uwezo wake wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi.

Katika kupanga safu pia nchi ndogo kieneo na yenye idadi ndogo ya watu ila ina uwezo mkubwa wa kiitelijensia zinapabanishwa na nchi kubwa kieneo lakini haina intelijensia nzuri, tatizo kubwa la nchi ndogo kuweza kuwekwa safu ya kwanza licha ya intelijensia yake kuwa nzuri ni uwezo wake mdogo wa kuweza kulinda pwani yake kutokana na kutokuwa na uwezo wa manuari za kijeshi endapo ikishambuliwa kutokea majini.

Pia wanaangalia uwezo wan chi kulipa deni lake ikiwa inadaiwa, uwezo wake wa ubadirshaji wa fedha za kigeni au dhahabu.
Kutokana na vigezo hivi nimekusogezea nchi kumi zenye uwezo mkubwa wa kijeshi barani afrika.

Nchi yenye jeshi imara africa


Misri
Misri ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $4.4 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla

Misri ina wastani ya watu wapatao 94,666,993, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 35,306,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 1,535,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 1,329, 250. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 454,250 na wanajeshi 875,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.

Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 1,132.

Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini) wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 22,080.

Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari pamoja na nyambizi za jeshi zipatazo tano. Kwa ulinzi wa majini nchi ya misri ina jumla ya silaha 319.

Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.

Nchi ya misri ina uwezo wa kuzalisha mapipa 478,400 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 740,000 kwa siku. Huku ikiwa na akiba ya mapipa 4,400,000,000.

Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa vita. Nchi ya misri ina bandari 7, zaidi ya kilomita 65,050 za barabara, kilomita 5,083 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 83.


Algeria
Algeria ni nyingine barani afrika iliyoendelea sana kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $10.6 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla.

Algeria ina wastani ya watu wapatao 40,263,711, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 20,400,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 675,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 792,350. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 520,000 na wanajeshi 272,350 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.

Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 502 ikiwa ni ndogo kulinganisha na nchi kama Misri.

Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini) wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 9,825.

Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari pamoja na nyambizi za jeshi zipatazo sita. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Algeria ina jumla ya silaha 85.

Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.

Nchi ya Algeria ina uwezo wa kuzalisha mapipa 1,370,000 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 350,000 kwa siku. Huku ikiwa na akiba ya mapipa 12,000,000,000.

Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa vita. Nchi ya Algeria ina bandari 9, zaidi ya kilomita 111,261 za barabara, kilomita 3,973 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 157.


Ethiopia
Ethiopia ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola milioni $340 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla

Ethiopia ina wastani ya watu wapatao 102,374,044, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 40,000,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 1,950,000 , jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 162,000. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 162,000 na wakiwa hawana wanajeshi wa akiba.

Wana uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 80.

Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini) wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 2,568.

Hawana manuari na nyambizi za jeshi kutokana na jiografia ya nchi yao.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.

Nchi ya Ethiopia ina uwezo wa kuzalisha mapipa 100 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 57,000 kwa siku. Huku ikiwa na akiba ya mapipa 430,000.

Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa vita. Nchi ya Ethiopia ina bandari 2, zaidi ya kilomita 36,469 za barabara, kilomita 681 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 57.


Nigeria
Nigeria ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana kijeshi licha ya changamoto za ugaidi kwa kigundi cha itikadi kali ya kiislamu Boko Haramu ambacho kimekuwa na tabia ya kuteka na kuuua wananchi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $2.33 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla.

Nigeria ina wastani ya watu wapatao 186,053,386, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 72,400,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 3,456,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 181,000. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 124,000 na wanajeshi 57,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.

Uwezo wake wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 110.

Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini) wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 1962.

Uwezo kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari, wakiwa hawana nyambizi. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Nigeria ina jumla ya silaha 75.

Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.

Nchi ya Nigeria ina uwezo wa kuzalisha mapipa 2,423,000 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 302,000 kwa siku. Huku ikiwa na akiba ya mapipa 37,000,000,000.

Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa vita. Nchi ya misri ina bandari 3, zaidi ya kilomita 193,200 za barabara, kilomita 3,505 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 54.


Afrika kusini
Afrika kusini ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana kijeshi na yenye uchumi mzuri ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $4.61 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla

Afrika kusini ina wastani ya watu wapatao 54,300,704, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 26,000,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 965,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 94,050.

Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 78,050 na wanajeshi 16,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.

Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 231.

Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini) wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 2650.

Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari pamoja na nyambizi za jeshi zipatazo tatu. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Afrika kusini ina jumla ya silaha 30.

Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.

Nchi ya Afrika kusini ina uwezo wa kuzalisha mapipa 3000 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 605,000 kwa siku. Huku ikiwa na akiba ya mapipa 15,000,000.

Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa vita. Nchi ya Afrika kusini ina bandari 5, zaidi ya kilomita 362,099 za barabara, kilomita 20,192 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 566.
"wanajipa"...lini JWTZ wanajipa sifa?
 
Watanzania mnajenga chuki sana kwa vitu ambavyo mnapaswa kujifunza na kuelewa kwa kina kuhusu jeshi. Kuna vitu lazima uviangalie
1. Bajeti ya ulinzi na usalama kwa mwaka
2. Idadi ya askari na vifaa
3. Uwezo wa kuhudumia jeshi kwa mavazi na ubora wa mafunzo n.k pia mtambue kuna majeshi ya serikali (nation army) na majeshi ya wananchi( people defence force) na Tanzania sisi tupo katika jeshi la Defence force na wanajeshi wetu hawalipwi mshahara maana serikali haina uwezo wa kumlipa mshahara mwanajeshi bali wanalipwa posho za kujikimu yote kwa yote ubora walionao lakni ndio nchi zinazoongoza kwa machafuko na uasi mfano. Nigeria bokoharam toka nazaliwa hadi leo wameshindwa kuwatoa alafu bado utasema ni bora
 
Tatizo mnataka jeshi lifanye matakwa yenu kwa manufaa yenu ya kisiasa na kuacha jukumu kuu la kulinda nchi na mipaka yake kuwa salama
 
Watanzania mnajenga chuki sana kwa vitu ambavyo mnapaswa kujifunza na kuelewa kwa kina kuhusu jeshi. Kuna vitu lazima uviangalie
1. Bajeti ya ulinzi na usalama kwa mwaka
2. Idadi ya askari na vifaa
3. Uwezo wa kuhudumia jeshi kwa mavazi na ubora wa mafunzo n.k pia mtambue kuna majeshi ya serikali (nation army) na majeshi ya wananchi( people defence force) na Tanzania sisi tupo katika jeshi la Defence force na wanajeshi wetu hawalipwi mshahara maana serikali haina uwezo wa kumlipa mshahara mwanajeshi bali wanalipwa posho za kujikimu yote kwa yote ubora walionao lakni ndio nchi zinazoongoza kwa machafuko na uasi mfano. Nigeria bokoharam toka nazaliwa hadi leo wameshindwa kuwatoa alafu bado utasema ni bora
Kwani hata hapa kwetu si machafuko hapo njiani na yanahamasishwa na ccm na serikali yake
 
Hahaha naona nchi inawashinda sasa ni kuua kuteka na kucharanga mapanga tu
We huoni kama ccm na serikali yenu mnayahamasisha machafuko
 
Hapa Tz hakuna jeshi ...yaani unakuta Askari police au mwanajeshi kakondeana utadhani anamwaka mzima Ajala hata chakura ....Alafu wanatuambia tarh 26. /04 tusiandamane kuwa watatuvunja miguu au kutuua kabisa ...kiukweli uwa nashangaa mno ..Labda itokee miujiza trh 26/04 la sivyo iyo kazi yao wataijutia kuifanya.
Utafanya nini mkuu?? Angalia Sana usijiamin sana ukiwa nyuma ya keyboard kuandika kwa hasira au chuki hakusaidii ww kaza kupambana na hali yako usitoe maneno ya kashfa kwa majeshi yetu
 
Back
Top Bottom