NCCR Mageuzi yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake!

Hizi demokrasia uchwara baadhi ya ubaya wake ndio kama hivi.............yaani Walipa kodi sasa itabidi waingie gharama za uchaguzi mdogo eti kwasababu NCCR imemfukuza Kafulila uanachama............damn!.........

Fundamental right ya wananchi waliomchagua Kafulila iko wapi?......
 
Nilimwambia Kafulila kwamba VYAMA VINGINE VINA WENYEWE NA WENYEWE NDIYO WALIOMFUKUZA. Arudi cdm aombe radhi kama mwana mpotevu.
 
Kama Kafulila alilia kweli jeuri yake yote ilikuwa ya nini kupayuka kila mara? Hata hivyo naye ana matatizo kama Mbatia maana ukiangalia alivyopeleka majungu na tamaa CHADEMA unamuonea huru. Hata hivyo asikonde. Mbatia naye atafuatia baada ya Maalim Seif kutimuliwa CUF.

Go Kafulila go,
Go Kafulila it is time to go
Go never turn back go
Go lick your vomits go
Go drink from the mess you brew go
Go Kafulila go
Worry not go
Mbatia too will go
Go Kafulila g,
Go it the right time to go
Go Kafulila go.
 
Hivi Zitto anahusika nini na mkutano wa NCCR? sometimes huwa simwelewi.

Nadhani~Zitto~Ule ugonjwa wa kipanda uso bado unamsumbua. Ndiyo maana masaa yote anawashwa, kushadadia mambo ya kijinga! Na pia nasikia ni mdau mkubwa wa ule mkakati wa CCM kuanzisha chama kipya kitakacho kuwa na idadi kubwa ya vijana ilikupunguza vijana wa CDM. Hatimaye CCM kiweze kupenya kwenye tundu la shindano uchaguzi 2015. Na pia Zitto ni mamluki wa jk, na yuko sawa kwa viroja anavyofinya kutimizi matakwa ya Jk!!!
 
Sina hakika NCCR-Mageuzi wana ubavu wa kulirudisha jimbo. Waulizwe CCM Igunga wanaweza kutoa ushuhuda mzuri
katika hili
 
Mbatia hapa haangalii kurudisha ua kulikosa jimbo bali ku-survive. Mbatia is useless and desperate. Viongozi wa aina ya Mbatia hawaoni wala hawana akili ya kawaida common sense bali kulinda kitumbua chao. Waangalie Seif, Mrema, Cheyo na wengine mafisi kama hao.
 
Hivi haki ya maelfu ya wananchi walomchagua Kafulila iko wapi?
Wachache walokuwa kikaoni jana ndio wamemtimua na hivyo atakosa ubunge.

Na kwa maana hiyo wachache wameshinda na wachache hao hao wanawapa wengi (wananchi) hasara ya muda na gharama za uchaguzi mpya mdogo(kwa kodi zetu).
 
Huyu Kafulila kwa vyo vyote ana tatizo. Kama aliiona Chadema wabaya sasa amekwenda kukutana na wabaya wenyewe, maana Chadema walimnyang'anya madaraka tu kwa ajili ya kumfunza adabu, lakini NCCR wamefanya kweli kuondoa udhia. Kwa vyo vyote Kafulila anatatizo na kama hajisahihishi kila anakokwenda matatizo yatakuwa ni yaleyale. Kujifanya unajua sana nitatizo.

Nawashauri vijana wenzangu kuwa karibu na wazee kupata ushauri, maana vijana damu inachemka, na wanaona wanaweza kufanya lolote likawezekana, lakini hekima na busara ni haba, hapo ndipo mambo yanapowaharibikia vijana na ndoto zao kubaki za kuwazika tu.
 
...hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Undava undava tu.
Siasa ni balaa, leo una kibarua, kesho omba omba.
Maskini Kafulia ooh!, Kafulila pole sana kaka. Ni muhimu kusoma misingi ya eneo husika kuliko kutokea ndani ya mwaka unataka kumiliki chama. Hii ni Afrika na hapa ni Tanganyika. Najua utaendelea ila ni vema kujifunza.
 
Dah,imeniuma sana,watu hawana ubinadamu,Mtu hadi kapiga magoti,kalia akiomba msamaha,watu hawajamsamehe,aisee
 
Mbunge wa Kigoma kusini Mh.David Kafulila na wajumbe wengine sita(6) wafukuzwa uanachama ndani ya NCCR akiwamo alie kuwa mgombea urais wa chama hicho 2010,Bw.Hashim Rungwe.

Maamuzi hayo yaliotolewa na kikao cha dharura cha NEC ya chama hicho yalifanyika jijini Dar.

Wengine waliofukuzwa ni Lucy Kapya na Ally Mbwana.

Inasemekana Kafulila aliomba msamaha na kudai hatarudia tena mbele ya Jemes Mbatia,ambaye ndo mwenyekiti wa chama chaNCCR,alipokua tayari kukubali wajumbe wa NEC wakagoma na kudai kijana huyo hafai na ana kiharibu chama.
 
Magazeti yamepata cha kuandika kwa siku mbili tatu....

Mbatia anaweza kushinda katika hili, ila mwanzo wa mwisho wake ndo huu.
 
Back
Top Bottom