NCCR na MASLAHI YA TAIFA

Kahangwa tangu mwanzo sikujua nazungumza na mtu ambaye ni learned. Ahhh kumbe nazungumza na mtu aliyesoma na kwa maana nyingine ni mwepesi kujua upepo.

Nilikuwa wa kwanza kusema "NCCR is a dead thing" katika thread hii na kwa hiyo uliposhambulia katika hilo ulinilenga mimi.

Ni lazima ndugu yangu nikiri kwanza kwamba nililisema hili kutokea ndani ya moyo wangu na wala sijatumwa na chama chochote.

Kama walivyosema wengi mimi ni mmoja kati ya watu waliopenda sana mageuzi nyakati zile za NCCR mageuzi ya wakina Mabere na Bagenda na Baregu, n.k. Sioni aibu kusema 1995 niliwapa kura yangu na nilikipenda chama hiki, kabla hakijaingia mizengwe.

Lakini pia nikiri wazi kwamba pamoja na upenzi wangu wa vyama vilivyo na mlego wa upinzani kwa sababu sisiemu niligundua ni waongo na wachumia tumbo kwa migongo ya walala hoi, sijawahi kuwa na kadi ya chama chochote cha siasa, zaidi ya kadi moja tu niliyoipata nikiwa JKT Ruvu mwaka 1983 kwa lazima, maana ilikuwa ni lazima uwe mwanachama wa sisiemu na kadi ulikuwa unapewa upende usipende.

Nilidumu na kadi hiyo hadi 1985 ambapo niliamua kuitupa mwenyewe. Hii ina maana wala sikuikabidhi kwa kiongozi wa chama kingine cha kisiasa kama wanavyofanya wengi siku hizi. Bali niliamua kuitupa kabisa tena C***ni.

Sasa ninapopima mwelekeo wa chama sipimi kwa kuangalia maslahi ya chama kinachonimiliki, hapana, ninapima kutokana na current political era.

Kusema ukweli, natamani kupata na mimi chama kimoja cha kujiunga na sijakipata, lakini niko kwenye mchakato wa je ni kipi kinanifaaa? Na hapo nilipokuwa naendelea na mchakato, kwa NCCR mageuzi nimeshaweka X.

Kumbuka bado naendelea na mchakato. Hata hivyo lazima nikiri pia naona kama muelekeo wa CHADEMA unanivutia. Uenda siku moja nikawa mwanachama wao kama wataendelea kwa jinsi ninavyoona. Wakibadirika nami sintakwenda huko maana si lazima niwe na chama. Nitapiga kura tu yule aliye na sera safi, na zinazoigwa na chama tawala.

Kuhusu masuala ya siasa za nchi hii nayaelewa kwa sehemu kubwa maana kwa umri huu nilionao ( above 50 ) mtu hawezi kunidanganya chochote katika siasa. Najua tunakotoka, lakini najua pia tunakoelekea. Najua nilikopenda lakini najua pia kulipobomoka. Hapo mtu hawezi kunidanganya. Hapana. Hizi siasa za "hiki ni chama kilichozaliwa enzi za baba na mama" wakati wako taabuni, zimepitwa na wakati. Au siasa za "Kidumu" mimi hazinivuti katika kokolo lao.

Kitu kimoja tu nimeshangaa ni kwamba watu wengi katika thread hii wameonyesha kuwa kinyume na NCCR mageuzi na sababu baadhi wamesema. Na wewe umekuwa ukihisi wanafanya self attack kwako. Hapana. Hawa wanajua wazi kwamba kwa sasa NCCR mmepoteza mwelekeo na si ile ile ya zamani tuliyokuwa tunaipigia debe na kuipenda.

Kumekuwa na kulega lega katika uongozi. Na hili si haba. Kila mtu anajua.
NCCR inayosema kuwa iliasisi mageuzi si hii ya leo, ingawa ni kweli kwamba tangu mwanzo ni chama hiki kiliasisi mageuzi ya nchi hii. Msipo jirekebisha mtabaki kuimba wimbo huo kama wenzenu wa sisiemu wanavyoimba kuwa wao ndiyo waasisi wa uhuru na amani ya nchi hii. Mtajikuta mmepigwa chali.

Chukulia challenge unayokutana nayo hapa kama challenge ya kweli maana mbali na kwamba tunayajadili na kuyazungumza hapa JF bado ndiyo yaliyo katika sehemu nyingi ya jamii tunayoishi nayo na inayotuzunguka maana tunayajadili sana huku vijijini tunakoishi. Ukichukulia kuwa haya ni mawazo ya sisi hapa, shauri yako maana hulazimiki kuyakubali.

Mwisho nataka kukwambia kuwa mimi naweza kurudisha imani yangu kwa NCCR itakapofufuka maana is a dead thing. Usishangae siku moja kunikuta ni kadi ya chama chenu maana bado natafuta chama. Lakini chama kama chenu ambacho hakikubali hata umoja na wengine simply tu kwa sababu kinatafuta kuingia ikulu au bungeni! sintakikubali! maana mwisho hata uko katika chama tutapoteza umoja ikifika nani agombee katika chama!.

Hii umethibitisha wewe mwenyewe kwa maneno yako kwamba katika upinzani mna maadui. Na mimi sijui iweje muwe na maadui katika upinzani wakati nanyi ni wapinzani. Kwa hiyo tuseme nyinyi si wapinzani tena?

TUNATAKA MAGEUZI YA KWELI SI HIZI POROJO AMBAZO WALA HAZIWAOGOPESHI SISIEMU MAANA WAMEZISIKIA KILA SIKU.

Mchukia Fisadi,
Ahsante sana kwa mchango wako. Hata hivyo nasikitika sana mnapoamua kuchukulia mambo haya too personal, haya maneno ya kahangwa umesoma..umesoma, sijapenda mlivyoyaingiza katika mjadala huu. Hoja niliyowaomba watanzania wenzangu ni kujadili maslahi ya taifa, yawezekana mtoa hoja (NCCR) mmmemchukia sana kiasi cha kumtangazia kifo, well hayo yanabaki kuwa maamuzi yenu, lakini bado hoja iliyotolewa ni muhimu kwetu sote, awaye yeyote asidhani kulileta hili kwenu mimi nina maslahi binafsi, tambueni kwamba usomi mnaonishambulia nao kwa sasa unanipa riziki ya kunitosha kabisa.Nikiamua leo kuwa mbinafsi (kama wasomi wengine/baadhi wanavyofanya),nitajitoa katika mijadala inayolihusu taifa langu, jambo ambalo litakuwa ni usaliti.
Tafadhalini tujadili yahusuyo taifa letu, kama ni ufu wa NCCR basi ulianza na wewe uliyeamua kukimbia badala ya kukisahihisha chama kipenzi chako.
 
pole kahangwa....

Mbio za sakafuni huishia ukingoni.. Tanzania kuna chama kimoja tu kimebaki... CHADEMA, omba Mungu wakukubali aisee
 
Nimeanza kuwaamini watu Mbatia na NCCR yake ipo kwa maslahi ya CCM, tena kuiuwa CDM, tamko kama hili ndio linazidi kuijenga CDM, kama vp kamanda Machali njoo chadema tupige mzigo huko naona majungu, fitina na makundi... Join CDM mpiganaji wa ukweli
 
Imekaa kama tamko la Kafulila featuring Zitto, via NCCR anyway ni mtazamo tu!
 
Imekaa kama tamko la Kafulila featuring Zitto, via NCCR anyway ni mtazamo tu!

Tamko hili lilitolewa kabla wewe hujajiunga JF, kabla kafulila hajawa mwanachama wa NCCR-Mageuzi, na lilitokana na malumbano yaliyokuwako wakati ule, hususan suala la OIC
 
Back
Top Bottom