NCCR na MASLAHI YA TAIFA

Mimi ninaposikia au soma NCCR - Mageuzi napata kichefuchefu mpaka nakosa akili, chama hiki nilikipigia kura mwaka 1995, sikujua ubaya wake masikini, ingekuwa bora kife kabisa sasa.

Kimsingi, natamani Tanzania tuwe na Chama kimoja cha upinzani chenye nguvu. Sasa hawa NCCR ni kama DP tu, kuvuruga upinzani. kife, kife kabisa, sitaki kukisikia.

Nzikuuuu!
Wadhani chama kimoja chenye nguvu kitapatikana kwa kuiombea NCCR mauti?
 
Tatu, suala la Tarime, niwambie wazi kwamba sababu kubwa ya NCCR kutofanya vizuri Tarime ni propaganda ya adui yetu tunayemjua aliyeamua kueneza uongo kwamba sisi tumetumwa na CCM na kwamba ana ushahidi.

Duh! Kumbe kuna chama cha upinzani cha chama cha upinzani !
 
Tanzanianjema,
I hope you are not trying to intimidate me and you are not accusing NCCR of plagiarism, ARE YOU?

As i said...Kipanga darasani lakini sio katika siasa kaka......

Nimi nduguyo katika mapambano enzi zile...

Tanzanianjema
 
George,

Watanzania walikuwa wanaelekea kuisamehe NCCR kwa uasi walioufanya baada ya uchaguzi wa 1995. Lakini hili mlilolifanya kule Tarime limewathibitishia wapenda mageuzi pasipo chemba kuwa lengo la NCCR sio zuri na sidhani kama watanzania watakuwa tayari kuwasamehe tena. In fact sasa utafanya kazi kubwa mno kuwashawishi mwananchi yeyote, hasa wa vijijini wanaojua siasa vizuri za Tanzania, kwamba NCCR nacho ni chama serious cha upinzani. Bahati mbaya hatuna peridic opinion polls, lakini hata hivyo ukitaka kuhakikisha nafasi yenu subiri uchaguzi wa mwaka kesho na 2010, utaniambia.

Ulichonimaliza zaidi ni kuendelea kushikilia msimamo kwamba NCCR ndio ilistahili kusimamisha mgombea Tarime hata baada ya kupata kura chini ya 1000!! Ina maana nyie mlikuwa tayari jimbo liende kwa CCM madamu NCCR waweke mgombea?

Kama walivyosema wengine, wewe ni mtu makini lakini kuendelea kutetea makosa yaliyofanyika, ama kwa kujua au kutokujua, unatuchanganya sana sisi tunaokujua.

Mwisho, madamu mmeamua kuwatupa chadema katika ushirikiano wenu, basi hakuna haja ya kuendelea kuwanyooshea kidole; nyie endeleeni kufanya siasa na wenyewe waacheni waendelee kivyao, na wananchi wataamua huko mbele. Uzuri wa siasa, judge ni wapiga kura.
 
Kahangwa,

Bado najiuliza kwanini wapinzani msiunganishe nguvu? Natamani mgombea binafsi angewezekana kwa Tanzania!

Mkuu Invisible,
Thread hii ikupe clue ya kwanini hilo jambo jema unalolitaja linakuwa gumu kwa Tanzania, ndani ya vyama kuna ubinafsi, unafiki, kutoaminiana na baadhi wanaamini 'they can do without others' Waweza kuona kwa mfano, alichoniandikia paparazi kwamba kuna tuhuma eti mpango wa kuunganisha vyama ilikuwa ni janja ya NCCR, well kwa kuwa ameahidi kuja kunitembelea ninakofanya kazi, nitamweleza ukweli ninaoujua, msisitizie nitakachomwambia aandike hapa JF au gazetini kwake ili watanzania mjue sababu halisi ya kushindikana kwa uunganishaji wa nguvu za wanamageuzi.
 
Dah,

Mkuu wangu Kahangwa, kina Kitila na Mnyika ni wenzenu katika mapambano, kutofautiana kwenu kimitizamo na itikadi ni changamoto kwetu tusio na vyama maalum. Inatufundisha mengi na hoja zenu wapinzani pamoja ningeomba zilenge kuangalia maslahi ya taifa.

Kwakuwa JF ni open dialogue, sintoshangaa mkipigana vijembe, lakini mwisho wa siku tugongeshe glass na kutakiana mema!

Tunagundua mengi na kuujua udhaifu wa vyama vyetu. Bado nalilia mgombea binafsi, japo nayo inataka mjadala mrefu kwani ina athari zake!
 
Mkuu Invisible,
Thread hii ikupe clue ya kwanini hilo jambo jema unalolitaja linakuwa gumu kwa Tanzania, ndani ya vyama kuna ubinafsi, unafiki, kutoaminiana

Kaka ni ukweli kabisa. Mimi naongeza siasa hohehahe za kizazi cha mwanzo cha "wanamageuzi".

Sasa ninyi kizazi kipya badala ya kuelewana na kufanya siasa nje ya wigo huo ndio kwanza mnakubali siasa za kizamani. Inapofika Kahangwa anaamini Zitto ni adui....Zitto anayemjua yeye zaidi ya kina MBATIA, hio ni dalili mbaya.

Kaka rudia kusoma responce yangu ya mwanzo kwa umakini....ni kwa nia njema kabisa

Tanzanianjema
 
George,
Watanzania walikuwa wanaelekea kuisamehe NCCR kwa uasi walioufanya baada ya uchaguzi wa 1995. Lakini hili mlilolifanya kule Tarime limewathibitishia wapenda mageuzi pasipo chemba kuwa lengo la NCCR sio zuri na sidhani kama watanzania watakuwa tayari kuwasamehe tena. In fact sasa utafanya kazi kubwa mno kuwashawishi mwananchi yeyote, hasa wa vijijini wanaojua siasa vizuri za Tanzania, kwamba NCCR nacho ni chama serious cha upinzani. Bahati mbaya hatuna peridic opinion polls, lakini hata hivyo ukitaka kuhakikisha nafasi yenu subiri uchaguzi wa mwaka kesho na 2010, utaniambia.

Ulichonimaliza zaidi ni kuendelea kushikilia msimamo kwamba NCCR ndio ilistahili kusimamisha mgombea Tarime hata baada ya kupata kura chini ya 1000!! Ina maana nyie mlikuwa tayari jimbo liende kwa CCM madamu NCCR waweke mgombea?

Kama walivyosema wengine, wewe ni mtu makini lakini kuendelea kutetea makosa yaliyofanyika, ama kwa kujua au kutokujua, unatuchanganya sana sisi tunaokujua.

Mwisho, madamu mmeamua kuwatupa chadema katika ushirikiano wenu, basi hakuna haja ya kuendelea kuwanyooshea kidole; nyie endeleeni kufanya siasa na wenyewe waacheni waendelee kivyao, na wananchi wataamua huko mbele. Uzuri wa siasa, judge ni wapiga kura.

Don Mkumbo,
Nawe pia waenda huko? Kwa heshima nakusihi ujadili mada; National interests! Wasema vyema, wananchi wataamua, sasa ya nini basi kuiponda NCCR inapokuja na mada ya kutanguliza maslahi ya taifa mbele?
 
Kaka ni ukweli kabisa. Mimi naongeza siasa hohehahe za kizazi cha mwanzo cha "wanamageuzi".

Sasa ninyi kizazi kipya badala ya kuelewana na kufanya siasa nje ya wigo huo ndio kwanza mnakubali siasa za kizamani. Inapofika Kahangwa anaamini Zitto ni adui....Zitto anayemjua yeye zaidi ya kina MBATIA, hio ni dalili mbaya.

Kaka rudia kusoma responce yangu ya mwanzo kwa umakini....ni kwa nia njema kabisa

Tanzanianjema
That's nice of you Tanzanianjema... I like it!
 
Kaka ni ukweli kabisa. Mimi naongeza siasa hohehahe za kizazi cha mwanzo cha "wanamageuzi".

Sasa ninyi kizazi kipya badala ya kuelewana na kufanya siasa nje ya wigo huo ndio kwanza mnakubali siasa za kizamani. Inapofika Kahangwa anaamini Zitto ni adui....Zitto anayemjua yeye zaidi ya kina MBATIA, hio ni dalili mbaya.

Kaka rudia kusoma responce yangu ya mwanzo kwa umakini....ni kwa nia njema kabisa

Tanzanianjema

Naona umeamua kunichonganisha na Zitto, unadhani utafanikiwa?
 
Nilisoma maoni ya mchangiaji mmoja aliyesema kwamba ndio wakati wa NCCR Mageuzi kutoka na nadhani nu ukweli mtupu!Nyota sasa itawang'aria!Wataonekana na wao they are doing something!
 
Kahangwa,
Mkuu nakuuliza kitu kimoja hapa.. Kulingana na mada hii huoni kama unajaribu kutetea kitu wakati unazidisha gap ya utengano..
Sasa kama swala lako ni maslahi ya Taifa na unashindwa kuona haja kubwa ya kuwepo maelewano kati ya watu, vyama na kuziweka tofauti zetu kando kuweza kujenga jamii moja itakuwaje iwe rahisi ktk maswala mazito ya Kitaifa kama ulivyopendekeza!..
kama huwezi kuwa na suluhu na jirani yako mtaweza vipi kukabiri maadui toka nje!.. huoni kwamba mawazo yako yanazidi kubomoa badala ya kujenga?
 
Mkandara,
Wanaoharibu masikizano hapa ni wale walioacha kujadili mada wakaanza kurusha makombora kwa NCCR, ooh mara ife, mara ilitumwa na CCM, mara vitu gani, wakemee basi hao. Mimi niko tayari kwa majadiliano ya amani na mtu awaye yeyote yule, kama hilo ndilo na wenzangu wanaona linafaa, basi waweke kashfa na uongo pembeni tujadili issues.
tukubaliane, mwenye uongo wake auzuie ulimi wake, na mwenye roho ya kukashfu aikemee, sote tuiangalie Tanzania yetu kwa nia njema na kushauriana juu ya mustakabari mwema wa taifa hili.
 
Ndugu wana JF,
Nashukuru sana kwa mchango wenu unaodokezea picha potofu inayojengwa kuhusu chama cha NCCR-Mageuzi.Awali ya yote naomba niweke wazi kwamba mimi ni George Kahangwa, mwanachama wa NCCR-mageuzi, sioni sababu ya kuficha ukweli huo, maana ni vizuri niseme sasa ili hata mnapoendelea kututumia makombora mjue yanafika na tunaendelea kuyatafakari na kuyaona kama changamoto kwetu maana tunaamini ninyi ni watanzania na myasemayo ni sehemu ya ujumbe mlionao kwetu, japo yameghubikwa na hoja zilizojengwa juu ya uongo.

Napenda kutofautiana nanyi katika mambo kadhaa:
Mosi, si kweli kwamba NCCR ni a dead thing, we are alive and well. Kufa kwa chama huthibitishwa na msajiri wa vyama vya siasa kwa kufuata vigezo rasmi. vipo vyama vilivyokwisha kufa na kufutwa, nanyi mnalijua hilo.Aidha kumbukeni nchi yetu kwa sasa ina vyama vya siasa 18, vipo vinavyosikika vikifanya kazi na vipo vilivyosinzia, fanyeni tathmini ya kina ili madai yenu ya ufu wa chama yawe na msingi. chama gani mnathubutu kusema kimekufa wakati mnajua vizuri kinaongoza serikali za vijiji na kina madiwani kadhaa hapa nchini, nk.

Tunajua chanzo cha propaganda hii, tunamjua kiongozi mwandamizi wa chama fulani anayezunguka nchini akiwaaambia watanzania kwamba NCCR imekufa, tulipombaini na kumwuliza kulikoni akatuma ujumbe wa kutuomba radhi, au mwataka nimtaje jamani...

Pili,kumbukeni ujumbe tuliouandika unahusu maslahi ya taifa, someni vizuri ili mtambue kwamba hatudandii hoja bali tunatekeleza wajibu wetu kama chama cha siasa wa kutoa rai kwa jamii nzima ya kitanzania, hatukuiandika serikali tu na hata hivyo serikali isiposikiliza sisi tumetimiza wajibu wetu.

Tatu, suala la Tarime, niwambie wazi kwamba sababu kubwa ya NCCR kutofanya vizuri Tarime ni propaganda ya adui yetu tunayemjua aliyeamua kueneza uongo kwamba sisi tumetumwa na CCM na kwamba ana ushahidi.Mtakeni basi atoe ushahidi, vinginevyo itakuwa ni jambo la kusikitisha kama watanzania mtaendelea kuushabikia uongo ushinde na kutamalaki juu ya ukweli, wanatarime walituhukumu kwa kudhani ni kweli tumetumwa na CCM.

Wakati huo huo mtakumbuka kulikuwa na uchaguzi mwingine mdogo kule Nguruka, NCCR tukaishinda CCM, lakini vyombo vya habari vilivyolishwa sumu ya uongo vikaandika kuwa ni CHADEMA imeshinda Nguruka, tafuteni basi ukweli nani alishinda kule Nguruka.

Vile vile mtakumbuka kuwa chama chetu pamoja na vyama vingine vitatu tuko katika ushirikiano, katika suala la Tarime vyama hivi tulikaa kukubaliana kumsimamisha mgombea mmoja, katika kikao kilichofanyika huko huko Tarime tarehe 11 September, vyama hivi vilimpitisha mgombea wa NCCR, lakini CHADEMA hakikukubaliana na hayo,kikasimamisha nacho mgombea.Huu ukweli msiukimbie, pendeni kujua hasa ni nini kilitokea Tarime.Mkitaka niulizeni ikawaje CHADEMA kikashinda.

Nne, kuhusu mchango wa NCCR katika mageuzi nchini, uko wazi labda kwa wasiojua historia ya mageuzi nchini.Kwa ufupi tu kumbukeni NCCR ilianza kama vuguvugu la wanamageuzi nchini hata kabla ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Kutoka NCCR vilizaliwa vyama vingi sana kikiwemo hicho ambacho baadhi ya wanajf hapa mnaonekena kukishabikia sana.Someni historia hiyo, mtagundua pia kuwa kumbe hata jina la chama kipenzi chenu limetokana na maneno ambayo hadi leo yako katika nembo ya NCCR.

Binafsi mimi ni shuhuda wa jinsi ushirikiano wa vyama ulivyoanzishwa, na nilikuwepo siku tamko la ushirikiano linaandaliwa pale makao makuu ya NCCR, siku chache kabla ya tamko kutangazwa tr.10 May 2007.Ndugu zangu niwashirikishe siri ninayoijua,kabla tamko halijatoka neno ushirikiano lilisomeka muungano, aliyelibadili tunamjua na huyo ndiye mnapaswa kumtupia madongo ya kutokuwa na mchango wa kuviimarisha vyama vya upinzani.

Suala la muungano, NCCR tulilipendekeza kwa wenzetu mara kadhaa (na ushahidi upo) tulilipendekeza baada ya kulifanyia utafiti wa kina nchini (research report ipo), Hamtutendei haki kusema hatuna mchango wowote katika mageuzi ya nchi hii, kusema hivyo ni kupotosha ukweli.

Wana JF, yafaa basi tusimamie ukweli kuliko ushabiki.

NCCR Mageuzi ni waganga njaa ambao wako tayari kuuza haki na utu wa mlalahoi Mtanzania ili washibe.
 
Kahangwa,

Mkuu hawa jamaa wanaandika matakwa yao na sidhani kama haya matakwa yao yanaweza kubadilisha sura nzima ya NCCR kuwa mbaya zaidi kama mtaweza kufikiria ama kuomba sababu zao. Na hoja zao haziwezi kuharibu maslahi ya nchi wala maslahi ya wananchi wenyewe kama NNCR itakufa kwa sababu hiki ni chama na wewe Kahangwa utaendelea kuwepo na kupendwa na wananchi wote kama Mtanzania, bado tutaendelea kuungana panapohitajika.
Nadhani ni muhimu kwako kujitazama vizuri zaidi pale uliposimama na kile unachosimamia kwani wewe kama kiongozi ama msemaji wa NCCR mageuzi unaweza kuwa sio sababu kubwa ya hawa vijana kukashifu mwongozo wa chama hicho. Kumbuka hapa hawazungumzii wewe isipokuwa chama na mapungufu yake..
Binafsi naongea na wewe kwa sababu sio hawa jamaa walioweka mada hii wala kutaka maslahi ya Taifa yawe na tafsiri hii ambayo inanipa shida ikiwa Preacher mwenyewe amekubali UADUI na anazidi kujenga hoja zinazoonyesha utengano...
Sidhani kama Chadema wanawaita CCM maadui wao pamoja na kwamba kuna mengi mabaya yamewakuta na mara nyingi huelkekeza mashambulizi yao kwa wahusika!.. Mapungufu ya CCM hutajwa kama sio tija ya matatizo ya wananchi na pengine kuwaonyesha wananchi mwelekeo wa chama hicho dhidi ya maslahi ya Taifa..Rostam Aziz ambaye ametajwa sana ktk mada nyingi humu ameonekana kuwa ni Fisadi na adui wa maendeleo yetu na sababu zilizosukuma hoja hivyo huwekwa wazi.
 
Kahangwa tangu mwanzo sikujua nazungumza na mtu ambaye ni learned. Ahhh kumbe nazungumza na mtu aliyesoma na kwa maana nyingine ni mwepesi kujua upepo.

Nilikuwa wa kwanza kusema "NCCR is a dead thing" katika thread hii na kwa hiyo uliposhambulia katika hilo ulinilenga mimi.

Ni lazima ndugu yangu nikiri kwanza kwamba nililisema hili kutokea ndani ya moyo wangu na wala sijatumwa na chama chochote.

Kama walivyosema wengi mimi ni mmoja kati ya watu waliopenda sana mageuzi nyakati zile za NCCR mageuzi ya wakina Mabere na Bagenda na Baregu, n.k. Sioni aibu kusema 1995 niliwapa kura yangu na nilikipenda chama hiki, kabla hakijaingia mizengwe.

Lakini pia nikiri wazi kwamba pamoja na upenzi wangu wa vyama vilivyo na mlego wa upinzani kwa sababu sisiemu niligundua ni waongo na wachumia tumbo kwa migongo ya walala hoi, sijawahi kuwa na kadi ya chama chochote cha siasa, zaidi ya kadi moja tu niliyoipata nikiwa JKT Ruvu mwaka 1983 kwa lazima, maana ilikuwa ni lazima uwe mwanachama wa sisiemu na kadi ulikuwa unapewa upende usipende.

Nilidumu na kadi hiyo hadi 1985 ambapo niliamua kuitupa mwenyewe. Hii ina maana wala sikuikabidhi kwa kiongozi wa chama kingine cha kisiasa kama wanavyofanya wengi siku hizi. Bali niliamua kuitupa kabisa tena C***ni.

Sasa ninapopima mwelekeo wa chama sipimi kwa kuangalia maslahi ya chama kinachonimiliki, hapana, ninapima kutokana na current political era.

Kusema ukweli, natamani kupata na mimi chama kimoja cha kujiunga na sijakipata, lakini niko kwenye mchakato wa je ni kipi kinanifaaa? Na hapo nilipokuwa naendelea na mchakato, kwa NCCR mageuzi nimeshaweka X.

Kumbuka bado naendelea na mchakato. Hata hivyo lazima nikiri pia naona kama muelekeo wa CHADEMA unanivutia. Uenda siku moja nikawa mwanachama wao kama wataendelea kwa jinsi ninavyoona. Wakibadirika nami sintakwenda huko maana si lazima niwe na chama. Nitapiga kura tu yule aliye na sera safi, na zinazoigwa na chama tawala.

Kuhusu masuala ya siasa za nchi hii nayaelewa kwa sehemu kubwa maana kwa umri huu nilionao ( above 50 ) mtu hawezi kunidanganya chochote katika siasa. Najua tunakotoka, lakini najua pia tunakoelekea. Najua nilikopenda lakini najua pia kulipobomoka. Hapo mtu hawezi kunidanganya. Hapana. Hizi siasa za "hiki ni chama kilichozaliwa enzi za baba na mama" wakati wako taabuni, zimepitwa na wakati. Au siasa za "Kidumu" mimi hazinivuti katika kokolo lao.

Kitu kimoja tu nimeshangaa ni kwamba watu wengi katika thread hii wameonyesha kuwa kinyume na NCCR mageuzi na sababu baadhi wamesema. Na wewe umekuwa ukihisi wanafanya self attack kwako. Hapana. Hawa wanajua wazi kwamba kwa sasa NCCR mmepoteza mwelekeo na si ile ile ya zamani tuliyokuwa tunaipigia debe na kuipenda.

Kumekuwa na kulega lega katika uongozi. Na hili si haba. Kila mtu anajua.
NCCR inayosema kuwa iliasisi mageuzi si hii ya leo, ingawa ni kweli kwamba tangu mwanzo ni chama hiki kiliasisi mageuzi ya nchi hii. Msipo jirekebisha mtabaki kuimba wimbo huo kama wenzenu wa sisiemu wanavyoimba kuwa wao ndiyo waasisi wa uhuru na amani ya nchi hii. Mtajikuta mmepigwa chali.

Chukulia challenge unayokutana nayo hapa kama challenge ya kweli maana mbali na kwamba tunayajadili na kuyazungumza hapa JF bado ndiyo yaliyo katika sehemu nyingi ya jamii tunayoishi nayo na inayotuzunguka maana tunayajadili sana huku vijijini tunakoishi. Ukichukulia kuwa haya ni mawazo ya sisi hapa, shauri yako maana hulazimiki kuyakubali.

Mwisho nataka kukwambia kuwa mimi naweza kurudisha imani yangu kwa NCCR itakapofufuka maana is a dead thing. Usishangae siku moja kunikuta ni kadi ya chama chenu maana bado natafuta chama. Lakini chama kama chenu ambacho hakikubali hata umoja na wengine simply tu kwa sababu kinatafuta kuingia ikulu au bungeni! sintakikubali! maana mwisho hata uko katika chama tutapoteza umoja ikifika nani agombee katika chama!.

Hii umethibitisha wewe mwenyewe kwa maneno yako kwamba katika upinzani mna maadui. Na mimi sijui iweje muwe na maadui katika upinzani wakati nanyi ni wapinzani. Kwa hiyo tuseme nyinyi si wapinzani tena?

TUNATAKA MAGEUZI YA KWELI SI HIZI POROJO AMBAZO WALA HAZIWAOGOPESHI SISIEMU MAANA WAMEZISIKIA KILA SIKU.
 
neno NCCR Mageuzi halina maana tena. Credibility na intergrity imekwisha baada ya kuwa mbele kuuwa upinzani. Itanichukua muda mrefu sana kuelezwa kuwa NCCR sio agent wa CCM. Kitamko gani hicho mmetoa cha kitoto.

Ni dharau gani hizo, yaani kiswahili hicho cha kuzungushazungsha tu ndicho mnasumbua nacho watu, kwa taarifa yenu nimesoma paragraph ya kwanza tu, nikaona mnarudia maneno nikaacha.
Hopeless,

Mmebakia mkilinda jina muda mrefu sana lakini sasa hata kwa sentensi halilindiki. Yaani kweli ccm imezunguka ikimba mwenge mwenge na nnyi wimbo ni uleule wa mafisadi, kwa hiyo na nyie vijana wenu wakienda na mwenge ndo maslahi ya taifa hayo. Unajua budget ya mwenge ni zahanati ngapi? unajua kwenye mwenge ni watu wangapi wanaambukizwa ukimwi? acheni ccm waambukize wenyewe na mwenge wao. Mimi sio mwana siasa lakini mnapaswa kuchapwa viboko kabisa. Hopeless, An empty vessel makes the most noise.

Aiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu NCCR...! Labda mtuombe radhi isisi wananchi, radhi kabisa kwamba juzi mlipopromote kutengana mlipotoka. Vinginevyo, Kwaherini. mazishi yenu tumeyasikia na tunasubiri matanga na arubaini. kwa taarifa yenu mimi wala sio chadema wala ccm. Sipo wala Tz useme ninafaidika na Tshirt za ccm.
Hopeless. Moderator ondoa hicho kitangazo cha NCCR humu weka kule kwenye udaku.
 
Ahsante sana kwa matusi tanayodhihirisha wewe sio hopeless
 
Back
Top Bottom