NCCR Mageuzi yaambulia Patupu Babati

kesi ya kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo la babati vijijini ,dhidi ya mbunge wake mwenye asili ya kisia ,Jitu son mahakama imetoa hukumu ya kubariki ubunge na kumpiga chini mlalamikaji kutoka chama cha NCCR mageuzi
 
Nakuunga mkono ndugu; KWa mtazamo wangu ni kwamba sasa hivi Serikali kutokana na UMKAPA uliopo tusitegemee kama kuna kesi yoyotwe ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iwe wa Uraisi, Ubunge au Udiwani itakayopewa hukumu ya Mlalamikaji kuwa ameshinda kesi kiasi ya kwamba italazimu Uchaguzi urudiwe. Kesi zote iwe zimefunguliwa na CDM, CCM, NCCR, UDP nk. hakuna hukumu itakayotoka tofauti na hii ya BABATI, ILEMELA. Kwani kurudia uchaguzi ni gharama sana hivyo serikali itabidi itumie pesa nyingi sana. Mfano amgalia sakata la Mbunge Kafulila wa NCCR au Mbunge wa CUF ambao vyama vyao vimewavua Uanachama ambapo kisheria inakuwa wamevuliwa ubunge. Lakini tumeshuhudia hata Bunge lilitoa mpya kwa kumteua Kafulila kuwa mwakilishi wake katika Msiba wa RIP Regia Mtema, hii ni kuonyesha kuwa bado Bunge linawatambua, na hawako tayari kufanyike uchaguzi tena. Hivyo ni matokeo ambayo tuliyatarajia na pia tunayatarajia kwa kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi mbalimbali. MIZAMBWA NABII MTARAJIWA!!!

Unachokisema hakina maana yoyote kama mtu ana akili timamu na anatumia mantiki (logic) katika hoja zake.

1. Mazingira ya kesi zilizofunguliwa si sawa, hivyo siyo mantiki kusema mbona siyo madai ya wapinzani kutupiliwa mbali katika kesi husika. Kwa mfano kwa kesi ya uchaguzi huko Babati Magharibi, wakati wa kutangaza matokeo msimamizi ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya alikuwa akitangaza matokeo tofauti na yale yaliyo katika fomu za matokeo. Mgombea wa NCCR - Mageuzi alipolalamika wakati ule aliambiwa aende mahakamani. Leo tunasema ni gharama kurudia uchaguzi?

2. Kitu cha ajabu ni kuwa katika mwenendo wa kesi hiyo tajwa hapo juu mlalamikaji ( Laurent Tara) alikuwa na nakala za fomu za matokeo katika vituo vyote ambavyo ndivyo vinavyoonyesha kuwa yeye ni mshindi. katika kesi hiyo alitaka atanngazwe kuwa mbunge wa Babati magharibi.

3. Katika utetezi kwenye kesi hiyo, aliyekuwa msimamizi, alijitetea alitangaza matokeo halali na akiwa na fomu za zenye matokeo yaliyompa ushindi Jitu son (mgombea wa CCM). Tofauti kati ya fomu za mlalamikaji na msimamizi ni kuwa, fomu za msimamizi ni nakala halisi (orginal) lakini hazina sahihi za wakala bali zimesainiwa na wasimamizi wa vituo tu. Nakala za fomu za mlalamikaji zilikuwa na sahihi za wasimamizi na mawakala.

4. Katika mwendelezo wa kesi hasa katika utoaji wa ushahidi baadhi ya mashahidi walikataa sahihi zilizo katika fomu original za msimamizi mkuu(Mkurugenzi) kwamba siyo zao.

5. Wakati wa majumuisho upande wa utetezi ulipeleka hoja kuwa nakala za fomu za matokeo toka mlalamikaji siyo nakala halisi hivyo haziwezi kutumika kwani zilipaswa kuidhinishwa (certified) na mwenye nakala halisi, ambaye atakuwa ni Tume ikiwakilishwa na Msimamizi mkuu ( Mkurugenzi). je? mkurugenzi angefanya kazi hiyo wakati yeye ni mmoja wa washtakiwa katika kesi kama hiyo?

6. Kuhusiana na suala la sahihi za wasimamizi wa vituo kughushiwa, wasimamizi hao walitakiwa kusaini katika karatasi ili kulinganisha sahihi hizo na zile zilizo katika nakala za mkurugenzi na zile zilizo katika nakala za mlalamikaji. Ikasemekana kuwa mashine za kusoma sahihi hazisomi sahihi katika nakala zisizo halisi. Hata hivyo, ilionesha kuwa sahihi zilizo katika fomu ya mkurugenzi ni tofauti na sample zilizochukuliwa.

Humumu ya kesi:
- Nakala halisi za mkurugenzi ndizo zinazotambulika na siyo za mlalamikaji.
- fomu za matokeo si lazima kusainiwa na mawakala. -
- Kuhusu sahihi za kughushi alieleza kuwa watu wanaweza kuwa na sahihi zaidi ya moja.
- Imetangazwa kuwa rufaa iko wazi.

My take:
1. Mgombea anaweza kupata wapi nakala halisi wakati nakala halisi zinarudishwa kwa msimamizi mkuu ( Mkurugenzi)

2. Kama hakuna ulazima wa mawakala kusaini fomu kuna umuhimu gani wa mawakala? Tunajua kuwa wakala akiwa na malalamiko na kwamba anapaswa kujaza fomu ya malalamiko ili nafasi yake ya sahihi katika fomu ya matokeo inapokuwa wazi basi sababu inakuwa katika fomu ya malalamiko jambo ambalo halikuwepo katika kesi ya Babati.

3. Kama mtu anaweza kuwa na sahihi zaidi ya moja kwanini kama suala ni kuthibitisha sahihi yake katika fomu ya tume asilazimishwe atumie ili aliyoitumia wakati wa ujazaji fomu. Kama ni suala la mtu kuchagua kutumia sahihi yoyote, basi benki wasingekuwa na haja ya kuhakiki sahihi katika ujazaji wa fomu zao.

Kwa ujumla sielewi aina ya hukumu inayotolewa mahakamani kwa mtindo wa aina hiyo. Hata humu jamvini tunaona wachangiaji nao hutoa aina ya hukumu bila kusikiliza malalamiko ya watu. Tukizingatia jinsi CCM inavyosaidiwa na dola katika upumbavu kama huo. Kama alivyoropoka huko Arumeru katika moja kuwa watu waimchague mbunge wa CCM kwa sababu mfumo wa uongozi wa nchi toka juu ni wa CCM - MaRC, MaDC, bila kutaja polisi na mahakama lakini najua hilo lipo wazi. Inatia aibu kiongozi wa serikali anapofika mahali na kuagiz katika vikao vya ndani vya CCM kuwa mgombea wa CCM atangazwe kwa namna yoyote na kwamba asiyeridhika aende mahakamani. Mahakama ipi?
 
Habari zilizotufikia sasa hivi ni kwamba Jaji Fatuma Massengi amekataa ombi la NCCR Mageuzi kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM Virajilal Jitu Son. Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa katika kesi za uchaguzi zilizofunguliwa na kusikilizwa hadi mwisho. Habari zaidi zitawajia hivi punde!
Zimeshatolewa nyingi tu.....Kilwa. Mtwara, Mwanza.......
 
Nakubaliana na wewe Gurtu kuwa kuna maswali mengi kuliko majibu kutoka katika hukumu hiyo! Hata hivyo, ni vyema Mawakili wanaowawakilisha walalamikaji wa jinsi hii wakawa na Plan B. Isingekuwa rahisi kupata nakala halisi au hata certified copy ya matokeo hayo. Walichotakiwa kufanya, pamoja na mambo mengine ni kuomba kura zihesabiwe upya au kura zifanyiwe scrutiny! Hata ukiangalia jinsi wataalam wa maandishi walivyofanya haraka kurejesha majibu, basi unaweza kuona kuwa labda njia rahisi ingekuwa ni kuomba masanduku ya kura yafunguliwe, iletwe orodha ya wapiga kura ili kuona mshindi ni nani. Naamini kuwa zoezi hili lingechukua siku mbili tatu, na hata ikiwezekana wataalam wa maandishi wakachukua sample kumi au ishirini na kuona kama kweli hakuna kura za bandia katika masanduku hayo. Bahati mbaya, mawakili na hata Majaji wanakuwa na haraka ya kumaliza kesi na kutoa hukumu bila kujali haki ya walalamikaji au walalamikiwa. Sidhani kama rufaa katika kesi hii italeta manufaa yoyote kama katika malalamiko Mlalamikaji hakuona umuhimu wa kuomba matokeo yabatilishwe kwa kuhesabu upya kura.
 
Kuna mambo mengi ambayo kama huna akili ya ziada huwezi kuyatambua na ukiyatambua huwezi kuyakubali. Moja ambalo sitakubaliana nayo na suala la kuhesabu upya kura. Kura zikishamalizika kuhesabiwa kwenye kituo huo ndio mwisho wa mambo yote. Hivi unategemea kuwa kuna ulazima wa kuhesabu kura baada ya kusafirishwa kutoka kituoni hadi ofisi ya Msimamizi Mkuu wakati Msimamizi Mkuu na vyombo vya dola ndio wanaoshakiwa kuwa wezi? Hao si ndio wanaoandaa vituo hewa?

Ukirejesha kumbukumbu nyuma, mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu maeneo ambayo wapinzani walishinda kura zilitangazwa baada ya jitihadi za wananchi kukesha wakisubiri matokeo wakiwa katika idadi kubwa. katika mazingira hayo ndipo kura zilitangazwa kwa kuhofia kufanya hujuma kwani hilo linaweza kusababisaha hasara kubwa zaidi.

Mimi sitabiri vibaya lakini ukweli ni kuwa Watanzania watachoka na uwezekano huo siyo ndoto. Silikilizia huko Arumeru kama kutakuwa na jaribu la kufanya hujuma majibu yatatolewa haraka sana.
 
Kwa uzoefu nilionao katika masuala ya uchaguzi, siyo Wasimamizi wote wanakuwa na vitabu vya bandia....wanachoweza kufanya ni kutumia vitabu vile vile walivyonanvyo kupiga kura za ziada...lakini kwa taarifa yako Wasimamizi huwa hawana muda wa kuhangaika na kura ndani ya masanduku, wao hucheza na zile fomu za kujaza matokeo. Kwahiyo ukiomba recount, kuna possibility kubwa kuwa matokeo yakabadilika. Kwa mfano katika kesi hii ya Babati, mlalamikaji alikuwa analilia matokeo ya vituo kumi tu, angeomba kura za vituo hivyo zihesabiwe hasa baada ya kuona kuwa taarifa ya mtaalamu wa maandishi imeenda kinyume na matarajiio yake na pia inapingana na maelezo ya msimamizi wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom