Naweza kujenga kwa mshahara wa laki tatu?

Mtoa mada unaweza kujenga na kufikia malengo Yako Kwa huo mshahara Kwa kuzingatia yafuatayo.
A. Kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
Mfano kuchangia harusi , ugeni , and related affairs
B. Kukuza hicho kupata chako.
Mfano fungua saluni Ili ikuwezeshe kupata matumizi ya nyumbani then mshahara usiguse baada ya miezi kazaa Ili ununue kiwanja.
C. Material za ujenzi .
Tofali fyatua mwenyewe tafuta local fundi wakutolee tofali nzuri za nchi tano au sita kwa gharama ya kawaida majukumu Yako ni kununua cement na mchanga kidodo kidogo .
Kamwe usinunue tofali utatumia gharama kubwa mwisho wa siku utachukia ujenzi.
D. Sitisha starehe na aina zake.
Kwa kipindi hiki cha ujenzi piga marufiku anasa zote utafanikiwa
Mwisho. Huo mshahara ni mkubwa sana unaweza kubalance na kufikia malengo Yako mfano kama mtu anauza mboga za amajani na amejenga sembuse wewe mwenye laki tatu.
Komaa utafanikiwa usikate tamaa achana na waliyoshdwa maisha wanao kukatisha tamaa na mambo ya familia wewe pambana.
 
Inawezekana kama kazi unayofanya ina michongo ya hela pemben na mshahara, maan hiyo ni kipato cha 10k kwa siku, ukila kwenye migahawa hutoboi inabidi ununue akiba ya chakula upike wenyewe, uishi karibu na unapofanyia kazi ili uepuke kulipa nauli, kama siyo mtu wa starehe kuna kitu cha maana utaweza kufanya kwa mshahara huohuo
 
Kama duniani tunapita, kwanini ujenge njiani...
Kujenga ni kama kufanya booking ya siti kwa basi la mkoani. Yani wakati tunasafiri uwe na siti yako umetulia, mtashuka kuchimba dawa utarudi kwenye siti yako, dereva anaweza fukia shimo( umepitia changamoto nyingine za kimaisha) upo kwenye siti yako.
Ndo maana ukifika mwisho wa safari, ushuki hata na uchafu ambao ulikuwa unatumia safarini unaachia kwa Dustybin..
 
Exactly
 
Back
Top Bottom