Nawaomba msaada wa maana halisi ya upotoshaji

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Imezoeleka na kukomaa kwa kila kitu au malalamiko ya wananchi wanapo lalamika kuhusu utendaji wa viongozi au ukosefu wa kitu fulani muhimu kwa jamii, basi kauli rahisi kutoka Serikalini huwa msiwasikilize hao ni wapotoshaji.

Je, Tanzania ikitokea mtu analalamika huduma ya Maji haipatikani au barabara mbovu ni upotoshaji? Mfano mzuri ni katiba inayopendekeznwa, Rais alisema ichapishwe ili tuisome lakini mpakaleo haiko mtaani, Wanaharakati mbalimbali wanajaribu kutuelimisha kuhusu katiba hiyo maana mtaani haipo, matokeo yake tunaambiwa tusiwasikilize ni wapotoshaji, Naomba msaada wenu
.
 
Upotoshaji, ni kitendo cha kuongoza/kupelekea katika mwelekeo/ namna isiyo sawa juu ya jambo, kitu mtu, kikundi cha watu au jamii.
pia upotoshaji huo unaweza kuwa katika mambo mengi kama siasa, uchumi, dini kijamii. ili hali tu kupekea katika mwelekeo au namna isiyo sahihi na yenye matokeo hasi.
 
Back
Top Bottom