Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 687
- 1,360
Kuendesha serikali ni sawa na kuendesha duka, mapato yatokanayo na makusanyo ya kodi mbalimbali na miradi ya nchi ndiyo mtaji kama ilivyo kwa mwenye duka.
Bidhaa za serikali ni huduma kwa wananchi ili waweze kulipa kodi na kuwekeza katika miradi mbalimbali kwa faida kama ilivyo kwa mwenye duka anavyoweka bidhaa ili apate faida.
Faida inayopatikana huwa inawekezwa zaidi au kutumika katika mahitaji mbalimbali bila kuathiri mtaji.
Inapotokea mwenye duka au watu aliowaajiri wakatumia vibaya mtaji duka huwa linafirisika, hivyo hivyo kwa serikali pia.
Unakuta serikali imetenga bajeti kadhaa kwenye umeme kama mtaji ili mapato yapatikane inapouza kwa faida halafu unatokea ubadhilifu wa bajeti hiyo serikali lazima ifirisike matokeo yake kamtaji kadogo kanashindwa kuwahudumia watz wote.
Nataka kuwakumbusha watumishi wa serikali kuwa mnapoajiriwa serikalini ni sawa umepewa kibarua na mwenye duka ukila mtaji duka linafirisika na kushindwa kutoa huduma.