Naungana na Zanzibar kuzuia Wamasai kutembea na SIME na RUNGU

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,248
4,087
Kwa maeneo ya mjini, haifai watu kutembea na SIME na Rungu, wakati mwîgine hawa wamasai wanakuwaga na mental issues , sasa vikimcharuka anarusha sime au rungu wakati wowote na kwa yeyote aliye mbele yake.

Kwa maeneo ya mjini, nashauri hata Serikali ya bara izuie hawa watu kutembea na hizi zana ambazo zinaweza KUUA.

Kuna siku kama sikusea mwaka 2009 , magari ya Mwenge Posta siti za nyuma kulikuwa na Mama mjamzito na Mmasai na baadhi ya watu, out of the blue yule mmasai alianza kujipiga kichwani, tukashangaa anachomoa sime, alimtandika yule mama na Sime ya Bega, jamaa wa pembeni kuona hivo na kwa kujihami ikabidi amrukie mmasai, na watu wengine wakaanza kumpiga mmasai, ikabidi gari iende kituo cha polisi.

Baadae ikajulikana mmasai alikuwa na ishu ya akili na ni mental challenged na hata kwenye mkoba wake alikutwa na dawa za Carbamezapine.

Tunaheshimu tamaduni za watu, hili liendewe kwa hekima, kwa maeneo ya mjini ikatazwe, kwa maeneo ya vijijini na porini sehemu za uwindaji waendelee na tamaduni zao.

Tusisubiri mpaka siku matatizo yatokee.

Ninaamini hata hao wapemba kutaka kuwachukulia Sime zao, kuna story behind na kuna tukio behind la kiusalama.

Shida watanzania kwetu kila kitu ni mzaha mzaha
 
Wamasai sio wakorofi miaka yote wanatembeaga na silaha zao za jadi bila tatizo. Hii laana ya kuwafukuza kwenye ardhi yao inawatafuna na mkome kabisa.

Mmasaai kuvaa lubega na kuchukua sime na rungu ndiyo utamaduni wao.
 
Yes , huwa hawana shida lakini nimeeleza wengine wanakuwa ni wagonjwa wa akili wanazunguka mitaani na sime.

Ukiwa umetulia zako mtu akikupiga Sime ya kichwa….. una asilimia kubwa za kufa

Panga na rungu ni silaha hatari, sidhani kama ni salama kuzurura nazo mjini haijalishi anatumia au lah, but ni potential risk
Think
 
Hivi kuna watu wanaongoza magonjwa ya akili kama polisi? Wanaenda kuua watu bar? Embu tuletee kesi ya Masai aliyeua kwa sime au panga mjini ?
 
Umejua hiyo ya polisi kwa sababu ni polisi
Nimejuaje nini tafuta nyuzi humu polisi wameenda kuua watu bar na silaha, leta kesi ambayo umesikia Masai kampga mtu na sime, hapo kuna ubaguzi unaendelea na wanatafutiwa sababu tu, miaka na miaka sijawah kusikia masai kapiga mtu mjini na panga au sime, tangu nipo mdogo mpaka napata ndevu.
Tuwekee wewe hio kesi tuione
 
Askari ni special case , kwenye Silaha kabla ya kupewa unakuwa unafanyiwq assessment ya mental strength and capability
Hakuna assessment ya mental strength kwenye majeshi yetu ,kipimo ni ukimwi ,miguu ,macho ,uvungu, marinda, makovu na homa ya ini ambapo ilianza intake ya 39 mwaka 2019 sasa hiyo mental strength wanapima wapi?
 
Askari ni special case , kwenye Silaha kabla ya kupewa unakuwa unafanyiwq assessment ya mental strength and capability
Askari mara ngapi tu kwa kufumaniwa wenzi wao wametoa uhai wa watu na WA kwao pia kwa hizo hizo silaha, sijaona kama hili tatizo la Masai limefikia hatua za mjadala labda kama Kuna kitu nyuma ya pazia
 
Kwa maeneo ya mjini, haifai watu kutembea na SIME na Rungu, wakati mwîgine hawa wamasai wanakuwaga na mental issues , sasa vikimcharuka anarusha sime au rungu wakati wowote na kwa yeyote aliye mbele yake.
Mbona hata polisi wetu ni hivyohivyo, kumbuka raia wangapi wamepigwa risasi mitaani huko bila hatia, baki ya wao kwa wao kuuana wakiwa kwenye lindo, mental issues zipo kwa watu wote, waacheni wamasai wadumise mila, ipo siku mtaawaambie waache kuvaa lubega
 
Yes , huwa hawana shida lakini nimeeleza wengine wanakuwa ni wagonjwa wa akili wanazunguka mitaani na sime.

Ukiwa umetulia zako mtu akikupiga Sime ya kichwa….. una asilimia kubwa za kufa

Panga na rungu ni silaha hatari, sidhani kama ni salama kuzurura nazo mjini haijalishi anatumia au lah, but ni potential risk
Think
Ni lini ulipigwa sime na mmasai?
 
Back
Top Bottom