Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,081
Ilikuwa 2005 hai 2007 wakati kaka akiwa na miaka 16 hadi 18, alikuwa anamfanya mama alie sana na mimi nilikuwa najisikia vibaya sana kumuona mama analia machozi na kupiga ukunga wa maumivu, very painfull!
Kaka alihamishwa shule kibao kwa utoro, uhuni, n.k. Alijiunga na makundi mabovu ya wavuta bangi, wanywa pombe enzi hizo vizroba ndio vilikuwa vinatrend sana, tunashukuru hakuingia kwenye madawa tu maana tulikuwa mkoani.
Nyumbani anatoroka usiku kwenda disko. Kaka alianza kuuza vitu vya pale nyumbani kama glasi, deki, baiskeli, n.k. Mzee kashatoa dozi nzito hadi jirani alikuja kumstop, mzee alitoa kipigo kizito cha takribani nusu saa yani hakuna mapumziko, alikuwa anampiga kwa mkanda wa ngozi na kuna muda anamtandika kule mwisho wa mkanda kwenye kachuma, mzee aliwahi hadi kumtishia kuwaita mapolisi lakini bro alikuwa kapinda si mchezo.
Asubuhi ikifika tunaenda kumcheki chumbani kwake hayupo basi mama analia sana na mimi naumia, mchana unakuta tu mama katulia machozi yanamlenga.
Mama alishampeleka kwa wachungaji na hata akapelekwa kusomewa visomo lakini wapi, walidhani ni pepo ila kiukweli ilikuwa ni stage ya ukuaji.
kaka alikuwa msumbufu sana ila kama utani vile licha ya kurudia form 4 mara 2 baada ya hapo hakuwa msumbufu aliweza kusoma hadi masters huko nje na leo hii hapa navyoongea ana cheo chake kizuri tu na biashara zake zinaendelea vizuri, ana tabia nzuri kabisa mfano wa kuigwa.
Kila nikikumbuka stress alizompa mama huwa nasikitika sana nikikumbuka mama alivyokuwa analia.
Je, kuna mwengine hii hali iliwahi kutokea kwao?