Nataraji Kuoa nipe somo la ndoa

Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
180
wadau nataraji kuoa hivi karibuni naomba mnipe do and donts za ndoa
 
Fanya yote uliyokua unamfanyia wakati mkiwa wapenzi/wachumba mpaka akakubali kua mke wako!!

1.Mheshimu mwenzako.
Heshima ni kitu kidogo sana kutoa ila kikubwa kwa anaepokea.Kua muangalifu unavyomwongelesha na kumfanyia mwenzako pindi muwapo na watu wengine.

2.Kua muelewa na mvumilivu.
K.m kama mlikua mmepanga ama kuahidiana kitu fulani alafu hakijafanyika usianze kwa lawama...ohh hunipendi..mara hunijali!Omba sababu na ukipewa elewa.Kama hakikufanyika leo kitafanyika kesho....dunia haikimbii!!

3.Msome mwenzako.
Ukijua tabia za mtu ni rahisi sana kumuelewa na kukidhi mahitaji yake.K.m ukijua mwenzi wako anahitaji nini pindi anapokasirika...nafasi ya kutuliza hasira ama kubembelezwa papo hapo itasaidia kutokuongezeana hasira kwa kumfanyia kile ambacho sicho anachohitaji.

4.Kua mwepesi wa kuomba samahani.
Usipende kujikweza...kujishusha kidogo kwenye mahusiano haimaanishi wewe ni duni.

5.Kua msikilizaji zaidi ya muongeaji.
Kuna wakati mwenzi wako anakua anahitaji kutoa yaliyomo moyoni mwake tu....iwe ni hasira ama furaha bila kuingiliwa na ushabiki ama upinzani kwahiyo soma alama za nyakati.

6.Onyesha kujali.
Wakati mzuri kumwonyesha mwenzako unamjali ni pale anapokua na wakati mgumu...iwe ni kifedha..kiafya...kikazi na mengineyo.Sio lazima umpe pesa kama ndicho anachohitaji...ama kumpiga mtu ngumi kama ni swala la ugomvi....maneno mazuri ya faraja...kumuonyesha uko mapoja nae na kwamba unaumia anapoumia yeye inatosha kabisa kumpa mwenzako ahueni.

7.Kua msiri.
Jiheshimu wewe pamoja na mwenzi wako.Matatizo yenu ya ndani sio yakuanika nje kila anaepita aone.Inapotokea mmekosana sio mwenzako akitoka tu kwa hasira na wewe unachukua simu ama mguu huyo mpaka kwa shoga na shangazi wote wajue leo kwako kuna kauogomvi.Na sio hata mambo madogo tu utake msuluishwe na mtu wa nje...malizeni humo humo ndani kwenu.

8.Wivu.
Wivu ni mzuri katika kupendezesha mahusiano ila ni zaidi ya kero pale unapozidi.Kua na kiasi....

9.Mpe nafasi yake.
Kua pamoja ndani ya mahusiano haina maana mfuatane pamoja kila upande wa jiji...kumbuka yeye ana marafiki zake na wewe una wako na sio kila unachofanya lazima na yeye afanye!

10.Imani.
Iwapo mtu hajakupa sababu ya kutokumuamini..muamini.Inakera sana pale mtu anapoonyesha wasiwasi na wewe iwapo hujafanya chochote kusababisha hilo.Pia jiamini wewe mwenyewe kama wewe...unapendwa wewe...unathaminiwa wewe...sio hata salamu tu ikitolewa kwa mwingine unaanza kuwaka.

11.Kua mkarimu.
Kua mkarimu kwa ndugu na marafiki wa mwenzi wako.Sio lazima mdogo wake umlipie ada wewe...ama umpelekee mama yake gunia la mchele, kitendo cha wewe kumsukuma kufanya hivyo iwapo atakua anajiuliza afanye au la inatosha kuonyesha upo upande gani.

12.Usiwe na kiburi.
Kiburi hakijawahi kujenga popote.Kununa kwa muda mfupi kunaeleweka na kunakubalika iwapo umekorofishwa.Ila kususa chakula....kuhamishana chumbani na kunyimana unyumba havijengi bali vinabomoa.Ndo mwanzo wkutafutiwa msaidizi.

13.Mwisho kabisa usisahau KUSHUKURU na KUTOA SIFA kila mara.
Kumsifia na kumshukuru mwenzi wako kila mara itamfanya ajihisi anapendwa na itamfanya afurahie kua karibu na wewe tofauti na mtu ambae anatoa malalamiko tu.

Kwa zaidi chungulia hapa https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/101189-dondoo-za-mapenzi.html#post1464830
 
Asante Lizzy... Brucker imebaki tu kusoma, kukalili kisha kuelewa...
 
jifunze kuwa "wanaume wote duniani akiwamo baba yako mzazi ANATAKIWA KUWA NA NYUMBA NDOGO"...Na kwa taarifa yako hata "mamako mzazi anaishi kwa hisia kuwa babako ana-nyumba ndogo" ILA AKILI KICHWANI MWAKO MAANA UKIKAMATWA READY/RED-HANDED ndoa ndio inakuwa ndoana na mnaishia kutalikiana na kuachana...ahahahaa ndoa tamu sana dogo wahiiiii sie wenzio tunafaidi sanaa
 
ila dogooo... unaweza ukachanganyikiwa na ushauri mbalimbali wa kuishi na mkeo...ndoa hazitazamiwi kama mitihani ya sikuhizi...SIMPLE SOLUTION " ISHI KAMA DINGI YAKO ANAVYOISHI NA MAZA WAKO"...au wee unasemaje?
 
Cha kwanza na cha muhimu kabisa UPENDO. make sure unampenda mkeo kwa dhati na kwa moyo wako wote. Kisha hayo aliyosema Lizzy yafuatie.
 
swali langu kabla ya kukupa NONDOZ

UMEAMUA AU UMEAMULIWA KUOA;
JE UKO TAYARI NA MAJUKUMU KAMA MUME WA NDOA NA SI UUME WA NDOA
WAZAZI WAKO WAMEKUBALIANA NA HII NDOA??
MUNGU AKIKUPA MTOTO UKO TAYARI KUMLEA AMA KULELEWA??

NIMEULIZA KWA MANTIKI IFUATAYO
1. YAWEZEKANA KUTOKANA NA UMRI AMA KWENU AKUNA ALIE OA UKAONA UKAMATE MZGO USAFISHE NYOTA ..SINA MAANA MBAYA ILA YANAKUSAIDIA UKIJIBU HILI


2..UKO TAYARI NA MAJUKUMU KAMA MUME?
NASEMA HIVI NIKIMAANISHA NDOA NYINGI WANAFIKIRI HARUSI AMA NDOA NIKUVALISHANA MASHELA NA PETE NA LINAPOFIKA MAJUKUMU YA NDANI WANAUME WENGI HUKIMBIA NYUMBA ZAO NA MAJUKUMU MWISHO WAKE HUANZA KUTUNZIWA WAKE ZAO NA UPANDE WA MKE MUULIZE HILI MAANA WENGI WAKIOLEWA AWAJUI MAJUKUMU YAO WANAHISI NDOA NA KUVUA NGUO NA KUBAKI NA KHANGA MUDA WOTE LA HASHA..MATOKEO MUME ANARUDI JION ANAKUTA UMEPIKA UGALI SAA 12 WAAKATI UNAJUA ANARUDI SAA TATU UKIFUNGUA YANATOKA MAJI KAMA MAFURIKO YA HAITI...HILI MMHH,, NA HILI KAMA NDUGU YANGU WA KARIBU SIPENDI LIKUFIKE NDIO MAANA NAULIZA KWA HERI

3.WAZAZI WAKO WAMEKUBALIANA NA NDOA YAKO
NAJUA WENGI WATAKUJA KUULIZA LAKINI UKWELI UNABAKI NDOA ISIYO NA BARAAKA ZA WAZAZI AIDUMU NA SITAKI URUDI HME BAADA YA MIEZI MITATU UNLESS UNATAKA KUINGIA KWENYE GUSSINESS BOOK

4.NIMEONA KWA MACHO YANGU MWANAUME AKIMWAMBIA MKEWE WA NDOA A SI HAWARA NAJUTA KUZAA NA WEWE
NDUGU KWA SIE WAKRISTO HII NI LAANA KWAKE ANAJUA YA KAWAIDA ILA MUNGU SI ATHUMAN MDOMO UNAJENGA UNATENDA..SASA BASI KUNA HILI LA KUZAA NA KUPELEKA WATOTO MOSHI KAMA WACHAGA WAKALELEWE NA BABU NA BIBI;;HILI NISINGEPENDA LIKUFIKE KAAMA NDUGU YANGU...WA KARIBU...., AKUNA LAANA KAMA YA KUTUNZIWA MTOTO NA MWISHO WAKE HUTUNZIWA MKEO MTARAJIWA NASEMA SIO KWAKO KAMA UTAIFATA HILI WATAKUFANYIA HIVYO

BAADA YA MAJIBU NTARUDI ZAIDI
 
Kama uamini uliza wachaga waliopeleka wake zao na watoto kulelewa na babu watoto wanaofata ni wa babu lakn kiheshima wanaitwa wajukuu lakn sio...anyway sihukumu wachaga la hasha nakujuza tu ndoa ilivyo..utaanza na sweet darling mwisho wake usipokuwa na mungu utaishia mahakamani..mbayyyyyyyyyyyyyyyyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kitu kikubwa kabisa ni kujua tu ndoa ni nini na kwanini unataka kuoa. Ukishajua hayo utafurahia hii life!
 
Thnax Lizzy na wadau wote, hakika kwa yote nitayafanyia kazi yale mema kadri mungu atakavyopendezwa na kuyawezesha kuyafanya, hakika ni somo kubwa sana mmenipa, thanx woooooooooooottteeeeeeeeeeeeee
 
Na wewe uwape wenzio sio unakaa nalo kama chemistry ok wenzio wafunde umepewa bure toa bure
 
Back
Top Bottom