Natamani kugombea ubunge jimbo la kalambo! Nipitie chama gani?

Kateka Sanza

Member
Jun 8, 2013
44
8
Wadau mi ni mkazi wa jimbo la kalambo na ni kijana umri wangu miaka 30. Nimemaliza shahada ya kwanza UDOM nilipata nafasi ya kuwa Wazir serikali ya wanafunzi. Sasa nawiwa kuingia kwenye siasa nikiomba kugombea ubunge jimbo la kalambo. Haja yangu kubwa ni kutaka kuwatetea wanyonge waliotelekezwa hadi wamekata tamaa sasa naona ndo muda muafaka kwangu kuwatumikia wananchi. Je nipitie chama gani? Naomba ushauri wadau.
 
chama chochote kilicho UKAWA but haujaeleza ni nani mbunge wa hapo ili wadau wanaomfahamu waweze kutoa cv yake hapa
 
Ahsante Mkuu. Mbunge wa jimbo lile kwa sasa anaitwa ndgu Josephat Kandege. Jamaa pia kaenda shule lakin ameshindwa kuwaletea wananchi maendeleo na ni mtu mbinafsi sana. Maoni yenu wadau maana ni mda wa vijana sasa.
 
Wenye tamaa ni CCM ........................ Nafikiri huko kutakufaa sana!! UKAWA wanatakiwa watu wenye nia siyo tamaa!!
 
Ahsante Mkuu. Mbunge wa jimbo lile kwa sasa anaitwa ndgu Josephat Kandege. Jamaa pia kaenda shule lakin ameshindwa kuwaletea wananchi maendeleo na ni mtu mbinafsi sana. Maoni yenu wadau maana ni mda wa vijana sasa.

Ujana siyo kigezo cha kugombea ubunge!!

Uzalendo na kuwa mpinga dhuluma na ufisadi ni moja ya vigezo vinavyotakiwa na wananchi!
 
Wadau mi ni mkazi wa jimbo la kalambo na ni kijana umri wangu miaka 30. Nimemaliza shahada ya kwanza UDOM nilipata nafasi ya kuwa Wazir serikali ya wanafunzi. Sasa nawiwa kuingia kwenye siasa nikiomba kugombea ubunge jimbo la kalambo. Haja yangu kubwa ni kutaka kuwatetea wanyonge waliotelekezwa hadi wamekata tamaa sasa naona ndo muda muafaka kwangu kuwatumikia wananchi. Je nipitie chama gani? Naomba ushauri wadau.

Ungeanza kutetea familia yako kwanza ikaondokana na huo umaskini halafu ndio ukaja kalambo...kwanza alie kuambia sisi wakaazi wa kalambo tuna shida mpaka tutafute mtu wakututatulia shida zetu? Ivi unajua kazi za mbunge?
 
haufai kugombea. Hujui hata chama kinacho faa kuleta maendeleo kwa wananchi? Inaonesha kwanza huna msimamo na kuamini kile unacho kiamini. By the way unataka kuwa mwanasiasa ilhali hujajua ni chama kipi kinafaa?

Umewah kuwa mwanachama hai wa chama chochote kweli? Napita tu kuwasabahi.
 
Kama wewe ni mkweli na usiependa wizi nenda CHADEMA au ukawa na kama wewe una tabia za uwongo na tamaa na mwizi nenda chama cha majambazi
 
haufai kugombea. Hujui hata chama kinacho faa kuleta maendeleo kwa wananchi? Inaonesha kwanza huna msimamo na kuamini kile unacho kiamini. By the way unataka kuwa mwanasiasa ilhali hujajua ni chama kipi kinafaa?

Umewah kuwa mwanachama hai wa chama chochote kweli? Napita tu kuwasabahi.
Eti naye kasoma UDOM!
 
Wadau mi ni mkazi wa jimbo la kalambo na ni kijana umri wangu miaka 30. Nimemaliza shahada ya kwanza UDOM nilipata nafasi ya kuwa Wazir serikali ya wanafunzi. Sasa nawiwa kuingia kwenye siasa nikiomba kugombea ubunge jimbo la kalambo. Haja yangu kubwa ni kutaka kuwatetea wanyonge waliotelekezwa hadi wamekata tamaa sasa naona ndo muda muafaka kwangu kuwatumikia wananchi. Je nipitie chama gani? Naomba ushauri wadau.
Wewe Unaonekana kama Mbabaishaji vile; Just wasting your time b'se you don't have any preparation for the intended goal.Kijana endelea kujipanga kwa miaka ijayo maana kama hadi sasa haujui ni Chama gani utapeperusha bendera; Nikushauri watu wenye Mashaka kama wewe wanagombea kupitia CCM, maana walioko upinzani wanajipambanua waziwazi.Nia yako ni ubunge na wala hauna kitu kinakutuma kukifanya kwa watanzania; Inaonekama hauchukii Rushwa na umasikini huu uliotamalaki.
 
... Kama Hujui Chama Gani Upitie, Basi Wewe Hujielewi. Kaa Pembeni. Kweli Wewe Ni Wa Udom, Sidhan Kama Kuna Wa Udsm Design Yako
 
Wadau mi ni mkazi wa jimbo la kalambo na ni kijana umri wangu miaka 30. Nimemaliza shahada ya kwanza UDOM nilipata nafasi ya kuwa Wazir serikali ya wanafunzi. Sasa nawiwa kuingia kwenye siasa nikiomba kugombea ubunge jimbo la kalambo. Haja yangu kubwa ni kutaka kuwatetea wanyonge waliotelekezwa hadi wamekata tamaa sasa naona ndo muda muafaka kwangu kuwatumikia wananchi. Je nipitie chama gani? Naomba ushauri wadau.
kama unashamba lima tu kwa sababu maelezo yako tu hufai hata kidogo kuwa mwanasiasa. Yaani unataka ushauriwe uanachama kijana mwenye miakat30? Back to your origin
 
Najua unafani nyingine kamanda mwenzangu itumie,kama hadi sasa hujajua upitie chama gani. Duh,utatoa kali ya mwaka wewe.
 
Pengine hata sera za vyama mbalimbali vya siasa hadi now hujui hata kimoja. Utagombea vipi?au unataka tukuchagulie chama ndo uingia darasani kusoma sera za chama husika? Huwezi siasa ndugu.
 
C d m for life others ni photocopy

Nashukuru sana wadau.Nimepata pa kuanzia kwanza mm ni mwanaharakati machachali tangu utoton kwan dhuluma kwangu ni sawa na ugonjwa hatari kwa jinsi nisivyo penda. Nimepata kuwa miongon mwa watu tegemez UDOM kupambana na dhuluma kwene bumu namshukuru Mungu nilifanikiwa mm cipo kama baadhi walivo comment ila niltaka kusoma mawazo ya wadau.Familia yangu nimeikomboa safari yangu ni kwa jamii yangu sasa. Matai sec ndo shule yangu kwa mapambano wananifahamu nikiwa kiongoz pale 2002-2002 mengi nimefanya.Lakin mm ni kamanda hai kadi yangu ya CDM iko hai. Shida yangu cio cheo bali uongoz uliotukuka wenye dhana ya utawala bora uliojamaa sauti ya kukemea maovu na yenye kupinga dhuluma kwa watanzania. Nakusudia kuleta uwazi ndani ya serikali utakao jali na kuwakumbatia wote wenye haki pasi kuwabagua kwa sura, rangi, kabila wala dini kwani ni tunu zilizokosekana kwa watanzania.Kwangu rushwa ni mlango wa nyuma sikufundishwa kuutumia kuingia ndani. Nilifundishwa kuhamasisha usawa na haki kati ya walionacho na wasio nacho.Namkumbuka sana mwl nyerere kwa kauli yake ya kutowaita baadhi ya watu waheshimiwa bali tuitane ndgu alikuwa na maana ya kutuweka tuwe sawa na kujiona tu wamoja na si kama ilivyo sasa. Wadau ninayo mengi ya kuwafanyia watanzania na si kukurupuka tu kwa sababu eti kila mtu anahaki ya kugombea bali ni kwa dhamira ya kwamba kwa nn watanzania tunaonewa,tunaibiwa,na kudharauliwa na watawala wetu? mfano eti ni vijisenti tu. Nn maana yake? sasa ni wakati wa mapambano kijana amka acha dharau na kejeli twende tukalipiganie taifa letu. Mm nimeanza wewe unasubir nn? Mwaga maoni yako hapa.
 
Back
Top Bottom