Nataka kujua tofauti ya crowd raising na deci

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Habari ndugu wanajamvi........

Hivi karibuni kumekua na aina ya shughuli ya kiuchumi ambayo inahusika na mtandao wa kuchangiana pesa uitwao Crowd raising.....ambapo mwanachama baada ya kujiunga anakuwa anapata malipo kadiri ya idadi ya wanachama wapya wataoingia kupitia ushawishi wake........

Sasa swali langu linakuja kwamba hivi haya mambo si ndiyo yalileta shida mnamo mwaka 2008 kama sio 2009 ambapo serikali ilipiga marufuku michezo kama hii ya watu kuchezeshana upatu na walikiri kuwa upatu ni kinyume na sheria..........na kama ni hivyo naomba kufahamu hiki kinachoendelea hapa katika hii kitu inayoitwa crowd raising ina tofauti gani na DECI na ipo kwa mujibu wa sheria za nchi .....au kama kawaida hawa viongozi wanafiki wasiomuogopa MUNGU wanaojifanya wapo juu ya sheria mashetani watu wamekaa kimya kumbe wanamgao wao.......?!
 
Ila unajua serikali sometimes ni wanafiki sana.....sasa walikaa kimya walivyoona DECI ina wadhuru maslahi yao wakaamua kuiwekea figisu..........hii nayo naitilia shaka inawezekana ni mtego tena wanawategea mchange ziwe nyingi halafu wanawapiga pini pesa hampati halafu mkitaka kudai wanawatishia kuwashitaki mahakamani kwa kushiriki upatu laanakhum wakubwa hawa.......na mwisho wa siku pesa za watu karibia bilioni saba za kitanzania walizikausha kimya.......pesa za masikini ambao waliweka ili wapate chochote wao wakazidhulumu..........viongozi hawa waliotangulia serikali yq kikwete wengi wao wanalaana manina zao na MUNGU yupo zile pesa mikosi yake itawaandama vizazi vyao miaka yote kama leo kizazi cha watu weupe kinavyolaumiwa na kizazi cha watu weusi juu ya umasikini ambao ni matokeo ya utumwa na ukoloni.......!
 
Tunahitaji huu mjadala wa DECI ufunguliwe upya........zile pesa zetu sisi raia tusiokuwa na hatia turejeshewe........maana kwa ninavyofahamu ni kweli kuwa kutokujua sheria haihesabiwi kama kinga mahakamani katika kushinda kesi lakini kama raia atashitakiwa kwa kutokujua sheria basi ni dhahiri hata hata serikali ishitakiwe kwa kutokuwafundisha raia sheria ambazo wanachukulia wamezivunja kwa makusudi............BRING OUR DECI MONEY BACK .
 
Crowd sourcing au raising ni harambee ya kuchangia pesa kupitia mtandao. Ni njia mojawapo ya kuraise capital.. Kwa wenzetu ni swala official na kuna website maarufu sana kwa kazi hiyo sema kibongo bongo kwa kuwa tushang'atwa na nyoka kama DECI, bas hata tukigusa na jani tu tunashtuka na kuogapa.
 
Habari ndugu wanajamvi........

Hivi karibuni kumekua na aina ya shughuli ya kiuchumi ambayo inahusika na mtandao wa kuchangiana pesa uitwao Crowd raising.....ambapo mwanachama baada ya kujiunga anakuwa anapata malipo kadiri ya idadi ya wanachama wapya wataoingia kupitia ushawishi wake........

Sasa swali langu linakuja kwamba hivi haya mambo si ndiyo yalileta shida mnamo mwaka 2008 kama sio 2009 ambapo serikali ilipiga marufuku michezo kama hii ya watu kuchezeshana upatu na walikiri kuwa upatu ni kinyume na sheria..........na kama ni hivyo naomba kufahamu hiki kinachoendelea hapa katika hii kitu inayoitwa crowd raising ina tofauti gani na DECI na ipo kwa mujibu wa sheria za nchi .....au kama kawaida hawa viongozi wanafiki wasiomuogopa MUNGU wanaojifanya wapo juu ya sheria mashetani watu wamekaa kimya kumbe wanamgao wao.......?!
Hii kitu nimeshawishiwa sana nijiunge nikaitilia shaka njia zake za kujiunga nikaona haiko sawa . watu waliomo humo hawajui hata inapotokea dhuluma watapata wapi msaada na hakuna uhakika wa mkataba baina ya wachangiaji iwapo unataka kujitoa kama unaweza kupata fao lako au asilimia fulani,kiujumla mambo yapo holela sana na wanajitahidi sana kutengeneza matangazo ya kuwapumbaza watu ili waingie tamaa ya KUJIUNGA.TAHADHARI kama unapesa na hujapata wazo la kufanya weka bank kwenye usalama haya mambo ya CROWD RISING ni usaniii
 
Tunahitaji huu mjadala wa DECI ufunguliwe upya........zile pesa zetu sisi raia tusiokuwa na hatia turejeshewe........maana kwa ninavyofahamu ni kweli kuwa kutokujua sheria haihesabiwi kama kinga mahakamani katika kushinda kesi lakini kama raia atashitakiwa kwa kutokujua sheria basi ni dhahiri hata hata serikali ishitakiwe kwa kutokuwafundisha raia sheria ambazo wanachukulia wamezivunja kwa makusudi............BRING OUR DECI MONEY BACK .
Serikali haiwezi kushitakiwa kwa kutokuwafundisha raia sheria isipokuwa inaweza kushitakiwa kwa kushindwa kulinda mali (pesa) za raia mpaka akatokea tapeli(DECI) na kupora watu na serikali isichukue hatua
 
Serikali haiwezi kuashitakiwa kwa kutokuwafundiaha raia sheria isipokuwa inaweza kushitakiwa kwa kushindwa kulinda mali (pesa) za raia mpaka akatokea tapeli(DECI) na kupora watu na serikali isichukue hatua
Sawa hata kama ni hivyo pia basi wafanye hivyo............watusaidie pesa zetu zirudishwe
 
Back
Top Bottom