Nataka kuishitaki serikali ya tanganyika na ya tanzania....!!!

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
407
133
wadau wa jf naomba mnisaidie hili jambo. Mimi nataka kuishitaki serikali ya Tanganyika kwa mambo iliyotuahidi lakini hadi leo miaka kama 50 hivi ya uhuru haijayatekeleza:-1. serikali ya Tanganyika ilitutoa katika makazi yetu ya asili (vijiji vya ujamaa wa kweli wa asili) nakutuahidi kuwa inatuweka katika vijiji vya ujamaa vya kukopi na kupesti vya uchina, ambapo iliaminika kuwa ingetuletea huduma zote za muhimu za jamii kama maji safi na salama ya bomba, umeme usio wa mgawo, shule kila kijiji, hospitali kila kijiji, bus moja kila kijiji, trekta moja kila kijiji,nk,nk,nk. Lakini hadi hivi ninapoandika hii thread hizo huduma zote hakuna hata moja hivo serikali ya TANGANYIKA ilitufanya sisi wakazi wa kijiji cha BUSEGA kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza kuwa ni MAZUZU. 2. Nayo serikali ya TANZANIA ilipoipokea ile ya tanganyika ikasema itaendeleza pale serikali ya tanganyika ilipoishia, ikiwa ni pamoja na:- Kujenga barabara za rami kila kijiji, kuweka taa za umeme katika kila barabara ya kijiji, kupunguza idadi ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito kila kijiji nk, nk, nk, nk. Lakini hadi leo hizo huduma hazijaweza kuendelezwa na hii serikali ya TANZANIA katika kijiji chetu cha BUSEGA kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza. Sasa kitu ambacho nina waomba wadau wa JF mnisaidie ni namna ya kuandaa na kutengeneza haya mashitaka kabla ya kuyapereka kotini kusikilizwa. Hilo tu mkiniwezesha mambo mengine nitayamaliza huko kotini mimi mwenyewe na wanakijiji wenzangu wa BUSEGA. Jamani nasubilia msaada wenu wa kuandaa mashitaka haya.


 
Nahisi mashitaka yako yatakuwa yenye sura ya "public litigation", kuna vigezo vya kufungua kesi yenye maslahi au mkondo wa umma, labda ili kupata mantiki ya madai yako dhidi ya serikali i wish upitie kesi hizi: Rev. C. Mtikila v. R (1993,1994,1995), Ndijumwa Shubi Ballonzi v. registered trust of ccm. n.k. Kuna wa2 wengi wanaopenda kufungua kesi dhidi ya serikali lkn taratibu za kufuata ni nyingi.
 
Nitafurahi ukifanikiwa. Nakupa nguvu utimize azma yako. Sheria ilinipita kushoto, hivo sinao msaada wa kisheria
 
watafute wanasheria watakusadia kuandaa hati ya madai na kukuwakilisheni mahakamani, ila wanaweza pia kukusaidieni kuandaa hati tu na mkajiwasilisha wenyewe huko mahakamani
 
Back
Top Bottom