Natafuta wateja wa Mafuta ya Alizeti

Bokina

Member
Feb 22, 2012
8
8
Ndugu wapendwa,

Ntafuta wateja wa mafuta ya Alizeti. Yeyote mwenye kujua soko zuri la mafuta haya naomba tuwasiliane.
 
Pakajimmy kasema ukweli. Wakati mwingine mtu anakuja na biashara hapa ila kwa jinsi anavyowasilisha inakuwa kama utani. Ni kwa nini kamamtu uko serious usitoe maelezo ya kueleweka na kumshawishi mtu ahitaji biashara yako? Kwa mfano unaweza kusema uko wap, mafuta yanapatikana katika ujazo gan, kwa bei gani, km utampelekea mtu au ni mtu afuate ulipo, nk. Then mtu anaweza kujifikiria na mafuta anayotumia saiv, bei ya sasa ukilinganisha na ya kwako na labda akaona kununua kwako kutakuwa na uafadhali!!!!
 
Nipo dar, nimepack kw lita tano tano na 20, bei itategemea na kiasi cha mzigo utakao chukua.
 
Nipo dar, nimepack kw lita tano tano na 20, bei itategemea na kiasi cha mzigo utakao chukua.

Mkuu kakukumbusha kujieleza ili ueleweke, bado unatoa maelezo ya jumla, sasa Dar kitongoji gani? Niko Dar, Tabata Liwiti. Lita tano ni sh kadhaa, na lita 20 ni sh kadhaa, ukinunua kuanzia lita kadhaa mpaka lita kadhaa punguzo ni hili au nyongeza ni hii. Kwa mawasiliano piga simu ya sasatel, mwenye kiwango kikubwa usafiri upo/haupo. nk nk
 
Una process mwenyewe au ni dalali? Ninavyojua mimi kama unaprocess hayo mafuta haya headache ya soko watu watakuja wenyewe hadi hapo kwako kuchukua,soko lake kwa kifupi ni kubwa sana,unayo kiasi gani? weka bei
 
Ukishatoa maelezo ya kina na contacts tutakutafuta.

1.Lita tano unauza kwa sh ngapi?
2.Hayo mafuta hayajachakachuliwa kweli? Unayatoa mkoa gani?

Mengine wadau washawaweka!
 
Nina process mwenyewe, kwa sasa nina litre 15,000. Kwa mtu ambae yupo serious please PM me ili tupeane mawasiliano na kuongea biashara kirefu
 
Ukishatoa maelezo ya kina na contacts tutakutafuta.

1.Lita tano unauza kwa sh ngapi?
2.Hayo mafuta hayajachakachuliwa kweli? Unayatoa mkoa gani?

Mengine wadau washawaweka!
Sasa hivi wanayachakachua sana kwa kuyatia polymers, na kuyakamua tena...sasa matokea watumiaji wanastukia wanakufa macho taratibu!
Be careful!
Muuzaji tafadhali usije ukawa ajenti wa upofu kwa wanunuzi!
 
Weka bei ya wastani, ili hata mtu akitaka kuja ajue aweke mfukoni bei ngapi!
Yaani huyu jamaa anashangaza kweli!
Anatangaza biashara halafu hatoi maelezo ya kutosha, hadi watu wanamtafunia halaf yeye anameza. Tena anajibu kimkato tu.
He can't be seious!
 
Huyu member aliyeangusha thread hii kwa ujumla ni dalali flu
Naweza kusema hivyo kwa sababu ya maelezo yake isiyojitosheleza.

Kazi kweli kweli!
 
Jamani mimi sio dalali,

Nina kiwanda changu kipo Dodoma
  • Lita 5 Tsh. 19,000
  • Lita 20 Tsh. 64,000
  • Ni afuta mazuri sana Label ni Dodoma Sunflower, Double purified, hayajachakachuliwa, ukitaka kujua alizeti iliyochakachuliwa weka kwenye friji, yale mengine yataganda alafu alizeti itabaki haijaganda.
Napatikana Mbezi Tank bovu kwa mawasiliano zaidi piga 0767821301
 
excellent

now you sound like an entrepreneur
 
Hahahaa, hatimaye umeipata ABC. Pakajimy safi sana.

Mkuu usiwe na hasira kwa member hapa maana watu kama Malila ni Wajasirimali wazuri sana. Badala ya kuomba watu waku-PM, basi wewe ndiyo ulitakiwa uwa-PM hao member ili wakupe hiyo ABC na bidhaa zako ziuzike kiurahisi.

Kama kiwanda kipo Dodoma, je watu wa Dodoma wanaweza kununua hapohapo Dodoma au hadi yaje Dar na mwisho yarudi tena Dodoma. Morogoro je? Tabora je?

Kama kiwanda kipo Dodoma, na hulipi nauli hadi Dar, bei yake inakuwaje?

Mkuu, jipange vizuri na uweke maelezo mengi ya kutosha kiasi kwamba mtu akitaka, basi anakutafuta.

Nakupa HONGERA kwa shule nzuri uliyoweka jinsi ya kujua mafuta yaliyoCHAKACHULIWA. Hayo ndiyo maelezo unayotakiwa kuyaweka mwisho wa tangazo lako kwa maneno kama:
"ONYO: Kuna mafuta yamechakachuliwa na hatari kwa afya yako, utayajua kwa jinsi hii....... Karibuni mumuendeleze Mtanzania mwenzenu."

Kila la kheri.
Jamani mimi sio dalali,

Nina kiwanda changu kipo Dodoma
  • Lita 5 Tsh. 19,000
  • Lita 20 Tsh. 64,000
  • Ni afuta mazuri sana Label ni Dodoma Sunflower, Double purified, hayajachakachuliwa, ukitaka kujua alizeti iliyochakachuliwa weka kwenye friji, yale mengine yataganda alafu alizeti itabaki haijaganda.
Napatikana Mbezi Tank bovu kwa mawasiliano zaidi piga 0767821301
 
Jamani mimi sio dalali,

Nina kiwanda changu kipo Dodoma
  • Lita 5 Tsh. 19,000
  • Lita 20 Tsh. 64,000
  • Ni afuta mazuri sana Label ni Dodoma Sunflower, Double purified, hayajachakachuliwa, ukitaka kujua alizeti iliyochakachuliwa weka kwenye friji, yale mengine yataganda alafu alizeti itabaki haijaganda.
Napatikana Mbezi Tank bovu kwa mawasiliano zaidi piga 0767821301

Mkuu, kwanza hongera kwa kuwa na ujasiri wa kuingia kwenye sekta binafsi na kujiajiri mwenyewe. Hata hivyo nina swali moja? Hiyo Trademark yako (Dodoma Sunflower) imekuwa registered? na Je bidhaa zako zina nembo ya TBS? Kama jibu ni HAPANA basi yafanyie kazi hayo, na kama jibu ni NDIYO basi endelea kusoma hapa; Soko la bidhaa hizo zipo popote pale, kwani mafuta ni bidhaa inayotumika kila kukicha na pia haya ya Alizeti ni CHOLESTEROL FREE.

Cha kufanya ni kutafuta wenye maduka ya Jumla au taasisi zinazohudumia watu wengi (kama vyuoni, shule). Vilevile ninaweza nikakuunganisha na hawa wadau kama Jibu la maswali ya hapo juu litakuwa ni NDIYO

Changamoto kubwa niionayo mimi kwa watu wengi wanaokamua alizeti ni hapo kwenye MARKET SEGMENTATION. Unapoamua kupack kwenye vifungashio vya 5ltrs & 20ltrs ni vyema, lakini unakuwa umejitenga na soko kubwa zaidi la wale wanaomudu 1ltr & 3ltrs, kwani watanzania tulio wengi ni kima cha chini. (chukua hii kama changamoto na uifanyie kazi pia).
 
Back
Top Bottom