Natafuta wateja wa Mafuta ya Alizeti

Kama kiwanda kipo Dodoma, je watu wa Dodoma wanaweza kununua hapohapo Dodoma au hadi yaje Dar na mwisho yarudi tena Dodoma. Morogoro je? Tabora je?

Kama kiwanda kipo Dodoma, na hulipi nauli hadi Dar, bei yake inakuwaje?


Kila la kheri.

Nasubiri jibu la swali hili
 
Mkuu, kwanza hongera kwa kuwa na ujasiri wa kuingia kwenye sekta binafsi na kujiajiri mwenyewe. Hata hivyo nina swali moja? Hiyo Trademark yako (Dodoma Sunflower) imekuwa registered? na Je bidhaa zako zina nembo ya TBS? Kama jibu ni HAPANA basi yafanyie kazi hayo, na kama jibu ni NDIYO basi endelea kusoma hapa; Soko la bidhaa hizo zipo popote pale, kwani mafuta ni bidhaa inayotumika kila kukicha na pia haya ya Alizeti ni CHOLESTEROL FREE.

Cha kufanya ni kutafuta wenye maduka ya Jumla au taasisi zinazohudumia watu wengi (kama vyuoni, shule). Vilevile ninaweza nikakuunganisha na hawa wadau kama Jibu la maswali ya hapo juu litakuwa ni NDIYO

Changamoto kubwa niionayo mimi kwa watu wengi wanaokamua alizeti ni hapo kwenye MARKET SEGMENTATION. Unapoamua kupack kwenye vifungashio vya 5ltrs & 20ltrs ni vyema, lakini unakuwa umejitenga na soko kubwa zaidi la wale wanaomudu 1ltr & 3ltrs, kwani watanzania tulio wengi ni kima cha chini. (chukua hii kama changamoto na uifanyie kazi pia).
Kweli nimekuamini wewe ni Entrepreneur ahsante kwa darasa, hapo umefundisha wengi walio na biashara za aina hiyo!!! Ubarikiwe uzidi kutoa darasa!!!!

 
Kwanini utafute wateja hapa? kwanini usi distribute kwenye maduka makubwa ya jumla?
Mkuu,mleta mada hajakosea. Kuleta suala hili huku, anajua hatapata wateja tu (wa kununua bidhaa) bali atakuwa na fursa ya kupokea changamoto mpya (kama issues za intellectually property protection) na kujua wateja wake wanataka nini?
 
mambo ya IPP, Market Research ni mazuri lakini, nadhani aliyetoa topic either hafahamu nini anataka au clearly from the topic description s/he is looking for something different, this is what he said, "Yeyote mwenye kujua soko zuri la mafuta haya naomba tuwasiliane"; hence my response "kwenye maduka makubwa";
 
Back
Top Bottom