Natafuta nyumba nzima ya kupanga dar

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Wana forum ninatafuta nyumba nzima yenye usalama mzuri maeneo ya sinza,mwenge,kinondoni,mikocheni,kijitonyama au kawe.Naoba mwenye taarifa anisaidie haraka.
 
mtafute bwana mmoja anaitwa Kitomai katika hii namba 0755312233
 
Wana forum ninatafuta nyumba nzima yenye usalama mzuri maeneo ya sinza,mwenge,kinondoni,mikocheni,kijitonyama au kawe.Naoba mwenye taarifa anisaidie haraka.
Kama uko vizuri, pitia kwenye maofisi ya madalali wametapakaa kote, ila pia ujue, fee ya dalali ni kodi ya mwezi mmoja, unalipa wewe, na mwenyenyumba pia anampa kodi ya mwezi mmoja, hivyo ili zipatikane fedha za dalali, anamshinikiza mwenye nyumba kupandisha kodi!.

Kama hauna haraka ki hivyo, tembelea maeneo unayoyataka, utaona vibao vya matangazo ya kupangishwa nyumba kwenye kona za mitaa, hapo unazungumza direct na wenye nyumba unajipatia unafuu wa kodi.

Ngarama za kupanga nyumba nzima ya kawaida, vyumba 4 vya kulala, kimoja ni master, sitting, dinning na jiko yenye geti na usalama ni kama ifuatavyo
Kinondoni kuanzia laki 3
Sinza Laki 4
Mbezi Beach laki 5
Masaki-milioni,
Osterbay- 1.5
 
Asante sana Pasco nimeileta jamvini ili kuepuka vurugu za mtaani madalali wengine sio waaminifu unaweza kujikuta unachapwa bei mbovu ngoja tucheck zaidi kuna mwana forum pia kanipa namba za simu.
 
kuna nyumba naifahamu ipo sinza,na mwenye nyumba namfahamu,jee upo interest?wapangaji wamehama j.2 hii,wamepata kazi arusha.sehemu nzuri mno,na ni ya vyumba 3,ina geti na sehemu ya kupaki gari kama 3,jee ya vyumba 3 itakufaa?lakini ndani ya hilo eneo kuna nyumba nyengine 2,ila wanaokaa humo ni wastaarabu mno,na ni watu ambao wapo busy na kazi,hawana watoto
 
Asante sana Kisukari check inbox yako nime ku PM huko tuongee vizuri.
 
kuna nyumba naifahamu ipo sinza,na mwenye nyumba namfahamu,jee upo interest?wapangaji wamehama j.2 hii,wamepata kazi arusha.sehemu nzuri mno,na ni ya vyumba 3,ina geti na sehemu ya kupaki gari kama 3,jee ya vyumba 3 itakufaa?lakini ndani ya hilo eneo kuna nyumba nyengine 2,ila wanaokaa humo ni wastaarabu mno,na ni watu ambao wapo busy na kazi,hawana watoto

Sisi wenye familia za watoto wanane tutaishi na watu kweli? lol
 
Kisukari hope umeamka salama check tena inbox yako
 
Wana forum ninatafuta nyumba nzima yenye usalama mzuri maeneo ya sinza,mwenge,kinondoni,mikocheni,kijitonyama au kawe.Naoba mwenye taarifa anisaidie haraka.

Kama utapapenda Kinyerezi ipo nyumba kubwa ina vyumba vyenye nafasi kubwa ya kuweka hata vitanda vitatu, living room kubwa ya kifahari, dining room, stoo, jiko kubwa n.k. karibu na barabara, usafiri wa kuaminika na kama una usafiri wako parking ipo. Kodi laki 8 kwa mwezi.
 
Kama uko vizuri, pitia kwenye maofisi ya madalali wametapakaa kote, ila pia ujue, fee ya dalali ni kodi ya mwezi mmoja, unalipa wewe, na mwenyenyumba pia anampa kodi ya mwezi mmoja, hivyo ili zipatikane fedha za dalali, anamshinikiza mwenye nyumba kupandisha kodi!.

Kama hauna haraka ki hivyo, tembelea maeneo unayoyataka, utaona vibao vya matangazo ya kupangishwa nyumba kwenye kona za mitaa, hapo unazungumza direct na wenye nyumba unajipatia unafuu wa kodi.

Ngarama za kupanga nyumba nzima ya kawaida, vyumba 4 vya kulala, kimoja ni master, sitting, dinning na jiko yenye geti na usalama ni kama ifuatavyo
Kinondoni kuanzia laki 3
Sinza Laki 4
Mbezi Beach laki 5
Masaki-milioni,
Osterbay- 1.5
labda room moja na sebule sefu kontena......kwa mahitaji yake si chini ya $600....
.....
 
Hapa Jangwani, Nyumba zipo lakini uwe tayarimkuhama wakati wa masika. Bei poa 22,000/= kwa room moja. Unaondokana na adha ya foleni mjini unatembea tu kidogo unafika
 
Lakini hivi haya majengo marefu yanayojengwa wanapanga wazungu/wahindi/wasomali n.k tu. Hewbu jaribu mtaa wa MINDU upanga yapo mengi kama saba hivi na nasikia moja lina apartment kama 100 hivi. Hebu jaribu utujuze
 
Sisi wenye familia za watoto wanane tutaishi na watu kweli? lol

kwa nini usiishi na watu?,au waliohama walikuwa na watoto 3,na pengine huyo alietaka nyumba nzima na yeye bila shaka ana watoto.nimemuelezea tu mazingira ya hiyo sehemu.
 
Ni kweli ni kueleweshana mazingira ya kitu tu wadau ishu sio with watoto au watotoless.
 
[QUOTE=Nyati;1578521]Lakini hivi haya majengo marefu yanayojengwa wanapanga wazungu/wahindi/wasomali n.k tu. Hewbu jaribu mtaa wa MINDU upanga yapo mengi kama saba hivi na nasikia moja lina apartment kama 100 hivi. Hebu jaribu utujuze[/QUOTE]

Mwenye habari kuhusu hizi apartment za MINDU tafadhali tunaomba atujuze!.
 
Back
Top Bottom