Natafuta mchumba/mke ila tuishi kujaribiana kwanza

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,231
Natafuta mrembo humu JF,tusomane kwa miezi 6 kwanza.

1.Bill ya nyumba alipe miezi 3 na Mimi nitalipa miezi 3 jumla miezi 6 ya kujifunzana tabia.
Tukikoleana tufunge harusi.

Nimechoka kuishi single JF
 
Mkuu imeandikwa wapi? Kwennye kitabu kipi kitakatifu kwamba muishi kwa majaribio ? Kwanza....
 
Kifupi kodi inakaribia kuisha na bado una mambo mengi ya kufanya..

Maana ndio kikubwa ulichosema hapo,huna vigezo wala nini ila bill tu..anyway,best of luck kwenye hiyo safari.
 
Kifupi kodi inakaribia kuisha na bado una mambo mengi ya kufanya..

Maana ndio kikubwa ulichosema hapo,huna vigezo wala nini ila bill tu..anyway,best of luck kwenye hiyo safari.

Acha hizo basi
 
Kama sio nidhamu nilitaka nikuulize kama uliwahi kumuuliza baba yako aliishi na mama yenu kwa majaribio kwa muda gani kabla ya kumuao! Ama muulize mama probation yake ilikuwa muda gani kabla hajapata mkataba wa kudumu kwa mzee!
 
Sasa mkuu kuna tatizo gani kushare kodi ili tujuane kama mmoja ni mbahili

Chakula,matumizi ya ndani,uko romantic,handsome kama avatar yako???,unajua maisha,miaka yako mingapi,unajua mipaka ya mwanaume kwenye nyumba,unajua majukumu ya mwanaume wa kibongo,hauna mtoto,mchumba hawara..
Jibu maana na mie nimeshachoka kuwa mpweke...
Ila kodi sahau kuchangia mda huu
 
hahha kwa hivi vigezo akipita vyote tutakuwa na malaika Gabriel humu ndani...
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hivi mnapotezaga kumbukumbu au unamaanisha kweli ukisemacho?? Binafsi nakumbuka vizuri kabisa umewahi weka uzi humu wa mwandani wako, Au UMEACHANA NA MPENZI/ MKE WAKO?
Umewahi weka uzi humu KUHUSU MKEO KUCHELEWA KURUDI HOM KISHA KUFIKA TU HIYO USIKU AKAFIKIA KUOGA, ulikuwa na mashaka nae, na wala si muda mrefu sana, nafikiri mwaka jana!
Kulikoni au unatafuta wa kuongeza inawezekana wee ni mfuasi wa wale wenzetu?!!
 
Chakula,matumizi ya ndani,uko romantic,handsome kama avatar yako???,unajua maisha,miaka yako mingapi,unajua mipaka ya mwanaume kwenye nyumba,unajua majukumu ya mwanaume wa kibongo,hauna mtoto,mchumba hawara..
Jibu maana na mie nimeshachoka kuwa mpweke...
Ila kodi sahau kuchangia mda huu

Hizo sifa zote ninazo,sasa mbona unakwepa kuchangia kodi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom