Natafuta mbwa

Nasikia obama uauza yule mbwa toka ufaransa, jaribu kuwasiliana naye.
 
Kwenye hii breed ya Rottweiler a.k.a Butcher dog, jiandae na misosi, na kesi...!
Tulikuwa na hii breed, mbwa wawili wanakula hawa balaa, mmoja peke yake anakula zaidi ya kilo nne 4kg. Kila mmoja alikuwa na kilo nadhani arobani na kitu... (40+kg).

Tuliwahi kuwapeleka mafunzo, jamaa akawarejesha kwanza walikuwa wanamtia hasara na pili waliuwa mbwa mwenzao.

Ila ni mbwa wenye kusifika sana kwa akili zao...!

Nikikumbuka jina a aliyetuuzia nitakuwekea hapa.



Mambo vipi?
Rottweiler ni breed nzuri sana, na mimi nahitaji kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwangu, kwa sasa nina germany shepherd jike, nikipata Rottweiler dume basi najua ulinzi umekamilika.
Tatizo la walinzi wanalala na unamlipa hela nyingi, ni bora hizo hela ninunulie chakula cha mbwa tu.
Nitashukuru sana mkuu ukinisaidia kwa hilo.
 
Inawezekana ni njaa, Rottweiler wanakula sana na wanahitaji mafunzo na mazoezi ya kutosha, hii ya kula plastic ni dalili ya frustration na nakushauri ukimuona Rot ameanza hivi bora tafuta mbinu ya kuachana nae, hawa mbwa wana hasira sana na kuna siku atachanganya hasira zake za njaa na frustration za mtu mgeni machoni pake utapata murder case! Kuwa makini sana.

Mkuu Kabachubya unataka hawa mbwa kwa ajili ya Ulinzi? Mimi ningelikushauri utafute German Shepherd, kwa mazingira ya Bongo wana-adapt vizuri na ni rahisi kuwa-train.
Matatizo ya Rotweiller au Dober wanahitaji proper training ama sivyo wanaweza kuwa killing machine na hawapendi mikonomikono mingi kwa hio nakushauri tafuta G.Shepherd.


Mkuu KWELI ni kweli unavyosema, lakini mimi nahitaji Rott kuongeza ulinzi, nina german shepherd jike kwahiyo nikipata Dober au Rott naona itakuwa safi na cost za kuwaudumia itakuwa chini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom