Natafuta kazi, nina Shahada ya Sheria

jonas255

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
222
104
Jamani nimemaliza chuo mwaka 2012 hadi sasa sijapata kazi nimemaliza degree ya kwanza ya sheria na nimeenda law school bahati mbaya matokeo ya law school hayajakaa vizuri...

Tatizo ni kua nina mchumba wangu nimeishi nae miaka miwili sasa bila kazi... Mwaka huu amepata uja uzito na anatarajia kujifungua muda si mrefu a mimi sina kazi... Jaman naombeni ushauri wenu nifanye nini maisha yamenipiga ngwara mwenzenu nimechanganyikiwa na rafiki zangu wananicheka sina hata wa kunishauri... Nimeona bora nikipimbie uku kwa wenzangu mnishauri
 
Pole sana but ungefanya ata biashara ukiwa unangoja kupata kazi usitegemee sana elimu
 
Jamani nimemaliza chuo mwaka 2012 hadi sasa sijapata kazi nimemaliza degree ya kwanza ya sheria na nimeenda law school bahati mbaya matokeo ya law school hayajakaa vizuri...

Tatizo ni kua nina mchumba wangu nimeishi nae miaka miwili sasa bila kazi... Mwaka huu amepata uja uzito na anatarajia kujifungua muda si mrefu a mimi sina kazi... Jaman naombeni ushauri wenu nifanye nini maisha yamenipiga ngwara mwenzenu nimechanganyikiwa na rafiki zangu wananicheka sina hata wa kunishauri... Nimeona bora nikipimbie uku kwa wenzangu mnishauri

kimbia tu mwenzangu
 
bro haya maisha tu,kama n hivyo embu tafuta kazi yoyote kwanza ufanye,halafu ndio ukomae kusaka kazi nyengine.Big up kwa kutomkimbia shemeji maisha ana panga Mungu zamu yako itafika tu usikate tamaa mkuu
 
Sasa ndugu wewe situation uliyo nayo unaijua still bado unafanya ngono zembe kweli.. Mimi nilitegemea uwe unamwomba mungu zaidi akufungulie njia. Ukome sasa ushaaribu.
 
Mmh hapo kuna kazi kijana Mimi naona issue no kupigana tu mzazi huckate tamaa wangu.
 
Pole jombaa endelea kuomba mungu.....ila kam unauwez nenda chuo cha bandar.au veta usom koz zenye practical utapat kaz harak kulik kung'ang'an na hiy digrii ya according....
 
usikate tamaa..Komaa tafuta tubiashara ya kuingiza kipato..Mungu ndie mtoa riziki..kama IPO IPO tu.kuzaa si kosa LA jinai kama nyie wengine mnavyomjudge mwenzenu.. take it from me.. maisha ni kutafuta na sio kutafutana. Nakuelewa situation uliyopo..
 
Tazama fursa zinazokuzunguka jitupe humo kijana usichague kazi, kupata kijikazi kwa LL.B bila postgraduate ya law school inabidi uwe na bahati ya mtende so usichoke kuitafuta hiyo postgraduate coz ndio taaluma uliyochagua hiyo. Tafuta shule (zipo nyingi tu hasa za msingi English medium hizi) waoneshe kiwango watakukubali tu or tafuta ofisi ya uwakili komaa nao mwisho wa siku wataanza kukufikiria. Niliwahi kupata hard time nafikiri zaidi yako baada ya kumaliza bachelor bt niliishi kwa mbinu hizo, wewe si wa kwanza & maisha ni lazima yaendelee muda haukusubiri.
 
Mtu mzima hadi akiandika hv ujue hali taiti, kuna ya kufanya moja pita kweny vishule hv vya english medium uwenda ukapata dili. Pili tafuta kamtaj ufungue gol lako la chips kuku nadhan chai itapatikana
 
ukishikwa shikamana...vua tai na hiyo suti nyeusi. ingia mtaani hata kutafuta kibarua kwenye saiti za ujenzi. au kijiwe cha shoe shine mwaya. lakini usimkimbie mama kijacho.
 
mbona huku kuna matenda mengi ya zege 25000@day zinduka kijana kuna watu wanamaisha mazuri wamesahau hata vyeti walimpaga nani awashikilizie..be creative and initiative aibu inakujaga bhana ukishapata hela usomi mbwembwe tu...
 
ukishikwa shikamana...vua tai na hiyo suti nyeusi. ingia mtaani hata kutafuta kibarua kwenye saiti za ujenzi. au kijiwe cha shoe shine mwaya. lakini usimkimbie mama kijacho.

Kaka mi mwenyewe nipo likizo ya chuo nkakutana na dogo nikawa nalalamika pesa sina akaniambia twende site kusaidia fundi , nliona ananzingua akanisisitizia basi siku ya kwanza nkaenda kazi ilikuwa ngumu lakini jioni unatia buku 10 mfukoni, leo hii nimetoka huko huko!!
 
mbona huku kuna matenda mengi ya zege 25000@day zinduka kijana kuna watu wanamaisha mazuri wamesahau hata vyeti walimpaga nani awashikilizie..be creative and initiative aibu inakujaga bhana ukishapata hela usomi mbwembwe tu...

mkuu thumb up!
 
Back
Top Bottom