Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Natafuta fundi mzuri sana anayeweza kunitengenezea Blackberry Bold 9930. Nimenunua mpya kabisa kama wiki mbili zilizopita, pasipo guarantee. Nilikuwa nimetoka ku snyc phonebook zangu kwenye Macbook usiku wa hivi karibuni. Nikafanya kosa la kuto eject ipasavyo (sijui kama ndio chanzo). Baada ya hapo iliendelea kufanya kazi ila nilipoamka asubuhi ikawa haiwaki tena zaidi ya ile red LED. Nimeipeleka kwa Mwesiga pale posta opposite na IPS Building Azikiwe/Samora Avenue lakini imewatoa knock out. Kabla sijaituma nataka nimpate guru wa BB bongo. Msaada tafadhali!!!