Natabiri: CUF itapoteza baadhi ya Majimbo Pemba

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
NB:
CCM inacheza hila mbaya Pemba kuwazuia wakazi wa huko wengi wao wakiwa wana CUF kujiandikisha ili wasipige kura mwakani kwa kisingizo cha kukosa sifa,lkn CUF haijatoa kauli yeyote kali hasa kwenye jumuia za kitaifa na kimataifa kuhusu jambo hili baya kabisa kisiasa!

Kama CUF wataridhika na kuacha watu wasijiandikishe ndiyo kusema kuwa CCM itatumia mwanya huo kuwapa wafuasi wao kadi za utaifa wa znz huko Pemba na kuwafanya wao washinde kwenye baadhi ya majimbo.

Lkn zoezi la uandikishwaji likihamia Unguja sina shaka kabisa kuwa kila mkazi wa huko atapatiwa kadi ya utaifa wa znz tena bure ili aweze kujiandikisha na hatimaye kupiga kura kwa sababu Unguja ndiyo makao makuu ya kura za CCM visiwani na hawapo tayari kumpoteza hata mtu mmoja asipige kura,labda kadi hizo wanaweza kunyimwa wakazi wa Mji Mkongwe tu ambao mara kwa mara huwa wanaichagua CUF!

kama CUF hawajashtukia jambo hili hapana shaka mwakani wana JF mtairudisha tena hii thread niliyotabiri maana itakuwa ndiyo habari "motomoto"kwetu kwenye siasa za ZNZ!

Soma habari hii ya gazeti la Mwananchi 07/14/09

ZOEZI la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Magogoni wilayani Micheweni, Pemba limeingia dosari katika siku yake ya kwanza baada ya mamia ya wananchi kutimuliwa na maofisa usalama katika baadhi ya vituo vya uandikishaji na kushindwa kujiandikisha.

Wananchi hao kutoka vituo vya Kinyasini, Finya na Wingwi Mapofu waliofika katika vituo hivyo na kupanga foleni mapema jana asubuhi, walijikuta wakitimuliwa vituoni na maafisa hao kwa kuwa hawana vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (Zan ID).

Maafisa hao waliwaambia wananchi hao kwamba hawapaswi kuonekana katika vituo hivyo kwa sababu hawana Zan ID.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi walilalamika kuwa maofisa wa usalama waliokuwa wamekaa karibu na maeneo ya vituo vya uandikishaji, waliwataka waondoke mara moja vituoni hapo.

Katika kituo cha Wingwi Mapofu, kulikuwa na maofisa wa usalama waliokuwa wamekaa katika baraza la jengo la kituo hicho wakitoa maelekezo kwa watendaji wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Micheweni, Abdallah Ali Said alithibitisha kupokea malalamiko hayo katika siku ya kwanza ya zoezi hilo kwenye Jimbo la Magogoni kisiwani hapa.

“Ukifika pale kituoni unaambiwa uondoke na maafisa usalama kwa sababu huna Zan ID, hii ni haki kweli," alihoji mtu aliyejitambulisha kwa jina la Khatib Hassan, 27.

"Mimi nina cheti cha kuzaliwa, kipande cha kupigia cha uchaguzi mkuu wa 2005 na uchaguzi mdogo wa mwaka 2003.”

Hassan alilalamika kuwa alipokwenda kwa Sheha ambaye anapaswa kutoa fomu za kuombea Zan ID, aliambiwa aende wilayani na alipofika huko aliambiwa anatakiwa kurudi kwa sheha.

"Ukienda kwa sheha anakwambia nenda wilayani na ukienda wilayani unaambiwa nenda kwa sheha. Wametufanya kama mpira wa kona; sheha apiga chenga, wilaya inafunga goli. Wanatunyima haki zetu hivi hivi,” alilalamika Hassan.

Naye Mbarouk Rubea, 48, alisema ana sifa zote za kuandikishwa kuwa mpigakura kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, lakini hadi sasa anahangaishwa hajapata kitambulisho na hatimaye amenyimwa kujiandikisha katika daftari hilo.

Akiwa amesawajika na mtoto mgongoni, Rehema Khamis, 32, alisema ameanza kukata tamaa ya kupiga kura katika uchaguzi ujao kwa sababu hajapatiwa kitambulisho licha ya kuwa ameshalipa Sh 500 za Zan ID.

"Hivi sasa nakaribia kulia maana nimeacha kwenda kuvuna mpunga wangu nikaamua kuja huku, lakini nahangaishwa na mtoto mgongoni. Nanyimwa haki yangu na maofisa wa usalama wanatufukuza hapa,” alisema Rehema.

Hata hivyo, maofisa wa usalama waliokuwa vituoni hapo walikataa kuzungumza na waandishi wa habari na kuwapiga marufuku watendaji wa tume kufanya hivyo.

Sheha wa shehia ya Mjananza, Hamad Said, ambaye pia ni wakala wa ZEC, alikatazwa na watu walioonekana kuwa ni maafisa wa usalama kuzungumza na waandishi wa habari waliofika kituoni hapo.

Baada ya kuitwa na waandishi kituoni hapo, sheha huyo alitoka na kusalimiana nao, lakini ghafla aliitwa ndani na kuagizwa asizungumze na waandishi.

”Nimekatazwa na wale pale nisiongee na ninyi,” alisema Said huku akielekeza kidole kwa maofisa hao na kurejea ndani ya kituo hicho.

Katika vituo hivyo kulikuwa na ulinzi mkali wa dola uliojumuisha polisi, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar (SMZ) na usalama wa taifa.

Wananchi wengi kisiwani Pemba hawana Zan ID, hususan wale ambao ndio kwanza wametimiza miaka 18 na wale waliokuwa nje ya Zanzibar.

Katika vituo vitatu ambavyo waandishi walitembelea, waligundua mamia ya wananchi walinyimwa haki hiyo kwa kukosa Zan ID.
 
CUF anzeni sasa harakati madhubuti za kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Pemba na baadae Unguja mwenye sifa za kupiga kura anajiandikisha,hizo ni hila za CCM kuchukua baadhi ya majimbo yenu,changamkeni na Operesheni zinduka haitakuwa na maana kama mtashindwa kuhakiki na kuondoa hila hizo mbaya za CCM chini ya kivuli cha maofisa Tume na Usalama wa Taifa!
 
CUF hii si ile yetu ya zamani bwana .Seif na Lipumba wamekula pumba na kuvuta chao .Si kawaida mambo yawe hivi na CUF hadi wadhani ni mchezo .CUF wanapashwa kujua kwamba kuanzia Pemba kunani ? Sasa wacha utaona mwenyewe itakavyo kuwa .

Lakini habari hii iunganishwe maana kuna mada hapa ina mambo haya haya
 
hivi utabiri maana yake nini? I thought watabiri husema kabla dalili hazijajitokeza kwa vile wana uwezo wa kuona mambo ambayo wengine hawayaoni kwa wakati ule.

By the way kabla hawajahukumiwa kuwa hawajafanya lolote kuhusu kutoa taarifa za mchezo mchafu kwa nini NK na Malyafale msitafute taarifa sahihi ili kujua km kweli wahusika wamelala na hawajayasema hayo mnayosema. Mbona bungeni tayari yamesemwa? Au?
 
Last edited:
Kama CHADEMA wana nia njema na Tanzania kama wanavyo-portray, naomba sana tena sana, waungane au kwa maana nyingine wawaambie CUF wa-merge kwa CHADEMA.

Hapa ndio na mimi nitakubali kwamba kuna chama cha upinzani na mbadala.

Na mimi naungana na mtoa hoja, Wazanzibar wanaweza kuwaadhibu CUF maana imeonekana kama muziki tu wa taarabu, hakuna jipya kutoka kwao.
 
Hapa ndio na mimi nitakubali kwamba kuna chama cha upinzani na mbadala.
CUF walianza na gia siyo wakati wa mfumo vyama vingi unaanza. Ukweli ni kwamba wakati huo wa-Zanzibari wengi tu walikuwa wamechoshwa na visa vya CCM na walikuwa tayari kwa Chama mbadala. Lakini kwa bahati mbaya visa vya CUF (na hasa vinara) ndivyo vilivyowafanya Wazanzibari walio wengi -waone ah!!! kama ni hayo basi ni afadhali ya hiyo hiyo CCM. CUF imeyumbisha upinzani Zanzibar.
Na pengine labda katika Jamhuri nzima ya Muungano.
 
Back
Top Bottom