Nassari aamua kugawa mashamba Arumeru, Polisi washindwa kuzuia zoezi

ngurati

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
221
240
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari jana aliungana na wananchi wa kata ya Makiba kijiji cha Valesca kugawa mashamba kwa wananchi hao baada ya Serikali kupitia Halmashauri ya Meru kushindwa kufanya hivyo.

Ikumbukwe mwaka jana wananchi hao walivamia mashamba Hayo yenye zaidi ya ekari 4600 na mbunge wao akaungana nao, Hali iliyopelekea ACU waliokuwa wamekalia ardhi hii na kuwakodishia wananchi hawa kwa kila msimu kukubali kutoa Jumla ya ekari 1,500 kwa wananchi lakini hadi leo halmashauri haikugawa kwa wananchi.

Sababu ya kushindwa kugawa ni pale madiwani wa halmashauri ya Meru (ambao wote ni wa ccm) walipotaka kuwapa wananchi ekari 500 tu Alafu wapige Dili ya ekari 1000 na wananchi wakagoma.

Polisi walikuja kujaribu kuzima zoezi na Mabomu na risasi Mbunge Nassari akawaambia leo hamuondoki na mtu Kama mnataka mtu wamchukue mbunge lakini wajue hii ni Meru. Baada ya Kama saa mbili wakaondoka na zoezi likaendelea.

=========

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari juzi aliongoza wapiga kura wake kugawa shamba linalomilikiwa na Chama cha Ushirika mkoani Arusha (ACU), akisema amechoka kuona wananchi wake wakisotea ardhi ilhali kuna maeneo hayaendelezwi.

Nassari aliongozana na wapiga kura wake hadi eneo la shamba la Valeska na kuanza kuwagawia ardhi bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mmiliki wa ardhi husika.

Akiwa katika eneo hilo, alipima ardhi kwa kuhesabu hatua na kuigawa kwa wapigakura wake wenye uhitaji wa ardhi.

Kutokana na uamuzi wake huo wa kujichukulia madaraka na kuigawa ardhi kuonekana kuwashangaza wengi, mwandishi wa habari hizi alilazimika kuomba ufafanuzi wa tukio hilo kupitia simu yake ya kiganjani, ambapo alisema amelazimika kuchukua uamuzi huo anaouona unafaa ili wananchi wake wapate ardhi.

Alisema amelazimika kuingilia kati suala hilo, kutokana na migogoro isiyoisha ya ardhi wilayani Arumeru kwani awali wahusika wa ushirika huo walitoa ekari 1,500 za ardhi na kuzigawa kwa wananchi ili kuepusha maandamano na uvamizi wa mara kwa mara, lakini kinyume chake ardhi hiyo hawakupewa wananchi, bali madiwani wa Halmashauri ya Arumeru wamekuwa nao wakiitaka ardhi hiyo.

Aidha, alisema wakati wananchi ambao ni wapigakura wake wakidai ekari hizo, kuna watumishi wamejitwalia ekari 400 kati ya hizo 1,500 zilizotolewa na ACU na kujimilikisha wao huku watumishi hao bila kuwataja majina wakiwakodishia wananchi wake.

Alisema madiwani wa Halmashauri hiyo walitoa ekari 500 na kuwapa wananchi na ekari nyingine wakipanga mambo yao na kutokana na hali hiyo, anaamini kuna maslahi ya watumishi wa halmashauri hiyo.

"Kutokana na hali hiyo nimeamua kama mbunge nigawe ardhi mwenyewe kwa kupima kwa miguu ili kila mwananchi aweze kupata ardhi sababu watendaji wameshindwa kusimamia haki.
"Hapa ndio nimeanza na nitaendelea kugawa ardhi kwenye mashamba yasiyoendelezwa na hayo ndio maamuzi yangu kama Mbunge. "Nasema siwezi kukubali wananchi wangu kila siku walalamikie masuala ya ardhi wakati kuna madiwani, Mkuu wa Wilaya (DC) na viongozi mbalimbali. Nimegawa Valeska, bado nitakweenda Mbughuni hadi Kikuletwa nitagawa ardhi, kama Mbunge nimechoka na migogoro isiyoisha".

Suala la Nassari kugawa ardhi bila kufuata utaratibu liliibuka mara baada ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene kufanya kikao na maofisa ardhi na wapimaji wa Mkoa wa Arusha kutoka Halmashauri tatu za Jiji la Arusha, Arusha Vijijini na Arumeru ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo na kutafuta suluhu ya migogoro hiyo.

Katika mazungumzo hayo na watumishi hao, pia walifika viongozi kutoka ACU ambao walisema chama hicho kilishatoa ekari 1,500 kwa wananchi wa wilaya hiyo, lakini madiwani walikataa eneo la Mashariki walilopewa na kutaka wachague eneo wanalolitaka wao.

Alisema ACU imeshatoa eneo hilo ili kuwapa wananchi, lakini kuna milolongo mingi ikiwemo masuala ya siasa kati ya madiwani ambao hawakubaliani na maamuzi ya ACU.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mjumbe wa Bodi ya ACU, Furahini Mungure alisema shamba hilo la ACU ni kubwa na linahitaji kuendelezwa ikiwemo kujenga vitega uchumi sambamba na mradi wa ghorofa 17, hivyo kutokana na mgogoro huo ukiwamo wa suala la Nassari kugawa ardhi kunarudisha nyuma masuala ya uwekezaji.

"Tunamshangaa Mbunge kwa kitendo cha kugawa ardhi tunayoimiliki bila kufuata taratibu, yeye amechukua kinamama, watoto, wazee, vijana na kwenda kuwagawia ardhi kwa kuwapimia na miguu… sasa hii ni siasa ili aonekane ni mwema kwao kumbe hakufuata taratibu hivyo tunakuomba Naibu Waziri uingilie kati mgogoro huu," alisema. Alisema wakati Nassari alipokuwa akigawa ardhi hiyo, Polisi walifika eneo hilo la shamba la Valeska ili kumwamuru mbunge huyo na wananchi wasitishe kugawana ardhi, lakini bila ya kutumia nguvu.

"Polisi walimhoji Nassari kwa nini anafanya hivyo, lakini yeye aliendelea kugawa ardhi na hapo tunawapongeza polisi licha ya ardhi ya shamba letu kugawiwa na mbunge kwa wananchi sababu kulikuwa na wananchi wa rika mbalimbali wakiwemo watoto kama wangeweza kuchukua maamuzi magumu watu wangeumia. "Lakini kwa busara, polisi waliondoka na kumwacha Nassari akigawa ardhi ambayo si halali kwa wananchi, hivyo hatujui hii ni mbinu ya mtaji wa kisiasa au ni nini maana masuala ya ugawaji ardhi yana taratibu zake kisheria," alisema.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arumeru, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Benedict Mapujila alisema polisi walitumia busara maana kulikuwa na wananchi wengi pamoja na watoto.
Naye Simbachawene alisema inashangaza kuona Mbunge anayejua sheria, taratibu na kanuni kuchukua maamuzi yasiyofaa na kuahidi kuonana naye ili kuzungumza zaidi juu ya suala hilo.

Pia alisema atapanga ziara ya kukutana na madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Nyirembe Munasa ili kutatua mgogoro huo, kwani ameshindwa kukutana nao kwa sasa kutokana na misiba iliyotokea ambayo ilisababisha wafanyakazi wa halmashauri hiyo kufa kutokana na ajali eneo la Nduruma.

Wilaya ya Arumeru imekuwa na migogoro mingi ya ardhi hali inayosababisha wananchi kuvamia mara kwa mara mashamba ya wawekezaji kwa madai ya kuwa mashamba hayo hayajaendelezwa.

CHANZO:
​Habari Leo

attachment.php

attachment.php

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    759.6 KB · Views: 6,713
  • image.jpg
    image.jpg
    627.6 KB · Views: 6,534
  • image.jpg
    image.jpg
    883.8 KB · Views: 1,668
Huyu kiongozi wa Polisi kajitahidi sana kutumia akili zake. Otherwise yangetokea maafa
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari jana aliungana na wananchi wa kata ya Makiba kijiji cha Valesca kugawa mashamba kwa wananchi hao baada ya Serikali kupitia Halmashauri ya Meru kushindwa kufanya hivyo. Ikumbukwe mwaka jana wananchi hao walivamia mashamba Hayo yenye zaidi ya ekari 4600 na mbunge wao akaungana nao.
Mkuu Ngurati, asante kwa taarifa hii, nchi hii huendeshwa kwa kitu kinachoitwa sheria, taratibu na kanuni!,
Jee Mhe. Mbunge wenu Nasari, anayo mamlaka ya kugawa land?!.

Kwa kukusaidia wewe na wengine wengi wasio jua sheria, kati ya mikataba yote mingine, unaweza kuingia mkataba kwa kauli tuu, lakini umiliki wa ardhi, ni lazima ufanywe kwa maandishi!, hili la Mhe. Mbunge kugawa mashamba kwa kauli na vitendo, bila maandishi rasmi ni kujifurahisha tuu!.

Kama eneo linatolewa kwa kauli tuu!, basi mimi Pasco wa jf, nimemgawia Ngurati, lile eneo lote la Magogoni hadi lilipo lile jumba jeupe!, ni eneo lako, lichukue!. Utakubali?!.

Huu mtindo wa Mhe. Mmbunge kujitwalia mamlaka nje ya uwezo wake ili tuu kuwafurahisha wananchi, kwa manufaa ya kujijenga kisiasa ili kupendwa, inaitwa "populist leadership!", wanachi watampenda sana mbunge wao, na wale wote watakaopokea maeneo hayo kwa kauli tuu ya Mhe. Mbunge wao, watakuwa wanajifurahisha tuu!.Anachofanya Mheshimiwa Mbunge ni uwamizi!.

Kiukweli inawabidi Chadema waishukuru sana serikali ya bwana "dhaifu" kuendeea kuwachekea "nyani" shambani, kwani watakachovuna ni mabua tuu!. Kama tumefikia hatua ya vyombo vya dola kuangalia na kuviachia vitendo vya uvunjanji wa sheria wazi wazi bila kuchukua hatua zozote!, basi ndio tunaanza hivi kidogo kidogo hadi tutaweza kuhamashisha maandamano makubwa ya nchi nzima kuelekea pale magogoni, na kumtoa yule mpangaji mahali pale!.

Hongera zake sana Mhe. Nasari kusimama na wanachi wake, kuwapatia kila wanachokitaka!, to hell with sheria taratibu na kanuni!, its peoples power!.

Pasco.
 
Sheria ya ardhi ipo wazi acheni ushabiki wa kisiasa mbunge hana uwezo wa kugawa mashamba!
 
Naunga mkono hoja. Maana wakubwa hugawana tu Mfano KJ chukua IPTL na wewe Lowahasa Chukua Richmond, Kinannnnnna chukua Ndovu, Pindua kamata Escrow, Nkapa take that Kiwira etc........ Hivyo kwa wananchi ni haki yao after all wanataka kuzalisha
 
lakini mimi pia ni mmeru, na naishi haya maeneo, ila kijijini tuko takribani kaya 4000 na waliogawana haya mashamba haifikii hata kaya mia moja, je na sisi tuliobaki tujipange tukagawane yale yale maeneo nassary aliyogawa, je nini kitatokea endapo tutakutana na zile kaya mia waliogawana maeneo na nassary na sisi kaya 4000 tulobaki hatukupata???? Naombeni ushauri wenu kwa sababu kila mtu anataka ardhi, je ni namna gani tunaweza kupata wote sawa na kisheria zaid, ushauri kabla ya saa sita coz sisi tuliobali tunajipanga tukagawane yale yale mashamba
 
Unagawa mashamba kiholela kama maandazi, haya kila la heri maana mnatengeneza bomu lije kuwalipukia wenyewe.
 
Mkuu Ngurati, asante kwa taarifa hii, nchi hii huendeshwa kwa kitu kinachoitwa sheria, taratibu na kanuni!,
Jee Mhe. Mbunge wenu Nasari, anayo mamlaka ya kugawa land?!.

Kwa kukusaidia wewe na wengine wengi wasio jua sheria, kati ya mikataba yote mingine, unaweza kuingia mkataba kwa kauli tuu, lakini umiliki wa ardhi, ni lazima ufanywe kwa maandishi!, hili la Mhe. Mbunge kugawa mashamba kwa kauli na vitendo, bila maandishi rasmi ni kujifurahisha tuu!.

Kama eneo linatolewa kwa kauli tuu!, basi mimi Pasco wa jf, nimemgawia Ngurati, lile eneo lote la Magogoni hadi lilipo lile jumba jeupe!, ni eneo lako, lichukue!. Utakubali?!.

Huu mtindo wa Mhe. Mmbunge kujitwalia mamlaka nje ya uwezo wake ili tuu kuwafurahisha wananchi, kwa manufaa ya kujijenga kisiasa ili kupendwa, inaitwa "populist leadership!", wanachi watampenda sana mbunge wao, na wale wote watakaopokea maeneo hayo kwa kauli tuu ya Mhe. Mbunge wao, watakuwa wanajifurahisha tuu!.Anachofanya Mheshimiwa Mbunge ni uwamizi!.

Kiukweli inawabidi Chadema waishukuru sana serikali ya bwana "dhaifu" kuendeea kuwachekea "nyani" shambani, kwani watakachovuna ni mabua tuu!. Kama tumefikia hatua ya vyombo vya dola kuangalia na kuviachia vitendo vya uvunjanji wa sheria wazi wazi bila kuchukua hatua zozote!, basi ndio tunaanza hivi kidogo kidogo hadi tutaweza kuhamashisha maandamano makubwa ya nchi nzima kuelekea pale magogoni, na kumtoa yule mpangaji mahali pale!.

Hongera zake sana Mhe. Nasari kusimama na wanachi wake, kuwapatia kila wanachokitaka!, to hell with sheria taratibu na kanuni!, its peoples power!.

Pasco.

nadhani utakuwa unaongelea MSALANI unapiga kelele kama unajiha....rishia MSALANI.. inamana hujui au huoni picha hizo? we tamka vyovyote uwezavyo wananchi wameshajigawia chao. POLICCM wenyewe wameenda hapo lkn wameufyata wamesepa. we umekalia SHERIA tanzania kuna sheriaaa usanii??
 
Sheria ya ardhi ipo wazi acheni ushabiki wa kisiasa mbunge hana uwezo wa kugawa mashamba!

Mbona Jk na viongozi wake ndani ya ccm wanagawana rasilimali za taifa kama madini gasi maliasili hata hyo ardhi unayopigia kelele au wao wana haki zaidi?
 
Back
Top Bottom