Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Mwaka 2008 Aprili wakati wa kufungua shule baada ya likizo fupi ya pasaka Chidya Secondary iliyopo wilayani Masasi mkoani Mtwara ulitokea mgomo uliosababishwa na wanafunzi kupikiwa uji usio na sukari kwa siku 2 mfululizo.
Wanafunzi wakaamua kufanya uharibifu wa mali za shule ikiwemo na gari kubwa (Lory) ya shule na kwa kulichoma moto na staff ya walimu ilichomwa moto kisha wanafunzi wote ukimwondoa mmoja tu ambaye alikuwa kiongozi wa nidhamu walikimbilia porini. Kenneth kijana alikuwa mlokole na ni mtoto wa mkuu wa wilaya mstaafu alibaki shule na walipokuja FFU walimzoa na kuondoka naye.
Asubuhi wanafunzi walianza kurejea taratibu na kujiandaa kisha kuingia darasani kama kawaida na shule ilipoa kimya.
Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na bodi ya shule ikakaa kikao cha dharura na kuja na maadhimio kadhaa pamoja na;
1.Kuwafukuza shule wanafunzi wachache.
2.Kuwasimamisha shule wanafunzi kadhaa na kuwaambia warudi na 150,000/= pindi wataporudi shule na wazazi wao.
3.Kila mwanafunzi aje na 75,000/= atakaporudi likizo ya Juni/Julai.
4.Baadhi ya viongozi wa wanafunzi na wanafunzi ambao walionekana kuwa ni wahamasishaji wakubwa wa mgomo ule kuburuzwa mahakamani baada ya kufukuzwa shule.
5.Shule haitafungwa kwa dharura na hatimaye wanafunzi waendelee na masomo mpaka Juni itakapofungwa kwa mujibu wa ratiba ya wizara ya elimu. Msimamo huu ulisimamiwa kikamilifu na headmaster nguli aliyekywa mjeshi Mr. Mwatenga.
Mkuu wa mkoa Albert Chalamila na timu yake wamefanya uamuzi nzuri sana ingawa wapo watakaoumizwa na kuathirika kwa uamuzi huu. Kama atatumbuliwa basi ni kwasababu za kisiasa tu.