Nashukuru jitihada za wazazi wangu nikaacha kuwa kilaza na kumaliza kwa ufaulu mzuri chuoni

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,047
Tukija kwenye suala la shuleni, mimi niwe mkweli, Sikuwa na uwezo wa kufundishwa na mwalimu pekee darasani, pia kujisomea ilikuwa taabu, nimeanza kujisomea form 2.

Nashukuru wazazi waliweza kunipigania nisome english medium lakini hii pia isingezaa matunda kama ningeachwa nisome kivyangu.

Tangu nikiwa darasa la kwanza Mzee alikuwa anamlipa mwalimu wa shuleni kila mwezi anakuja kila siku nazoenda shuleni kunifundisha na hapa ndio nilikuwa naelewa vizuri zaidi, shuleni nikawa nashika namba 6 kati ya 40.

Darasa la tano nikaanza kwenda tuisheni tupo watu wanne wa darasa letu, huko nilipoenda nikakuta wote wanaoshika namba 1 na 2 wapo hapo, hii ilinisaidia kidogo kupata ushindani nikawa nashika namba 4 darasani.

Form 1 sasa nilipelekwa boarding yani huko nilikaa miezi mitano hata sielewi elewi, namba zilikuwa zinashuka kila mtihani. Ikabidi niwaambie wazazi nirudi kuendelea na mfumo wa tuishen.

nilirudi shule ya day ila sasa upande wa tatizo darasa moja watu 30, hapa kwangu haikuwa tofauti na shule, wala haikunisaidia kupata ile attention ya mwalimu. Ikabidi nitafute tuition ambayo tupo wanafunzi watatu tu kuna ile attention mwalimu anakupa, nilikuwa naenda kila siku ili kufidia mambo ya nyuma yaliyonipita boarding, matunda nikaanza kuyaona nilianza kuwepo top 10 darasani.

Basi kuanzia hapo hadi form 4 nikawa vizuri darasani na nikaweza kuchapa division 1 yangu.

Form 5 na 6 nilienda nilichagua mkondo wa masomo ya boashara. sikutaka kurudia kosa kwenda boarding, nilikomaa na day huku nikipewa assist ya tuition yenye wanafunzi wachache, form 6 nikaweza kugonga division 1 japo ya kuchechemea.

Chuoni sasa hakunaga tuisheni ila nilifanya uchunguzi mapema nikaambiwa kunakuwaga na group discussion mnakuwepo watu kama 8 hivi mnadiscuss.

Kiukweli chuo kilikuwa kigumu, ila discussion zilinisaidia sana, Kila siku jumatatu hadi ijumaa ilikuwa ni lazima nishinde kwenye magroup, nikiona group lolote mimi nimo, yani ilifikia hatua naitwa mzee wa groups. Kiukweli pale chuoni watu wengi walikuwa wanakuja kufanya sup ila kwa hii system ilinisaidia nisizijue, chuo nacho kwenye suala la GPA walikuwa wanakaza ila nikaweza ku graduate na 4.2.

Baada ya hapo nilimalizia proffesional certificate ya taaluma yangu, ila huku nilitegemea sana youtube.

Ndio sysytem iliyoweza kunifikisha chuo na hatimae kupata ajira ambayo nayo imenisaidia niweze kufanya biashara zangu hapa mjini, nashukuru sana kwa walimu wote wa tuishen na watu wa groups.

Ujumbe wangu kwa wale wenye uwezo mdogo darasani, Hakikisha tuishen iwe kipaumbele na ukifika chuoni stick sana kwenye group discussions.
 
Sky Solidier ! Hii mada ungepeleka kwenye jukwaa la watoto
 
Back
Top Bottom