Napingana na Mahakama kuzungumza na Mbowe peke yake bila watuhumiwa wengine, watuhumiwa watatu wanatetewa na Mbowe Kwenye Haki yao ya Kula?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Askari ma gereza wamemfuata FREEMAN Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani.

Hapa Kuna utata na mahakama imeshindwa kabisa kusimamia Haki, ushahidi wa Upande wa utetezi unaonyesha Hawa askari makomando walipandikizwa kwenda Kwa Mbowe na walipobaini Kwamba Kuna viashiria vya uhalifu wakamjulisha Urio na ukamataji ukafanyika. Kwa hiki kilichotokea Leo mahakamani unabaini Kwamba mahakama na serikali vimeshindwa kutafsiri Hii kesi.

1. Kama maelezo ya watuhumiwa walikiri kwanini Leo wawekwe pamoja na Mhe. Mbowe?

2. Kama walikiri na wakasimama na Jamuhuri Mbowe afungwe kwanini Mbowe awe mtetezi wa watu ambao Jamhuri inatuaminisha ni maadui wa Mbowe?

3. Haki ya kula ni ya wote, nani amemwambia Mhe. Jaji Kwamba watuhumiwa watatu wanakubaliana na kauli ya Mbowe?

Ni kitu Gani kilichomkata Mhe. Jaji kuuliza mtuhumiwa mmojammoja kama kauli ya Mbowe ni kweli au so kweli? Au Mhe. Jaji alikuwa anatambua kinachoendelea akajifanya hajui?

Kwa upande wa mawakili wa upande wa serikali, kwanini awakupinga kauli ya Mbowe Kwamba Wana miezi mitano awali? Means wao walijua lakini wakaona ni sawa? Kwamba mawakili wa serikali walishindwa kuomba Mhe. Jaji ajiridhishe?

Mwisho, kitendo cha Jaji kujifanya afahamu watuhumiwa awali na wakati Kila siku anakaa nao Hadi saa Kumi na Moja si Jambo la kibinadamu Bora angekaa Kimya. Kibaya Zaidi badala akae Kimya anataka kumrushia mpira kibatala wakati Msajili amepelekewa Hiyo taarifa akaikalia.

Hata kama awa watu ni magaidi kama mnavyotaka jamii iamini haikuwa sahihi kuwanyima chakula. Masaa ishirini na nne watu wanakunywa uji kikombe kimoja kisa CHUKI za Kisiasa na mnataka watu waamini Tanzania tunapendana? Watu wapate magonjwa wafe kisa chakula? Its painfull
 
Inasikitisha sana, miezi mitano watuhumiwa hawali chakula na magereza/serikali inaona powa tu?! There might be misconductions amonga the prison officers in there.

Kama taarifa zilishafika, wahusika wawajibishwe kwakulikalia kimya hili swala muda wote huo wa miezi mitano.
 
Askari ma gereza wamemfuata FREEMAN Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani....
Usichokijua ni hiki.

Mbowe kunyoosha mkono na kuzungunzia chakula ni code language.

Mbowe kuitwa chemba na Jaji akiwa na mawakili wa pande zote ni coded kuna jambo mtambuka wanaenda kuwekana sawa.

Kama ilikuwa ni chakula tu, ilitakiwa amri ya Jaji itoke kwamba, watuhumiwa wawekewe ratio yao wanapotoka mahakani waikute huko mahabusu.

Kinacgotafutwa ni mazingira ya kuimaliza kesi kabla hatujaingia aibu zaidi.

Mimi ni CCM
 
Acha kupotosha ,hao sio makomandoo wajeshi (JWTZ) bali ni raia tu kwani walikwishafukuzwa kazi.

Pili hawakupandikizwa kufanya ugaidi yule urio aliyewatafuta alieleza kabisa aliwatafuta ili kufanyakazi ya Ulinzi binafsi.

Tatu katika ushahidi uliotolewa hakuna sehemu yeyote kwamba hao ex makomandoo walieleza kwamba kunaviashiria vya ugaidi.

Nne hadi huyu shaidi wa leo hakuna shaidi yeyote wa upande wa serikali aliyeweza kutoa ushaidi wa kufanyika vitendo vya ugaidi , kama yupo mtaje na ueleze alieleza nini
 
Ni Tanzania tu ambapo jaji hajui kama watuhumiwa wanakula au laah!!!!. Miezi mitano jaji hajawahi kuwaza kama hawa watuhumiwa napataje chakula?

"Jaji kuteta na MBOWE naziona dalili za jamhuri kupiga magoti kesi ifutwe"
 
Askari ma gereza wamemfuata FREEMAN Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani...

Kuna kitu sijakielewa hapa. Nimewahi kusikia kuwa gerezani chakula cha jioni kinaliwa mapema sana (pengine kabla ya 5pm). Sasa kama hawa wanatoka mahakamani 5pm, maana yake, wanakuta milo yote imeshapita. Wamewezaje kuishi kwa miezi mitano bila kula? Au labda wanatunziwa chakula cha jioni?
 
Back
Top Bottom