Uchaguzi 2020 Napinga viongozi wa dini kukutana kwa lengo la kuelezea kinachoitwa mafanikio ya Rais Magufuli, hii ni kampeni na haikubaliki

Kwa mtazamo wako upo sahihi kulingana na mfumo unakuendesha (siujui) Ukweli viongoziozi wa dini wanao jielewa hawawezi kujiingiza katika mambo ya vyama (mambo ya hovyo) tuweni wa kweli hao viongozi wamepotoka.
Hii amani unayoiona na yenye kutuwezesha kuwasiliana humu jukwaani chanzo chake ni nguvu za Mungu. Chanzo chake ni nchi kukabidhiwa mikononi mwa Mungu tangu tarehe 8 Desemba 1961. Huo ndio umuhimu wa wale viongozi wa dini uliowaona ndani ya ule ukumbi.

Kuna nchi za kiafrika hazina bahati ya kuwaona marais wastaafu wakipiga picha ya pamoja wakiwa wanacheka na kufurahi. Viongozi wa kidini wana nguvu za ndani ya nafsi zao na zile nguvu za nje, ni watu muhimu sio wa kuwadharau.
 
We jamaa ni muongo sana !
 
Kimbunga cha LISSU kimefunua nyeti za kuku watamuita hadi yesu feki yule alikuja Kenya kwamba amerudi duniani kuunga mkono juhudi.
Mwisho watamwita na shetani ndugu yao
 
Kimbunga cha LISSU kimefunua nyeti za kuku watamuita hadi yesu feki yule alikuja Kenya kwamba amerudi duniani kuunga mkono juhudi.
Mwisho watamwita na shetani ndugu yao
Hivi mbona mnapambana Sana kupamba kitu kisichopambika? Mnampa Sifa TL aszistahili mbona kuliko I😂🤣😂! Au ndio mahaba niue hayo😂🤣😂! Anyway, nawapa pole Sana kwa aibu ya mwaka inayoamza kuwapata! Mbowe katimuliwa na wapiga kura, huyo robot wenu TL naye Sasa hivi wameshaanza kumtumua wapiga kura maana wameshamshitukia na ukibaraka wake😂🤣😂! Hamna sera na Wana Hamna kitu Cha kuonyesha mlichofanya kwa manufaa ya nchi yetu lakini bahati yenu mbaya mna Kila kitu kubaya mlichofanya kutuhujumu nchi yetu...na wanchi wanatambua🤔! Na kwa bahati yenu mbaya Hamna hekima ya kuchutama🙊!
 
Utaafiki hivyo hivyo kama viongozi wa dini watakusanyika Kwa lengo la kuelezea mabaya ya serikali ya awamu ya 5?

Viongozi wa dini kwa nafasi zao wanapaswa kuunga mkono au kukosoa serikali, napinga hili la kukusanyika kwa ajili ya hilo!
Hivi CHADEMA wangefanya hivyo si watu mapovu yangewatoka! Lakini acha wafanye tu. Hao viongozi wa dini kwa kuwa wamepewa chai na kitu kidogo hata kama wakipigia kura CCM haitawasaidia. Sisi waumini wenye idadi ya mamilioni ndo tuna kura nyingi. Tunajua wa kumpigia.
 
Taarifa hii imetolewa na Alhaji Musa Salum ambaye ni Sheikh wa Bakwata wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba eti viongozi wa dini wanatarajia kukutana tarehe 30 July jijini kwa lengo la kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya 5!

Taarifa inazidi kueleza kwamba Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu ndugu Kassim Majaliwa.

Tangu lini viongozi wa dini wakawa wasemaji wa serikali? Hii mbona ni siasa ya kiwango cha chini sana! Sasa tukisema hawa viongozi njaa wa dini wakiwemo maaskofu kadhaa walioshuka hadhi wanatumika tutakuwa tunakosea?

Tutahakikisha tunahamasisha wananchi kupuuza kila kitakachojadiliwa na hawa mamluki bila kuchoka.

Lazima upate kiharusi safari hii.....
manake kichapo kinaendelea kuharibu mudi yako
 
Mwalimu aliondoka wala hakukuwa na kampeni kama hii, ila mafanikio hata mtoto mdogo wa darasa la nne atakwambia. ..haya mafanikio ya huyu mwendazake kuhubiliwa namna hii? Kunani?
Hivi marehemu wenu alikuwa na mapungufu gani? Mbona CCM mnahangaika saana...

Naunga mkono hoja!! Legacy haihubiliwi kama neno la Mungu kila jpili...kama ipo ipo tuna kama hana hana tu hata uhangaike vipi kuipamba!!
 
Back
Top Bottom