Napendekeza kufanyike maandamano ya vyama vyote

JIS

Member
Dec 5, 2011
73
48
Wana JF napendekeza kuwepo na maandamano ya vyama vyote vya siasa kutokea Mnazi Mmoja hadi Uwanja wa Taifa. Maandamano hayo yaongozwe na CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, UDP, na vyama vingine. Wanachama wakae kwenye kundi la vyama vyao ili kujua chama kipi kina wanachama wengi. Hakuna kutoa posho wala usafiri kwa wanachama. Mwisho wa maandamano kuwepo na Hotuba za Wenyeviti wa Vyama kuzungumzia muskakabali wa siasa wa nchi hii na wito wa kudumisha amani na mshikamano. Pia, viongozi hao wakemee ufisadi kwa aina zake, na uvivu.
Nawasilisha.
 
Sawa na kuomba chui na swala wafanye amani kati yao wasiuane! Halafu chui akale nyasi?
 
mmh! Hivi wewe si kipindi kirefu ulikuwa Umeacha Kunywa Pombe!

Hata harufu ya pombe siijui mwenzangu. Natamani maandamano hayo ili vyama mfu vijulikane waziwazi na iwe kipindi cha chama kitakachoshika dola 2015. Nimeona kampeni za diwani wa CUF Arusha nikachekaaaaaa.
 
Polisi watapigaje mabomu kama na chama chao kipo tena na hawara yake
 
Hata harufu ya pombe siijui mwenzangu. Natamani maandamano hayo ili vyama mfu vijulikane waziwazi na iwe kipindi cha chama kitakachoshika dola 2015. Nimeona kampeni za diwani wa CUF Arusha nikachekaaaaaa.

Jombaa jamaa bado hawajakuelewa.
 
Back
Top Bottom