Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Ndugu zangu,
Kuna tabia imeanza kujengeka miongoni mwa wanasiasa hususan wa aina ya Nape kutaka kuwazuia wazee na viongozi wastaafu kutoa maoni yao kuhusui mwenendo wa serikali katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivi karibuni, Nape ameamua kumjibu Mhe. Lowassa kuhusu kauli yake ya mara kwa mara ya kuikumbusha Serikali kuhusu umuhimu wa kuwa na mkakati maalum wa kushughulikia ajira kwa vijana na kwamba kadri Serikali inavyozidi kuwaacha vijana wamezagaa mitaani bila kazi au ajira, ndivyo Serikali inavyozidi kutengeneza bomu litakalokuja kulipuka baadaye. Hali hii pia imewahi kumkumba Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye. Kuna maoni fulani alitoa lakini alijibiwa na kiongozi mmoja wa umoja wa vijana wa ccm kuwa yeye wakati wa uongozi wake alifanya nini.
Kwa nchi inayoheshimu uhuru wa kutoa mawazo, sioni kama hilo ni tatizo. Hata kama Lowassa alikuwa Serikalini na hakushughulikia suala la ajira kwa vijana kwa namna anavyoongea sasa, je, hiyo immnyime uhuru wa kusema ili Serikali au viongozi waliopo sasa nao wasisahau! Je, kama Mzee Mkapa kuna jambo ambalo kwa masusudi au bahati mbaya hakushughulikia wakati wa utawala wake na sasa analiona kwa ukaribu zaidi na umuhimu wake kwa ustawi wa nchi, je akae kimya asiishauri Serikali!!! Upuuzi gani huu!!
Tabia hii ya kuwashona mdomo viongozi wasiongee na kuikosoa Serikali yao ni udikteta wa hali ya juu uliopitiliza. Viongozi wastaafu ni hazina muhimu na haswa nchi inapokumbana na changamoto mbalimbali za kiuongozi kama wakati huu wa uongozi uliopwaya wa kikwete. Ndiyo maana wengi wao bado wanaendela kulipwa mafao au marupurupu manono yanayotokana na kodi ya wananchi.
Kwa mantiki hiyo, namshauri Nape aache siasa zake za majitaka kuwazuia viongozi wetu wastaafu watamke wanachoona kinafaa kwa ustawi wa nchi yake. Anachotakiwa Nape ni kuishauri Serikali ya chama chake kueleza hali halisi na kutoa takwimu zinazojibu hoja iliyotolewa na Mhe. Lowassa na siyo kuwaita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja maneno yasiyo na mbele wala nyuma.