Nape waache wazee na viongozi wastaafu waikosoe serikali hata kama wao hawakutenda

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Ndugu zangu,

Kuna tabia imeanza kujengeka miongoni mwa wanasiasa hususan wa aina ya Nape kutaka kuwazuia wazee na viongozi wastaafu kutoa maoni yao kuhusui mwenendo wa serikali katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivi karibuni, Nape ameamua kumjibu Mhe. Lowassa kuhusu kauli yake ya mara kwa mara ya kuikumbusha Serikali kuhusu umuhimu wa kuwa na mkakati maalum wa kushughulikia ajira kwa vijana na kwamba kadri Serikali inavyozidi kuwaacha vijana wamezagaa mitaani bila kazi au ajira, ndivyo Serikali inavyozidi kutengeneza bomu litakalokuja kulipuka baadaye. Hali hii pia imewahi kumkumba Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye. Kuna maoni fulani alitoa lakini alijibiwa na kiongozi mmoja wa umoja wa vijana wa ccm kuwa yeye wakati wa uongozi wake alifanya nini.

Kwa nchi inayoheshimu uhuru wa kutoa mawazo, sioni kama hilo ni tatizo. Hata kama Lowassa alikuwa Serikalini na hakushughulikia suala la ajira kwa vijana kwa namna anavyoongea sasa, je, hiyo immnyime uhuru wa kusema ili Serikali au viongozi waliopo sasa nao wasisahau! Je, kama Mzee Mkapa kuna jambo ambalo kwa masusudi au bahati mbaya hakushughulikia wakati wa utawala wake na sasa analiona kwa ukaribu zaidi na umuhimu wake kwa ustawi wa nchi, je akae kimya asiishauri Serikali!!! Upuuzi gani huu!!

Tabia hii ya kuwashona mdomo viongozi wasiongee na kuikosoa Serikali yao ni udikteta wa hali ya juu uliopitiliza. Viongozi wastaafu ni hazina muhimu na haswa nchi inapokumbana na changamoto mbalimbali za kiuongozi kama wakati huu wa uongozi uliopwaya wa kikwete. Ndiyo maana wengi wao bado wanaendela kulipwa mafao au marupurupu manono yanayotokana na kodi ya wananchi.

Kwa mantiki hiyo, namshauri Nape aache siasa zake za majitaka kuwazuia viongozi wetu wastaafu watamke wanachoona kinafaa kwa ustawi wa nchi yake. Anachotakiwa Nape ni kuishauri Serikali ya chama chake kueleza hali halisi na kutoa takwimu zinazojibu hoja iliyotolewa na Mhe. Lowassa na siyo kuwaita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja maneno yasiyo na mbele wala nyuma.
 
Gosbert,
Kwanza haya ni mawazo yako na tafisiri yako binafsi! Sijawahi kuwaza wala kutamani kuwanyamazisha wazee au wastaafu na hata vijana, kwani mie ni muumini wa uhuru wa kutoa mawazo!

Katika majibu yangu kwa mwandishi wa Mwananchi ambae alitaka kujua msimamo wangu baada ya majibu ya serikali kwa swala la ajira nilisema yafuatayo.....
"Pamoja na kwamba msemaji wa hoja ya ajira kwa vijana ni bomu ana uhuru wa kutoa mawazo yake, kwanza si mara ya kwanza analizungumzia hili na kuwaita vijana wasio na ajira ni bomu, hili siliungi mkono kwani hata mtoto ukimwita jina la hovyo linaweza kuathiri tabia na maisha yake.

Lakini pia ni vizuri anapolizungumzia hili alizungumze kwa takwimu badala ya kutoa statement general, takwimu zitasaidia kuonyesha ukubwa wa tatizo au kiasi cha tatizo. Serikali imefanya vizuri kutuonyesha halihalisi ilivyo kwa takwimu.

Serikali ijenge utamaduni huo wa kutoa majibu kila inaposhutumiwa badala ya kukaa kimya au kuchukua muda mrefu sana ndo ijibu.

La mwisho kila anayelaumu na hasa viongozi lazima ajiulize yeyey kafanya nini kulipunguza au kuliongeza tatizo? Katika kijiji chake,jimbo lake, au nafasi kubwa aliyo nayo au aliyokuwa nayo alifanya nini inayoongeza au kupunguza tatizo?!!

Kwa mfano kama wakati wa uongozi wako kuna mambo ulifanya yaliyoongeza tatizo la ajira pengine hata kwa matatizo kama ya ukosefu wa nishati kwa mfano ambayo ingesaidia uwekezaji mzuri ambao ungeongeza furusa za ajira!"

Sasa inawezekana kabisa kwa tafisiri yako haya maneno yanaziba midomo ya wazee wastaafu....

SINA NIA HIYO, SIO MUUMINI WA HILO.
 
"Kwa mantiki hiyo, namshauri Nape aache siasa zake za majitaka kuwazuia viongozi wetu wastaafu watamke wanachoona kinafaa kwa ustawi wa nchi yake. Anachotakiwa Nape ni kuishauri Serikali ya chama chake kueleza hali halisi na kutoa takwimu zinazojibu hoja iliyotolewa na Mhe. Lowassa na siyo kuwaita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja maneno yasiyo na mbele wala nyuma."

Hasa kwenye red,

HIVI NI WAPI NIMEITA WAANDISHI NA KUBWABWAJA KAMA UNAVYODAI?? UNAPOKARIRI KUMTUKANA TU NAPE POPOTE UNAPOTEZA MWELEKEO! SIJAWAHI KUITA WAANDISHI WA HABARI KWA HILO, ACHA KUDANGANYA WATU HAPA NI AIBU KUSEMA UONGO MTU MZIMA.....
 
Gosbert,
Kwanza haya ni mawazo yako na tafisiri yako binafsi! Sijawahi kuwaza wala kutamani kuwanyamazisha wazee au wastaafu na hata vijana, kwani mie ni muumini wa uhuru wa kutoa mawazo!

Katika majibu yangu kwa mwandishi wa Mwananchi ambae alitaka kujua msimamo wangu baada ya majibu ya serikali kwa swala la ajira nilisema yafuatayo.....

Sasa inawezekana kabisa kwa tafisiri yako haya maneno yanaziba midomo ya wazee wastaafu....

SINA NIA HIYO, SIO MUUMINI WA HILO.

Nape sasa umekuwa mwanasiasa zaidi na huongei hali halisi ya watanzania hasa vijana waliopo mitaani. Lowassa hajasema vijana wasio na ajira ni mabomu bali kuwepo na vijana wengi wasio na ajira ni bomu ambalo litakuja lipuka baadae. Tofautisha hii, hakuwaita wao bomu (noun) bali tendo la kuwa unemployed youth ni bomu (verb) na hilo ni ukweli.

Unataka takwimu kujua hili!!? Siamini kama akili yako ni MGANDO kiasi hiki kama ya yule mama Kabaka... Anaelinganisha sijui 75% ya Singida na 25% ya Dsm!!

Oneni ukweli na muufanyie kazi ndio mtaweza washawishi watu na wataamini chama chenu, lakini kudanganya danganya mnazidi poteza credibility mbele ya watanzania vijana ambao angalau mmewapa uwezo wa kuelewa baada ya kuwaanzishia shule za kata.
 
Gwanda gamba!!

images
 
Hasa kwenye red,

HIVI NI WAPI NIMEITA WAANDISHI NA KUBWABWAJA KAMA UNAVYODAI?? UNAPOKARIRI KUMTUKANA TU NAPE POPOTE UNAPOTEZA MWELEKEO! SIJAWAHI KUITA WAANDISHI WA HABARI KWA HILO, ACHA KUDANGANYA WATU HAPA NI AIBU KUSEMA UONGO MTU MZIMA.....
Nape, natambua uzito wa nafasi uliyonayo na umuhimu wake katika maendeleo ya jamii yetu. Maswali yangu ni JE? Ni namna gani unashauriwa Kabla ya kukabiliana na Changamoto za wadhifa wako? Washauri wako wanapatikanaje? Maswali yangu yanatokana na ukweli kwamba wewe binafsi huna uwezo wa kutathmini na hatimae kuwa na mwelekeo wa kimawazo wa jibu la Changamoto nyingi ziananazo kukabili katika kazi yako.
 
Gosbert,
Kwanza haya ni mawazo yako na tafisiri yako binafsi! Sijawahi kuwaza wala kutamani kuwanyamazisha wazee au wastaafu na hata vijana, kwani mie ni muumini wa uhuru wa kutoa mawazo!

Katika majibu yangu kwa mwandishi wa Mwananchi ambae alitaka kujua msimamo wangu baada ya majibu ya serikali kwa swala la ajira nilisema yafuatayo.....

Sasa inawezekana kabisa kwa tafisiri yako haya maneno yanaziba midomo ya wazee wastaafu....

SINA NIA HIYO, SIO MUUMINI WA HILO.

Ndugu Nape,

Nafahamu kwamba wewe ni mjamaa kwa matendo na kauli zako. Naomba usisite kusema ukweli pale unatapotakiwa kutokana na nafasi yako. Tunajua kwamba matatizo ya nchi yetu yanafungamana na namna viongozi wetu wanavyofanya maamuzi katika kutekeleza majukumu yao. Mfano ni kashfa ya Richmond/Dowans iliyopelekea taifa kukumbwa na aibu pamoja na hasara ya mabilioni. Hivi leo tungekuwa na umeme wa kutosheleza mahitaji yetuni Watanzania na wageni wangapi wangewekeza kwenye viwanda? Uwekezaji huo ungeibua ajira ngapi?

Tuache malumbano, binafsi sikubaliani na hoja za Waziri kabaka, ukosefu wa ajira ni tatizo. Kasi ya kulishulikia ni ndogo zaidi kwa sababu ya matatizo ya kimfumo yalichangiwa na viongozi watangulizi, hasa walipoamua kuhalalisha rushwa na ujanja ujanja katika kutekeleza miradi ya serikali. Kama tumeshindwa kuwavua gamba kwa njia ya moja kwa moja lazima tutumie mtindo wa kuwakumbusha makosa yao. Sisi watoto wa wakulima tunaelewa maana ya ukosefu wa ajira. Sidhani kama watoto wa wakubwa wanachagua kuwa watumishi wa serikali! Wanafanya kazi kwenye taasisi zenye mishahara mizuri na pengine wamewezeshwa kujiajiri wenyewe.
 
nape unakubali kuna tatizo la ajira tanzania au hapana?au ajira ni vijana kuuza vocha na line,bidhaa za mchina barabara
 
Sasa unakuja mahali penyewe penye mzizi wa tatizo. Sasa jiulize leo ikitokea analiyeongeza tatizo la umeme nchini kwa kushindwa kusimamia upatikanaji wa umeme wa uhakika basi hata huo mdogo tukaingia kwenye tatizo la malipo ya Richmond na baadae Dowans, pamoja na athari tulizozipata za uwekezaji, analaumu tatizo la ajira!!!!!!!!!

Bahati mbaya au nzuri kipimo cha uwezo wa akili yangu ulichotumia hakitumiwi na wenye akili zao....kwahiyo litabaki dua la kuku tu

Nape, natambua uzito wa nafasi uliyonayo na umuhimu wake katika maendeleo ya jamii yetu. Maswali yangu ni JE? Ni namna gani unashauriwa Kabla ya kukabiliana na Changamoto za wadhifa wako? Washauri wako wanapatikanaje? Maswali yangu yanatokana na ukweli kwamba wewe binafsi huna uwezo wa kutathmini na hatimae kuwa na mwelekeo wa kimawazo wa jibu la Changamoto nyingi ziananazo kukabili katika kazi yako.
 
nape unakubali kuna tatizo la ajira tanzania au hapana?au ajira ni vijana kuuza vocha na line,bidhaa za mchina barabara

Tatizo la ajira lipo na si dogo na wala halipo Tanzania pekeake, lipo dunia nzima. Lakini si la kiliita bomu na wanaolalamikia.....mwalimu alitwambia ukikataa rushwa kwa maneno basi hata sura ifanane na kukerwa na jambo lenyewe!!!
 
Nape mimi sio mwanasiasa wala huwa si mchangiaji sana kwenye issue za siasa.
Napenda tuu unapoongea swala la ajira Tanzania ongelea kama Tanzania na swala la kusema kuwa lipo dunia nzima sidhani kama ni kipimo
Jiulize wewe na sera za chama chako mnafanya nini kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ambao kila mwaka wanamwagwa kutoka vyuoni na sekondari ambao hawana uhakika wa nafasi yoyote ya ajira kwenye private sector au kwenye serikali
Mmetengeneza nafasi ngapi mpya za ajira toka mlipoingia madarakani maana rate ya viwanda kufa imeongezeka sana toka hii awamu iingie madarakani
Viwanda vingi vilivyobinafsishwa vimegeuka magodown ya kuhifadhia bidhaa kutoka china na korea
Je mlalishughulikiaje hilo au mna sera gani kuhusu hilo
Hizi takwimu za waziri wenu hazina lolote maana ukweli watu wanauoana wanaoishi huku mtaani vijana wengi waliomaliza vyuo na sekondary hawana tegemeo lolote la maisha
 
Tatizo la ajira lipo na si dogo na wala halipo Tanzania pekeake, lipo dunia nzima. Lakini si la kiliita bomu na wanaolalamikia.....mwalimu alitwambia ukikataa rushwa kwa maneno basi hata sura ifanane na kukerwa na jambo lenyewe!!!

penye nyekundu hayo nimaneno ya mtu mvivu huwa sipendi kuyasikia nappe ikiwezekana wewe kijana mwenzangu yatoe na UELEZEEE JINSI SERIKALI YAKO INAVYOFANYA JUHUDI KULIONDOA, unaposema dunia nzima wenzetu litatoka libaki kwetu tu, dunia nzima wanafanya juhudi lakuliondoa tunataka sehemu yenu ni ip??
 
Tatizo la ajira lipo na si dogo na wala halipo Tanzania pekeake, lipo dunia nzima. Lakini si la kiliita bomu na wanaolalamikia.....mwalimu alitwambia ukikataa rushwa kwa maneno basi hata sura ifanane na kukerwa na jambo lenyewe!!!

Yaani hata wewe ni kiongozi ndani ya nchi hii!? Kama tatizo la ajira lipo jawabu ni kulitatua, siyo kulinganisha kizembezembe kwamba lipo duniani kote. Pamoja na hayo, kama lipo duniani kote, lets say "tatizo lipo Tanzania na UK". UK the government pay Unemployment benefits to her people. Nyie mnafanya nini kama siyo kupiga mavuvuzela tu kujinufaisha peke yenu? Thinking yako kwa mjibu wa maelezo yako hapo juu...tatizo la ajira lipo na lipo Duniani kote, the inference from your slight cheap premise ni kwamba, kama lipo Tanzania na Duniani kote, therefore its not an issue in Tanzania, liendelee kuwepo tu. Inaonekena hata hujui uko Duniani ulokutaja wao wanadeal vipi na tatizo hilo.
Swali, Je Tanzania inakosa nini mpaka tatizo la ajira hasa kwa vijana liwepo? Wakati unajibu fanya ulinganifu wa resources zilizopo nchini (the vast fertile land, Geological resources, water, vegetation, animals, wind, sun including human resources...Vijana) just few to mention. Kama ni muungwana utasema "Leadership is missing".
NAPE, CCM and all its associates ni Janga la kitaifa. CCM italipeleka Taifa hili pabaya.
 
Sasa unakuja mahali penyewe penye mzizi wa tatizo. Sasa jiulize leo ikitokea analiyeongeza tatizo la umeme nchini kwa kushindwa kusimamia upatikanaji wa umeme wa uhakika basi hata huo mdogo tukaingia kwenye tatizo la malipo ya Richmond na baadae Dowans, pamoja na athari tulizozipata za uwekezaji, analaumu tatizo la ajira!!!!!!!!!

Nape unahitaji kujifunza kutoka kwa viongozi wenzio vijana kama Makamba na Zitto, huwa hawakurupuki, their minds run faster than their mouths! Kupambana na Lowassa hakutakusaidia, you are digging your own grave!
 
Tatizo la ajira lipo na si dogo na wala halipo Tanzania pekeake, lipo dunia nzima. Lakini si la kiliita bomu na wanaolalamikia.....mwalimu alitwambia ukikataa rushwa kwa maneno basi hata sura ifanane na kukerwa na jambo lenyewe!!!
Nape,

Katika jambo ambalo binafsi huwa silipendi ni kutaka kuhalalisha mapungufu yetu kwa kulinganisha au kutoa mfano wa mapungufu hayo hayo yanayotokea katika nchi zingine au maeneo mengine. Inawezekana wenzetu hali ya ajira ni mbaya kwa sababu ya uchache wa rasilimali au fursa nzuri za kiuchumi. Sisi kama Tanzania ni nini tusicho nacho? Tuna ardhi nzuri ya kilimo, mito mingi, tumezubgukwa na maziwa pande zote na mengine ndani kabisa ya nchi, tuna madini ya kila aina na mengine yanapatikana hapa kwetu tu, tuna mbuga za wanyama nyingi, tuna bandari Tanga, Dar na Mtwara bila kutaja za maziwani, tuna misitu, n.k na zaidi ya yote nchi yetu ni tulivu. Kwa fursa hizi, Bw. Nape kweli ni halali vijana wetu wakose ajira!!!! Nape, ni vizuri kukiri kwamba mipango ya serikali ya chama chako cha ccm ni mibovu na hii yote ni kwa sababu ya rais wetu kuendekeza utegemezi kwa wazungu. Wakati mwingine huwa najiuliza hivi kikwete huwa haoni aibu kuzunguka na bakuli la misaada wakati anaowaomba hawana hata robo ya rasilimali ilizonazo nchi yake!! Kijana kama wewe ulipaswa kulisimamia ipasavyo tatizo hili vijana kukosa ajira badala ya kupoteza muda kushindana kwa kauli na Mhe. Lowassa. Hata kama nae ana mapungufu yake, lakini kauli ya Lowassa kuhusu vijana ni sensible na msipoifanyia kazi haki ya nani Mungu shahidi bomu hilo litawalipukia.
 
Anachosema mwandishi wa thread ni kweli. Kuna mtindo mbaya umeanza kujengwa na ccm wa kuponda kila kinachosemwa na viongozi wastaafu hata kama kina mantiki. Njia inayotumika ni kutaja mapungufu ya kiongozi husika ili aogope na kukaa kimya. Tabia hiyo ni ya kipuuzi na ninamwonya Nape aache mara moja. Wenye nchi watakapoichukua nchi yao sijui atakimbilia wapi.
 
Back
Top Bottom