Nape: Sikuwahi sema kuwa Mafisadi wataondolewa CCM baada ya siku 90

Status
Not open for further replies.
Mambo ni mazito kwani siku zote utumwa wa kujitumikisha ni mgumu zaidi kuliko wa babu zetu. Wabunge asilimia kubwa wa ccm wamejikuta siku zote wanabanwa na chama chao kimfumo, na hii sasa ndiyo inajitokeza kwa cdm kwani wenye ownership na chama unaona wanavyomuona shibuda
 
Ni kweli kabisa...mkubwa wanakufanya kama kikaragosi.Wabunge wenu kule mjengoni wanarudisha nyuma harakati zako za kuifanya ccm ikubalike tena,...kwa upeo wa ufahamu wa kawaida huoni kuwa wamekutwisha gunia la misumari?Haya sasa hata mwenyekiti wako ameanza kukutosa live,ameamua kumsafisha AC,means sasa sio gamba tena linalotakiwa kuvuliwa.!Toka huko Kaka sio wakweli hao,wanafiki tu....!
 
Huu ni wakati wa kuchezesha video ya kauli ya Nape, wakati akitamba lazima Mapacha wafukuzwe ndani ya siku Tisini. Hakuna mwenye rekodi ya sauti au video. Bila kuwabana viongozi hawa kwa maneno yao na matendo wataendelea kutuona majuha.
 
Toka hapo awali waliisha mwambia hana uthubutu huyu dogo. Anacheza ngoma asiyoijua, kifupi huyu dogo katolewa kafara!
 
Tayari wamesha 2lia,hapa si ungekuwa umemsikia mwasisi wa ccj analonga but amekatwa break zote na sasa amepaki. Riz1 yeye zamani sana maana alitaka kujichanganya kwa Mtikila akaambiwa huyu anampa shit baba yako itakuwa wewe? Aka2lia. Kuhusu willy yeye ameanza kubadili fikra zake mgando na sasa amekiri kuwa Tanzania haiwezi kuendelea na chama cha magamba...!
 
either way,Nape is dead politically,he jumped into conclusion for something he didin't take time to analyze,.mapacha watatu are the DONS,even his boss player is afraid of,.they are there to stay,i can judge from the support chenge enjoyed yesterday in the HOUSE from those stupid mp's on radar saga,RACHEL are like GODS to ccm,..Nape BEAT IT or you gonna face the THRILLER trying hypocritely to HEAL THE WORLD...
 
wajumbe pendekezo zangu tuache kumuongelea Nape kwani ni mtu asiye na mwelekeo na hawezi kusabababisha jamii ipige hatua yeyote nadhani vyombo vya habari tuache kuandika habari zake awe kama mapuri
 
kwani hujui au nawewe unataka ufungiwe na jm kama alivyofungiwa malaria sugu, kila kitu kinaeleweka
kilichozungumzwa 10 april mwaka huu na makada wa ccm.
NIkifungiwa kwa kusema ukweli itakuwa si ajabu maana ukiiba kuku unafungwa miaka 3 ,ukiiba mabilioni unakuwa huru
 
Hpa Nape hauna hoja kabisa. kwa kuwa mapacha hao wamechafuataswira ya CCM kwa kufuja fedha za umma ambazo wakati wote huu ziko chini ya Serikali inayoongozwa na CCM ingekuwa ni vyema kama umngekuwa unazungumza wakati mapacha watatu hao wameshahukumiwa hapo tungeipongeza CCM kwa ujasiri wa kutumia Sheria kuwatia hatiani. Lakini hizi porojoza siku 90, mara vikao vya CCM, mara Nape kasema hivi n.k haziwezi kuwarejeshea uhai watanzania waliopoteza maisha kutokana na kukosa huduma za afya kwa ukosefu wa fedha kutokana na ufisadi wa watu hawa.

Wakati mwingine kama hauna cha kujisifia na kuisifia CCM bora ukanyamaza.
 
Tuesday, 05 July 2011 21:23
Na Elias Msuya
IMEPITA miezi miwili tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipotangaza mkakati wake wa kujisafisha, maarufu kama kujivua gamba.Katika mkakati huo, CCM ilibadilisha safu yake ya uongozi wa sekretarieti na kuweka viongozi wapya. Hatua nyingine ilikuwa ni kukisafisha chama hasa kutokana na tuhuma nyingi za ufisadi zilizokuwa zikikikumba.

Baadhi ya makada wa chama hicho walitajwa kwa kukiletea sifa mbaya chama hicho kikongwe.
Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho makada hao walitakiwa kutafakari na kujipima na baadaye maamuzi zaidi dhidi yao yangechukuliwa katika kikao kingine cha kijacho cha Halmashauri Kuu.

Tangu wakati huo kumekuwa na maswali kuwa hao makada watachukuliwa hatua lini?
Akizungumza na Mwandishi Wetu, ELIAS MSUYA, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye anajibu hoja hizo pamoja na mambo mengine.Swali: Baada ya kuingia Katibu Mkuu Wilson Mukama alisema baada ya siku 90 makada watatu waliotuhumiwa kuhusika na ufisadi na kukiletea sifa mbaya chama watapewa barua. Na kuna taarifa kuwa Makamu Mwenyekiti (Bara), Pius Msekwa alikutana na watuhumiwa hao na kuteta nao. Hadi sasa mmefikia wapi?
Jibu: Sisi hatukutoa siku 90, zimeletwa na vyombo vya habari. Tulisema kuwa maamuzi yatafanywa kikao baada ya kikao. Suala lilikuja baada ya mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete kusema tukutane mwezi Julai, sasa waandishi wakahesabu miezi mitatu wakapata siku 90.

Sina uhakika Msekwa alizungumza nini na hao watuhumiwa kwa sababu sikuwepo kwenye kikao hicho, ila ninachojua tutakapokutana kwenye kikao tutaangalia yatokanayo na kikao kilichopita.

Kuna njia mbili za kuwasilisha maamuzi kwa wahusika, ama kwa kuitwa na kuelezwa au kwa kupewa barua.
Kwa hiyo tutakapokutana tutafanya njia moja wapo ili kuhakikisha kuwa tunakisafisha chama.

Swali: Lakini kwa kuwa kujivua gamba ilikuwa ni mkakati wa dharura, kwanini msifanye vikao vya dharura vya haraka mkawaondoa watuhumiwa hao ili wasiendelee kukichafua chama, badala yake msubiri ratiba ya vikao vya Halmashauri Kuu?

Source: mwananchi Leo

Nimeamua kuja mwenyewe. Nashangaa wakati mwingine maana ni hapa ndo watu walisema Nape kashazibwa mdomo kama vile yale ni maamuzi ya Nape binafsi.
Jana nimewakumbusha tu watuhumiwa na wapambe wao si busara kujifariji kuwa maamuzi yatabadilishwa nje ya vikao, na vikao vyenyewe ni lazima iwe ama NEC au Mkutano Mkuu(Congres) na si vinginevyo.
Kuna hoja hapa eti kwamba Nape anabwabwaja tu, hakuna vitendo, let's be objective,hivyo vitendo ni vipi? Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi haya itatolewa kwenye kikao kijacho cha NEC na si siku 90 kama wanavyojaribu kueleza hapa. Tumelieleza sana hili la siku,WAANDISHI TENA BAADHI ndo walitafsiri siku tisini kutoka kwenye ratiba ya vikao vya NEC ambavyo Dodoma tulikubaliana tentively tunaweza kukutana July ndo wakahesabu na kusema siku tisini. Lakini hakuna kikao kinakutana exactly kwa muda ulopangwa,kuna flexibility.
Ushauri subirini NEC ikutane mtuseme tukishindwa kufukuza.

SI swala la kudai wala vikao kuamua upya bali vikao VILISHAFANYA UAMUZI NA UAMUZI NI WAJIPIME NA KUONDOKA WENYEWE WASIPOFANYA WATAFUKUZWA NA CHAMA.

SWALA LA LINI NI PERIOD KUTOKA KIKAO KILICHOPITA CHA NEC MPAKA KIKAO KIJACHO CHA NEC, AMBACHO KWA MUJIBU WA KATIBA HUWA KINAKUTANA KILA BAADA YA MIEZI MINNE. Lakini SI LAZIMA IWE MIEZI MINNE KAMILI,KATIBA YA CCM INARUHUSU KUWA NA VIKAO MAALUMU KATIKATI KABLA YA MUDA HUO,HIVYO NEC INAWEZA KUKUTANA KABLA YA MIEZI HIYO KATIKATI KAMA ITAONEKANA IPO HAJA. NA INWEZA IKAKUTANA BAADA YA MIEZI MINNE KUTOKANA NA MAZINGIRA,KWA MFANO NAFASI YA MKITI KAMA IMEBANA TUNAWEZA KUSOGEZA MBELE SO SI SWALA LA SIKU EXACTLY.

ANGALIA HATA BUNGE KUNA MUDA UMEPANGWA LAKINI LINAWEZASOGEZA SIKU ZA KUANZA AU KUMALIZA KUTEGEMEANA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO.

Kikubwa hapa NI KUWA WAHUSIKA WAMEITWA NA KUJULISHWA UAMUZI WA NEC NA KUWA UPO MUDA WA WAO KUTEKELEZA WASIPOFANYA KIKAO KIJACHO CHA NEC NI KUWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI ITAKAYO ONYESHA IMETEKELEZWA KWA KIASI GANI NA KUTEKELEZA SEHEMU YA PILI YA UAMUZI.

KUMBUKA ILISEMWA HAPA JF KUWA UAMUZI HUU HAUTATEKELEZWA NA KUWA HAYO YALIKUWA MANENO (yalitumika maneno makali, machafu) YA NAPE NA CHILIGATI SI UAMUZI WA CHAMA, AKATOKA DR. KIKWETE MWENYEKITI WA CHAMA AKASEMA PALE DIAMOND ALIPOONGEA NA MAASKOFU KUWA ANACHOSEMA NAPE NI UAMUZI HALALI WA CHAMA, WATU WAKAFUMBA MACHO NA MASIKIO NA KUENDELEA KUDAI NI YA NAPE NA KUWA WATUHUMIWA HAWATACHUKULIWA HATUA ZOZOTE HATA KUJULISHWA TU. WAMEITWA NA KUPEWAA UAMUZI WA NEC, WATU WAKAKIMBIA JF, HATA WALE WALIONITUKANA NILIDHANI WATARUDI KUPONGEZA HATUA ILIYOFIKIWA, SIKUWAONA.

NINACHOWEZA KUHAKIKISHIA HAPA UAMUZI HUU WA KUWAWAJIBISHA BAADHI YA WATUHUMIWA HAUTABADILISHWA KWA KELELE ZA BARABARANI NA SARAKASI ZA WATUHUMIWA, TUMETHUBUTU KUAMUA, TUTATEKELEZA MAAMUZI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Adui wa CCM ni mwana CCM mwenyewe. Urais 2015 utawagombanisha sana,na mwisho mtachemsha.
 
Dogo Nape unahitaji speed governer into you mouth. Unakurupuka sana, hivi unaweza kumbembeleza kobe kuvua gamba. unapoteza muda tu. CCM bila gamba haiwezekani lakini CCM bila Nape inawezekana.
 
SI swala la kudai wala vikao kuamua upya bali vikao VILISHAFANYA UAMUZI NA UAMUZI NI WAJIPIME NA KUONDOKA WENYEWE WASIPOFANYA WATAFUKUZWA NA CHAMA.

SWALA LA LINI NI PERIOD KUTOKA KIKAO KILICHOPITA CHA NEC MPAKA KIKAO KIJACHO CHA NEC, AMBACHO KWA MUJIBU WA KATIBA HUWA KINAKUTANA KILA BAADA YA MIEZI MINNE. Lakini SI LAZIMA IWE MIEZI MINNE KAMILI,KATIBA YA CCM INARUHUSU KUWA NA VIKAO MAALUMU KATIKATI KABLA YA MUDA HUO,HIVYO NEC INAWEZA KUKUTANA KABLA YA MIEZI HIYO KATIKATI KAMA ITAONEKANA IPO HAJA. NA INWEZA IKAKUTANA BAADA YA MIEZI MINNE KUTOKANA NA MAZINGIRA,KWA MFANO NAFASI YA MKITI KAMA IMEBANA TUNAWEZA KUSOGEZA MBELE SO SI SWALA LA SIKU EXACTLY.

ANGALIA HATA BUNGE KUNA MUDA UMEPANGWA LAKINI LINAWEZASOGEZA SIKU ZA KUANZA AU KUMALIZA KUTEGEMEANA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO.

Kikubwa hapa NI KUWA WAHUSIKA WAMEITWA NA KUJULISHWA UAMUZI WA NEC NA KUWA UPO MUDA WA WAO KUTEKELEZA WASIPOFANYA KIKAO KIJACHO CHA NEC NI KUWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI ITAKAYO ONYESHA IMETEKELEZWA KWA KIASI GANI NA KUTEKELEZA SEHEMU YA PILI YA UAMUZI.

KUMBUKA ILISEMWA HAPA JF KUWA UAMUZI HUU HAUTATEKELEZWA NA KUWA HAYO YALIKUWA MANENO (yalitumika maneno makali, machafu) YA NAPE NA CHILIGATI SI UAMUZI WA CHAMA, AKATOKA DR. KIKWETE MWENYEKITI WA CHAMA AKASEMA PALE DIAMOND ALIPOONGEA NA MAASKOFU KUWA ANACHOSEMA NAPE NI UAMUZI HALALI WA CHAMA, WATU WAKAFUMBA MACHO NA MASIKIO NA KUENDELEA KUDAI NI YA NAPE NA KUWA WATUHUMIWA HAWATACHUKULIWA HATUA ZOZOTE HATA KUJULISHWA TU. WAMEITWA NA KUPEWAA UAMUZI WA NEC, WATU WAKAKIMBIA JF, HATA WALE WALIONITUKANA NILIDHANI WATARUDI KUPONGEZA HATUA ILIYOFIKIWA, SIKUWAONA.

NINACHOWEZA KUHAKIKISHIA HAPA UAMUZI HUU WA KUWAWAJIBISHA BAADHI YA WATUHUMIWA HAUTABADILISHWA KWA KELELE ZA BARABARANI NA SARAKASI ZA WATUHUMIWA, TUMETHUBUTU KUAMUA, TUTATEKELEZA MAAMUZI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Hapo kwenye red maana yake nini (Double standard?)?
yaani hao baadhi ya watuhumiwa ni wale ambao hawana ndugu serikalini?
na ni kwa nini iwe ni baadhi? wengine wanaachwa kwa sababu ya nini? au ndo kulindana?
Hamwoni kuwa mnatudanganya tukiona? au mnafikiri sisis ni wajinga?
Aliyekuwa amekomalia suala la miezi mitatu si ni wewe?
Mbona unajikanyaga?

Mmekwesha.
 
Yale yale.. hekaya za abunuwasi!

Nape na Mukama ni vidagaa tu ndani ya bwawa kubwa ambalo wafalme ni Papa, Nyangumi na Mamba (Namaanisha mapacha watatu). Apende sipende, kusema hao jamaa waondoke ilikuwa ni kauli ya kujitafutia umaarufu kwenye media na kafanikiwa sana. Kibaya alisahau kuwa siku 90 ni chache na sasa kaanza kuleta habari za miaka 4. Ndugu yangu Nape nakushauri uwaige wenzio kina January Makamba, chuma chako ndani ya CCM usepe. Huwezi kuibadilisha CCM kwa maneno ya kuropoka kwenye vyombo vya habari wakati unajua wazi walioko juu yako wote akiwemo mwenyekiti ni wachafu kupitiliza. Vuta mafao alafu uangalie ustaarabu au kama uko that serious nakushauri uhame chama.

OVA!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom