Nape Nnauye: Kila nifanyalo wanaona kama namsema Rais hili linaudhi na kuniumiza sana

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kusema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakimkazwa na kumuudhi kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakitafsiri vibaya vitu vitu anavyoweka wakidai anamsema Rais.

Nape Nnauye alisema hayo wiki iliyopita alipoongea na mwandishi wa EATV na kusema baadhi ya watu wamekuwa wakichukua baadhi ya vitu anavyoweka kwenye mitandao yake ya jamii na kuanza kusambaza wakimtuhumu kuwa anamsema Rais kitu ambacho anadai si kweli.

Mbunge huyo wa Mtama amesema kitendo hicho cha watu kuchukua maneno yake na kuanza kusema anamzungumzia Rais ni kitu ambacho kimekuwa kikimuumiza sana siku hizi.

"Maana watu kila nifanyalo wanaona kama namsema Rais hili linaudhi na kuniumiza sana siku hizi" alisisitiza Nape Nnauye
 
Back
Top Bottom