Nape Nnauye atoa Tamko Maalum la CCM kuhusiana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini

[video=youtube_share;A-Jrd58cywo]http://youtu.be/A-Jrd58cywo[/video]
============================== ============================== ======================

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka watendaji wote waliosababisha kuharibika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya maeneo nchini wachukuliwe hatua kali.

Kimesema, watendaji hao wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kilichotokea ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika huku ikifahamika wazi kwamba tukio la uchaguzi huo ni kubwa na muhimu sana kwa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, kulingana na kosa lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.

"Kwa mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vicheche?" alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena kubaini aliyevurunda?".

"Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.

Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM imewagaragaraza vibaya.

Nape amesema, katika uchaguzi huo , CCM imepata zaidi ya asilimia 85 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 75 licha ya kwamba Chadema wanao wabunge wawili katika mkoa huo.

"Katika mazingira ya sasa ambayo vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu kuungana, asilimia 85 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.

"Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia. Katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape.

"Hata hivyo inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa 22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania hata kufikia asilimia 40 kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka zaidi ya 22".

Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa.

Nape wew nani asiye kujua kwa kubwabwaja..Unasahau ulivyokua ukinunua Dad poa hapa Arusha na kulala nae Pale Ngurudotto Hotel????
Kwanza ni mapema sana kutoa tathimn kwasababu matokeo meng hayajatumwa TAMISEMI na Sehem nyngn zaid ya 30% uchaguz haujafanyika...
 
Ukweli utaendelea kuwa ni ukweli.

Ndoto zitaendelea kuwa ni ndoto.

Baba wa demokrasia ataendelea kuwa baba wa demokrasia.

CCM bado inayaenzi maneno ya mwasisi wake aliposema, ‘’Bila ya CCM imara Tanzania itayumba’’.

Kazi ya CCM ni kupambana na changamoto zinazoibuka siku hadi siku.

CCM imesikia sauti za wananchi kupitia sanduku la kura ambao wamepiga kura kwa pande zote.

Mwananchi anayepiga kura ya hapana anakuwa na maana nyingi katika kura yake, kwa sasa kazi ya CCM ni kunyambua mantiki na maana ya kura za hapana kwa faida ya chama na taifa kwa ujumla.

Mkuu Mwanadiwani hongera kwa huo ushindi unaosema wa kishindo! Vipi unazungumziaje na ushindi wenu wa 42% wa bila kupingwa na hujuma kwa baadhi ya maeneo kupelekea nyie kushinda kwa hila? :sick:
 
toa upuuzi hapa, adanganywi mtu hapa, mlisema mtashinda kwa kishindo leo mnaanza kujitetea eti demokrasia;wacha kujipa hope kifupi ni kuwa UKAWA ni kali yenu.
Hata kama ukitoa povu pipa moja ukweli unabaki palepale kwamba viongozi wa CCM wa serikali za mitaa kipindi hiki 42% ''wameteuliwa'' na TAMISEMI badala ya kupigiwa kura na wananchi.
 
Chama cha malori
Chama cha mapingamizi
Chama cha mafisadi
Chama cha wezi/majambazi
 
Akiwa anatoa tathmini kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa Nape kasema wote waliovuruga Uchaguzi wawajibishwe.

Moja ya makosa ambayo Nape aliyatolea mfano, Ni kuwa kuna Karatasi za kupigia Kura ambazo zilikuwa na Picha ya Mgombea wa Cdm lkn imeandikwa Ccm.

Sasa ninachoshangaa ni hichi. Katika Uchaguzi wa vijiji wakati nilipoenda kupiga kura sikuona Picha za wagombea bali ni majina tu na sehemu ya kuweka tiki kwa mgombea unayemtaka.

Sasa mimi nauliza, je ni kwa nini karatasi za kupiga kura zilichapishwa zingine ziikiwa na Picha na zingine bila Picha?.

Mimi nashauri kuwa Waziri Tamisemi aachie ngazi mara moja kwa huu Uzembe. Hii ni aibu kubwa sana kwa Serikali Sikivu ya Ccm.
 
Hii stori ya Nape naweza kuiweka hivi....Sizitaki mbichi hizi..............Hii ni baada ya kuzikosa.
 
Habari wana jf,
Jana nimemsikia Nape akisema wana asilimia 84 sasa sijajua zinapatikan vipi, kwa mfano katika halmashauri ya Mbulu kuna kata zifuatazo ambazo ccm wameshindwa vibaya:
kata ya haydom(vijiji 6) CHADEMA-5, CCM-1 vitongoji vyote CHADEMA na wajumbe wote CHADEMA
Kata ya Dongobesh, vijiji, vitingoji wamebeba CHADEMA
Kata ya Tumati(vijiji-3) vyote wamechukua CHADEMA
Kata ya Ayamaami(vitongoji-7) CHADEMA-5,CCM-2. Hivyo ni kwa uchache tu bado zingine sijaweza kuweka hapa, ikumbukwe kuwa chadema haikuwa kiti hata kimoja katika kata ya Haydom Leo wameweza kuchukua karibu vyote.
Sasa Bw. Nape ajiangalia upya yasije kumkuta kama ya Makamba na Mkama maana nimewakuta makada wa ccm juzi mahali wakilaumiana kwa matokeo mabaya licha ya kuleta FFU kutoka Babati na mapingamizi yaliyosimamiwa na DC
 
Bila kusaidiwa na polisi, kuwahonga wagombea wa upinzani wajitoe, kuweka mapingamizi na mkurugenzi kuyakubali mgepata 30% subirini mwaka ujao mtakiona cha mtema kuni.

Ukweli utaendelea kuwa ni ukweli.

Ndoto zitaendelea kuwa ni ndoto.

Baba wa demokrasia ataendelea kuwa baba wa demokrasia.

CCM bado inayaenzi maneno ya mwasisi wake aliposema, ‘’Bila ya CCM imara Tanzania itayumba’’.

Kazi ya CCM ni kupambana na changamoto zinazoibuka siku hadi siku.

CCM imesikia sauti za wananchi kupitia sanduku la kura ambao wamepiga kura kwa pande zote.

Mwananchi anayepiga kura ya hapana anakuwa na maana nyingi katika kura yake, kwa sasa kazi ya CCM ni kunyambua mantiki na maana ya kura za hapana kwa faida ya chama na taifa kwa ujumla.
 
Habari wana jf,
Jana nimemsikia Nape akisema wana asilimia 84 sasa sijajua zinapatikan vipi, kwa mfano katika halmashauri ya Mbulu kuna kata zifuatazo ambazo ccm wameshindwa vibaya:
kata ya haydom(vijiji 6) CHADEMA-5, CCM-1 vitongoji vyote CHADEMA na wajumbe wote CHADEMA
Kata ya Dongobesh, vijiji, vitingoji wamebeba CHADEMA
Kata ya Tumati(vijiji-3) vyote wamechukua CHADEMA
Kata ya Ayamaami(vitongoji-7) CHADEMA-5,CCM-2. Hivyo ni kwa uchache tu bado zingine sijaweza kuweka hapa, ikumbukwe kuwa chadema haikuwa kiti hata kimoja katika kata ya Haydom Leo wameweza kuchukua karibu vyote.
Sasa Bw. Nape ajiangalia upya yasije kumkuta kama ya Makamba na Mkama maana nimewakuta makada wa ccm juzi mahali wakilaumiana kwa matokeo mabaya licha ya kuleta FFU kutoka Babati na mapingamizi yaliyosimamiwa na DC

Ebu ficha ujinga na upumbavu wako unaozeekanao,mfano unachukulia vitongoji vichache toka mkoa wa Arusha ambao hauna hata watu milion 3 kwa Tanzania yenye watu zaidi ta milioni 40.Halafu jiulize CCM imepita maeneo mangapi bila kupingwa,maeneo mangapi imechaguliwa kwa kura za kutosha halafu gawaneni vitongoji na mitaa iliyobaki kwa vyama vyote wa upinzani CUF,TLP,CHADEMA,NCCR n.k.
Maelezo ya Nape yanatokana na takwimu sahihi za uchaguzi toka TAMISEMI wewe unakuja na hisia.
 
Mlivyochachawa mnajidanganya na takwimu zenu mnadhani Watanganyika ni wajinga,Tsunami laja kwenye kura ya maoni ya katiba (kama mtakuwa na ujasiri hata wa kuruhusu iwepo baada ya kimbuga hiki) na October 2015! Tutaheshimiana tu
 
keshi ya swala simba hawezi kutoa suruhu mkuu manjitekenya hapo juu kunatakwimu kutoka mbozi mashariki imepotoshwa kabisa sasa hizo porojo projects za kutafutia political sympathy haziwasaidii mko very desperate.....
 
Mlivyochachawa mnajidanganya na takwimu zenu mnadhani Watanganyika ni wajinga,Tsunami laja kwenye kura ya maoni ya katiba (kama mtakuwa na ujasiri hata wa kuruhusu iwepo baada ya kimbuga hiki) na October 2015! Tutaheshimiana tu

umeshituka mkuu hata mbozi wamedanganya takwimu balaaa
 
Nape wew nani asiye kujua kwa kubwabwaja..Unasahau ulivyokua ukinunua Dad poa hapa Arusha na kulala nae Pale Ngurudotto Hotel????
Kwanza ni mapema sana kutoa tathimn kwasababu matokeo meng hayajatumwa TAMISEMI na Sehem nyngn zaid ya 30% uchaguz haujafanyika...

Mambo ya dada poa yametoka wapi hapa?
 
nape unamkumbuka waziri wa habari wa sadamu husein wakati marekani wanaipga iraq

tarek Aziz ningependa twende na nape na kinana hadi 2015 maana ukawa wakisema jambo wao pamoja na mwingulu wanaenada kuthibitisha badala ya kukanusha na kujifanya wanakemea wananchi hawaamini hilo la kukemea mfano magamba yallishia wapi? mawaziri mizigo mnaimba weee wanachi wanawaona wakidunda hawawezi kuwaamini
 
Back
Top Bottom