Nape Nnauye anatarajiwa kwenda Houston -USA kusuluhisha mgogoro wa Tawi la CCM

Unafikiri chadema hii ..ccm tuko huru

wewe huwezi thubutu kumsema mbowe unaondolewa kwenye chama (dictators)

Ha ha ha Afadhali kuondolewa Kwenye Chama, Nasikia Dogo akikatama Wasaliti Anashikisha Ukuta LoL! Kweli Nape Mwendawazimu sasa Wale Chipukizi si atawamaliza
 
Ya magamba wa hapa nchini yamemshinda, ndio atayaweza ya Houston? au anataka kusafiri tu?
 
Goddamn bastard....kwani mapaka sasa amefanya nini kwa migogoro ya ndani?
Halafu january anafanya kazi gani?
This country needs me.
 
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi anategemea kusafiri kwenda nchini Marekani mwishoni mwa mwezi wa kumi. Akiwa nchini Marekani atakuwa na kazi ya kusuluhisha mgogoro wa Tawi la CCM Marekani lenye makao yake makuu jijini Houston na lisilo na wanachama wengi nje ya jiji la houston.

Tangia kuanzishwa kwa Tawi hili limekuwa likikabiliwa na migogoro mingi ya kiutawala, na kushindwa kuwa na viongozi kwa muda sasa. Chanzo cha habari kinasema chanzo cha migogoro ni uchu wa madaraka, kujuana na undugu unaenziwa na wanachama wachache waliopo. Ujio wa Nape kwenye suluhu unaonekana ni neema kwa baadhi ya kambi kwani wanategemea kama ilivyo ada atachagua kuegemea upande huku baadhi ya mafungu yakitupwa pembeni. Mwanzilishi wa Tawi ameshapigwa pini na kuwekwa pembeni huku wajumbe wakizozana na kushindwa kufanya uchaguzi.

Nape akiwa na ujumbe wa kuvua watu magamba anakibaraua cha kuwavua magamba wanachama wenzeka wa Houston ambao ni wachache kuliko katiba inavyohitaji uwepo wa tawi.

Tawi hili la CCM jijini houstoni limekuwa likikumbana na vizingiti vingi ndani ya jamii ya wana-Houston wengi wao wakionyesha kutokuitaka CCM, na kuamini kila aliyekwenye Tawi ni kwa maslahi yake binafsi kwani hata wao kwa wao wameshindwa kuonyesha nini wanakitaka.

Maisha ya Watanzania ndani ya Tanzania na sababu za wengi kuondoka Tanzania kwa sababu ya kuzorota kwa uchumi, kushindwa kwa utawala wa CCM kutoa haki, ajira na elimu bora ndio sababu za wengi kuondoka nchini. Ajira za kujuana na maendeleo duni huku umeme ukiwa kama bidhaa adimu kuliko huduma. Viongozi wakiwa ni wezi na kuenzi hujuma badala ya haki, wajibu na kazi, huku wezi mapapa wakiwa mitaani na dagaa ndio wakipata mijeledi keko na segerea.

Utawala huu wa CCM umekuwa ni utawala dhalimu kwa maisha ya Mtanzania na kuwafanya vijana wengi kukosa imani na kila kiongozi wa CCM kwani ni viongozi mshahara na rushwa.

CCM ikiwa imeshindwa kusimamia hata ahadi zake yenyewe, CCM imeshindwa kupambana na rushwa na wizi wa fedha za umma. Nape amekuwa akiimba wimbo wa kuvua gamba wakati kilichotakiwa ni kuwafungulia mashtaka wote wanaotuhumiwa na ufisadi na kuacha sheria zichukue mkondo. Kweli leo chama tawala kinacheza mchezo wa kuigiza, kimekubali kuwa kina mafisadi halafu kinabembeleza mafisadi waondoke madarakani yaaishe, na Nape kwa sababu alijua watanzania hawajui kuhoji akawapelekea wimbo kuvua gamba. Fisadi anapelekwa kwa DPP mahakamani na segera. Sijawahi sikia duniani kunaswala la suluhu na wezi wa mali ya umma. CCM mnakiri kuwa hao ni wahujumu, wezi, na mafisadi. Sasa mwanasheria mkuu, mahakama, Dpp, takukuru, cid , usalama wa taifa wanafanya nini mpaka mfanye hujuma siasa???????


Sheria zisipofuatwa kwa sababu yeyeote ile ni maafa kwa taifa

Mambo yenyewe kama ndio hivi huko H-Town basi kwa mtaji huu naona Mange Kimambi aliongea point wakati alipowapaka wabeba box ughaibuni kuwa hawana nyimbo wala gitaa!!
 
hayo matawi huko ughaibuni yana faida gani? Mbona sijasikia matawi ya republicaan wala labor hapa bongo? Halafu kenya uganda na kwingine kuna watanzania pia. Mbona sijasikia matawi ya ccm kenya wala uganda. Mmekosa kazi enyi magamba.

Na huyu nape anafunga safari kabisa kwenda huko. Labda anaenda kwenye matibabu maana nasikia ana stress za kufa mtu, kisa ccm
 
Hawa magamba siasa zimewapofosha macho na kudumaza akili kwani mambo ya chama hayatakiwi yakavuka mpaka hadi ubalozini nchi za nje. Balozi kuwa kada wa chama hakatazwi lakini utendaji na utoaji huduma mbali mbali hautakiwi uwe na itikadi. Wao wacha waendelee kufungua matawi balozini ila wawe na angalizo. Waende ubalozi wa Zambia hapa nchini wamuulize mama wa watu kwanini ametolewa baru na utawala wa Michael Sata. Hayo hayo mambo ya kumpigia chapuo na kampeni Rais aliyeondolewa kwa kura (Banda) kutumia kodi za wananchi. Mwenzio akinyolewa wewe tia maji. Magamba angalieni angani kumepambazuka na jua hilooo. MUNGU ibariki Tz.
 
Back
Top Bottom